Tanzania inajengwa na nani?

herrypeter1

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2009
Posts
223
Reaction score
30
Nilipata kuwepo katika ofisi moja ya serikali katika maongezi ya apa na pale mtu mmoja akuliza swali
TANZANIA INAJENGWA NA NANI?
baada ya kuuliza kila mmoja alikuwa akisema yake wengine walisema tanzania inajengwa waandi,
wengine walianza kuelezea toka Tanzania ilipotoka ila kuna mmoja alinishangaza sana
ALIPOSEMA TANZANIA INAJENGWA NA mikopo....


ivi jiulize swali vp kuusu shule za kata zisizo na madawati, Je tunasubiri serikali ije inunue madawati?
au ndo tunasubiri watu wa wamerekani waje kununua ayo madawati, vp tukiandamana shule zisizo na ubora
za kata zifungwe,

swali ni kwako JE TANZANIA INAJENGWA NA NANI?
ni VIPI UNASHIRIKI KUIJENGA TANZANIA?
NA NI VIPI UNASHIRIKI KUIBOMOA TANZANIA?
 
huwezi kuongelea maendeleo bila kushirikisha sera za chama kinachoongoza nchi na upeo viongozi wake wote
 
Tanzania inajengwa na watanzania ambao ni walala hoi. Wapo maofisin au mashambani wakijitoa jasho ajili ya watanzania wenzao. Na ukumbuke kuwa kuna nguvu ambayo kubwa zaidi ya wale wasiojali watanzania wenzao na kujali nafsi zao ambao wananyonya jasho la walala hoi. Unapozungumzia maendeleo ni lazima utafakari kuwa nini kinacho rudisha nyuma maendeleo ya nchi yenye rasilimali ambazo tayari zinavunwa kwa faida ya makampuni na walio idhinisha uvunwaji wa hizo rasilimali bila ya kufikiria wenzao na kujinufaisha matumbo yao. Tafakari ni nini kinarudisha nyuma maendeleo ya Tanzania hata baada ya miaka 50 ya UHURU.

Imagination is more important than knowledge. For knowledge is limited, whereas imagination embraces the entire world, stimulating progress, giving birth to evolution.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…