Imekua kawaida sana, kwa vijana wengi pengine hata wazee ambao kwa namna fulani bado hawajafanikiwa kimaisha, kutumia hali ya kisiasa na kiuchumi kama kikwazo cha wao kutofikia malengo yao. Imefika hatua kumezuka hadi misemo ikisadifu fikra zao kuonyesha vile ilivyo vigumu kufanikiwa kwa Mtanzania anaeanzia chini. Huenda misemo kama "bongo bahati mbaya", 'bongo nyoso" isiwe migeni sana kwako, kama ni migeni pia, jua ipo mitaani na inasadifu hicho nilichokiandika awali.
Sikatai kwamba hali tuliyopo sasa kiuchumi, kijamii na kisiasa nchini, haishabihiani na rasilimali zetu na umri wa Tanzania kama Taifa huru, Ilipaswa tuwe bora zaidi. Kwa hili tunaweza peleka lawama moja kwa moja kwenye mfumo mzima wa uongozi uliotufikisha hapo tulipo. Tunathamini mazuri waliyoyafanya lakini bado wana jukumu la kuhakikisha rasilimali za taifa zinamnufaisha mwananchi bila kujali itikadi za chama, kabila au dini.
Swali lipo kwa upande wetu (wananchi). Je, tumetimiza majukumu yetu, kwa maendeleo yetu binafsi na taifa kwa ujumla? Au tunatumia makosa ya mfumo uliopo kama kinga ya Sisi kutofanikiwa. Pengine sisi ndio tulaumiwe zaidi kwakua tunahusika moja kwa moja kuruhusu mifumo iliyopo itukwamishe. Ukweli ni kwamba katika hali yeyote uliyopo iwe kiuchumi, kitaaluma au maendeleo binafsi, unahusika asilimia mia kua hapo ulipo.
Binafsi siamini katika kumtafuta mchawi ni nani, kutupiana lawama au kutia huruma, Bali juhudi binafsi katika kupambania jambo unaloliamini katika njia sahihi.
Fikiria kuhusu watu binafsi waliopambania ndoto zao katika hali hii hii ambayo wewe unaitumia kama kichaka cha kutofanikiwa, Tanzania ilitambulika kupitia wao, Hawakutambulishwa na Tanzania. Wapo ambao mifumo ya kisiasa ilikataa kuwatambulisha kama Watanzania mpaka pale walipofanikiwa, ndipo ililazimika Tanzania itajwe kupitia wao. Mchezaji wa timu ya taifa ya Denmark mwenye asili ya Tanzania (Yussuf Yurar Poulsen) ni mfano mzuri wa wapambanaji wa namna hiyo.
Fikiria kuhusu utumbuizaji wa Diamond Platinum kwenye uzinduzi wa fainali za Afcon Januari 2017, au Ushindi wa Idris Sultan kwenye shindano la Big brother Africa 2014. Wote hawa, hawakushawishiwa na mazingira rafiki, bali ndoto zao na hatimaye Tanzania iliwajitaji na waliiwakilisha vyema.
Pengine mambo ya kiburudani sio kipaumbele chako,unaweza ukaona hoja hii Haina mashiko. Lakini vipi kuhusu mchango wa Hayati Reginald Mengi katika kusaidia watu wenye uhitaji mbalimbali? Labda yeye alikua na pesa nyingi, je wewe kwa kiwango cha pesa ulichonacho umesaidia vipi watu wenye mahitaji maalumu, Au sio jukumu lako?
Kiuhalisia, katika mifano niliyotoa hapo awali ni dhahiri, wahusika walifanya kitu kwa ajili ya Tanzania kuliko vile Tanzania ingeweza kufanya kitu kwa ajili yao. Hata wewe unaweza kufanya hivyo katika hali yeyote ile, Usitumie vikwazo kama Kinga ya wewe kutofanikiwa.
Kuna usemi unasema "Maji yale yale(ya moto) yanayolainiasha kiazi, ndio yanafanya yai liwe gumu". Kwahiyo tatizo sio vitu vya nje(maji) bali vile umeumbwa kukabiliana navyo ndio kutaamua uwe imara au utie huruma, baada ya kupita katika changamoto fulani.
Tanzania bado ni mbichi, sekta nyingi bado hazijafanyiwa kazi vile inapaswa. Hii inatupa faida kufanikiwa zaidi au haraka ukilinganisha na wananchi kutoka nchi zilizokwisha endelea, kama utajitoa muhanga kufanyia kazi maeneo ambayo hayajaguswa au yameguswa kidogo. Ninaweza nikakupa mifano kadhaa.
Kazi ya "mpangilio wa ndani ya nyumba" maarufu kama (interior design). Ni kitu ambacho kwa wenzetu kama Kenya na Afrika ya Kusini wamekifanya kwa muda mrefu, lakini kwetu sio sekta iliyokomaa, Sisi tumezoa ukisha maliza kujenga nyumba au ofisi, unapanga vitu vyako tu maisha yanaendelea, Lakini kumbe mpangilio wa ndani ya nyumba ni sanaa na waliojitoa kufanyia kazi katika sekta hiyo wanapata kipato na upatikanaji wa kazi ni rahisi ukilinganisha na nchi nyingine.
Uongezaji thamani wa bidhaa ni mfano mwingine wa sekta inayokua kwa Kasi hapa Tanzania, ambayo unaweza ukatumia fursa hiyo vizuri kuongeza kipato chako. Kipindi cha nyuma ilikua nadra sana kukutana na bidhaa ya mjasiriamali Mtanzania imefungashwa kisasa na kibandiko cha taarifa ya bidhaa na mtengenezaji. Mara nyingi bidhaa za aina hii zilitoka Kenya, kwetu hapa ilikua ni makampuni makubwa yanafanya hivyo. Licha ya kwamba mabadiliko ya teknolojia na usafiri(kimataifa) yamechangia maendeleo haya hatuwezi kuacha kusifu watu binafsi walioona izo fursa na kuchukua hatua kupambania ndoto zao. Wapo waliopiga hatua zaidi Hadi kuuza bidhaa zao nje ya nchi, Hivyo kuitambulisha vema Tanzania katika sekta ya viwanda.
Ukweli ni kwamba unapopambania maendeleo yako binafsi, unapambania maendeleo ya taifa kwa ujumla, Fikiria wewe ni mjasiriamali na umeajiri watu kadhaa, unakuwa umepiga ndege wawili kwa jiwe moja, umeongeza kipato chako na pia umetoa ajira kwa wananchi wa Tanzania. Au umefanikiwa na umeweza kurudisha kiasi Fulani kwa jamii yenye uhitaji, unakuwa umejijenga kiroho (kwa dini zote) papo hapo umeisaidia Tanzania kwenye watu wenye mahitaji maalum.
Chukua hatua Sasa! Acha kulalamika. Amka nenda kapambanie ndoto zako, Tanzania ijivunie uwepo wako. Anza na ulicho nacho, jiboreshe kila siku, pokea maoni na uyafanyie kazi(chanya), Kikubwa zaidi baki kwenye mstari.
Sent from my HWV31 using JamiiForums mobile app

Upvote
0