MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Hii inatia huruma na hasira japo sio Mtanzania, yaani dah! Kibaya zaidi wote hao wameingizwa kinyemela na Watanzania wenyewe.
Watu mnapigwa kulia kushoto hadi namhurumia mkulu wenu japo anapiga makelele sana dhidi ya majizi, sijui kama mnamskliza kweli, mfumo wa ufisadi Tz umekita mizizi mpaka basi, sio kazi ya mtu mmoja ategemewe kufumua....ipo siku mtakubali kuiga Kenya na kupata katiba mpya ili asitegemewe mtu mmoja kwenye vita dhidi ya ufisadi
--------------------------------------
Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkoa wa Geita imewakamata raia 100 kutoka China wakituhumiwa kuendesha shughuli za uchimbaji wa dhahabu kinyemela katika mgodi wa dhahabu wa Eagle Brand uliopo Kata ya Magenge Mkoani Geita.
Operesheni hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa wa Geita, Mhandishi Robert Gabriel amesema watapita kwenye migodi yote usiku na mchana ili kuwakamata wageni wanaofanya kazi kinyemela.
Afisa Kazi Mkoa wa Geita, Bw.Mohamedi Majaliwa amesema wageni walioingia nchini kinyume na sheria watalipa faini Shilingi Milioni kumi pamoja na kifungo cha miaka miwili jela kwa kukiuka sheria ya ajira.
Msimamizi wa mgodi huo, ambaye ni raia wa kigeni amekiri kuwa na wafanyakazi hao bila kibali akieleza kuwa utaratibu wa kutafuta vibali unaendelea.
itv.co.tz

Wachina 100 wanaswa wakichimba dhahabu kinyemela Geita.