Tanzania inapewa misaada zaidi na Uingereza (DfID) sawa na nchi 6 za Ulaya mashariki pamoja!

Tanzania inapewa misaada zaidi na Uingereza (DfID) sawa na nchi 6 za Ulaya mashariki pamoja!

abudist

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2009
Posts
850
Reaction score
781
Waziri Mkuu wa Uingereza ameazimia kuivunja idara ya kimataifa ya misaada na maendeleo Department for International Development (DfID). Kwa kuona inatumia pesa bila ufanisi na Uingereza haifaidiki.

Na moja ya nchi iliyotajwa kufaidika zaidi ni Tanzania kuliko hata nchi za ulaya mashariki ambazo pia zinapata misaada hiyo. Kumbe sisi tunapata misaada mingi ya huyu 'Beberu' lakini pia hata hatuambiwi na serikali yetu? Au ndiyo Baniani mbaya kiatu chake dawa? Dah na hiyo misaada tunapewa bure siyo mikopo aghali
ya wachina.

Hapa chini ni baadhi ya maneno ya Waziri Mkuu Boris Johnson:

"Kwa muda mrefu sana, misaada ya nje ya Uingereza imekuwa kama eneo kubwa la pesa angani, ambayo hufika bila kumbukumbu yoyote ya masilahi ya Uingereza," Waziri mkuu alisema.
.
Johnson alihalalisha uamuzi huo, akisema: "DfID inasimamia Ofisi ya nje zaidi ya mara nne na bado hakuna mtu anayefanya uamuzi katika idara yoyote anaweza kuungana juhudi zetu au kuchukua muhtasari kamili."

Aliongeza: "Tunatoa msaada mkubwa kwa Zambia kama tunavyofanya kwa Ukraine, ingawa mwisho ni muhimu kwa usalama wa Ulaya. Tunatoa msaada wa mara 10 kwa Tanzania kama tunavyofanya kwa nchi sita za Balkan za magharibi, ambazo zina hatari ya kujiingiza katika Urusi. "

Source: Three ex-PMs attack plan to merge DfID with Foreign Office
 
Mkuu UK inaisaidia sana Tz. Ila naona huko tuendako na sakata hili la covid19 plus uchaguzi unaokuja na mwenedo mzima wa serikali ya awamu ya 5 misaada hii huenda ikaanza kupungua kwa Tz. Mwisho wa siku wanaoathirika ni waTz wenyewe maana kuna ajira nyingi zinaenda kupotea na nyingi ambazo zingeweza kuwepo siku za mbele huenda zisiwepo tena. Vilevile serikali itakosa kodi nyingi mfano PAYE, SDL WHT hizo ni kwa uchache tu. Kiukweli nchi hii inapoelekea waTz wajipange sana maana.
 
Ameona bajeti ni trillion 35 na ushee halafu hatuna hata nusu yake.. Anajua soon tutaanza kutembeza bakuli
 
Kwa hiyo unalilia "misaada" sio?
 
Ameona bajeti ni trillion 35 na ushee halafu hatuna hata nusu yake.. Anajua soon tutaanza kutembeza bakuli
Mkuu Tz inapoelekea, itakuwa sawa na mwanamke ambaye alishagombana na mume, kagombana na EXs wake, kagombana na michepuko, kagombana na ndugu wa mume, kagombana na majirani zake, na kibaya zaidi hata wale ambao amekuwa akiabudu nao amegombana nao pia, matokeo yake kila anapoomba msaada wanamtazama kwa jicho la tahadhari sana, maana ni mwanamke mshari.
 
Kwa hiyo unalilia "misaada" sio?
Sililii misaada ila nimeongea ukweli mchungu! serikali ndiyo inayolilia misaada tena kwa kuomba kabisaa kwa mabeberu ambao ikiwa na ninyi wananchi inawaita mabeberu ila ikiwa kwa wahisani inapiga magoti na kuwaita wafadhili na tena huwaita mabwana!!
 
Mkuu Tz inapoelekea, itakuwa sawa na mwanamke ambaye alishagombana na mume, kagombana na EXs wake, kagombana na michepuko, kagombana na ndugu wa mume, kagombana na majirani zake, na kibaya zaidi hata wale ambao amekuwa akiabudu nao amegombana nao pia, matokeo yake kila anapoomba msaada wanamtazama kwa jicho la tahadhari sana, maana ni mwanamke mshari.
Mtu anayefikia hatua hii hujikuta anagombana na mwenyewe..
Anajikasirikia
Anajisonya
Anajitukana
Akizidiwa kabisa anajipiga halafu anajikimbia mwenyewe [emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
na sasa hapo anatesa watoto maana hata mume/ndugu/majirani/na wengine wakimsaidia wanapotoa pesa ili alee watoto yeye anatumia pesa hizo kuweka nywele kalikiti, kujichubua, kununua madela na kuijikwatua ili mradi naye aonekane yumo na ana pesa matokeo yake watoto wake wanashindwa kupata elimu nzuri, na huduma nyingine nzuri, but yeye hajali!!!!
 
Back
Top Bottom