SoC02 Tanzania inavyopiga hatua kiuchumi katika sekta mbalimbali

SoC02 Tanzania inavyopiga hatua kiuchumi katika sekta mbalimbali

Stories of Change - 2022 Competition

EGF

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2017
Posts
387
Reaction score
986
Uchumi ni jumla ya shughuli zote za binadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji yao. Shughuli hizo ni pamoja na uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa kwa huduma kwa njia mbalimbali.

Uchumi mara nyingi hutazamwa kwenye ngazi za kijiji, eneo, taifa au Dunia. Kwa kipindi cha miaka kadhaa Tanzania imeshuhudia ukuaji mkubwa wa uchumi ukilinganisha na miaka mingi nyuma.

Mafanikio makubwa kiuchumi yametokana na utekelezaji wa mipango ya maendeleo lakini pia uchumi ulikua kwa asilimia 4.9 mwaka 2021 huu ni ukuaji mkubwa zaidi ikilinganishwa na miaka iliyopita na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache barani Afrika ambayo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi. Kutokana na ukuaji huo, Benki ya Dunia iliitangaza Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati mwaka 2019.

Katika kuhakikisha Tanzania inazidi kupiga hatua katika kukuza uchumi wake serikali imejikita zaidi katika kuanzisha miradi ya kimkakati ambayo itainufaisha Taifa . baadhi ya miradi hio ikiwemo mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), Mradi wa kuzalisha umeme wa mto Rufiji unaotambulika kama Stiegler’s Gorge pamoja na uamuzi wa serikali wa kuhamia Dodoma.

1623057004-1.jpg

Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kisasa ambao unaunganisha Tanzania na nchi jirani za Rwanda, Uganda, Burundi,
Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Picha kwa hisani ya Government project website.

thumb_2515_800x420_0_0_auto.jpg


Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akikagua maendeleo mradi wa kuzalisha umeme Mto Rufiji
Picha kwa hisani ya MwanaHalisi.


Lakini pia haikuishia hapo serikali imekamilisha miradi mikubwa ikiwamo ununuzi wa ndege saba kwaajili ya kufufua shirika la ndege Tanzania (ATCL). Ujenzi wa Daraja la Mfugale lililopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam, tayari limekamilika kwa gharama ya zaidi ya Sh106 bilioni huku Serikali ya Japan kupitia shirika lake la maendeleo, (Jica) ikitoa msaada wa zaidi ya Sh26 bilioni.

2.jpg

Moja ya Ndege Mpya zilizonunuliwa na Serikali kwaajili ya kwa ajili ya kutumiwa na Shirika
la Ndege la Air Tanzania. Picha na BBC Swahili.

Katika kutatua tatizo la foleni ya magari katika makutano ya barabara ya Sam Nujoma, Morogoro na mandela eneo la ubungo ambalo sasa limepatiwa ufumbuzi baada ya serikali kukamilisha ujenzi wa barabara za juu eneo hilo.

Hii ni hatua kubwa katika kukuza uchumi ukilinganisha na miaka sitini nyumba. Serikali imechukua hatua madhubuti ya kuanzisha miradi mbalimbali ambayo inamanufaa makubwa kawa taifa la Tanzania.

fff7d0e68c23ebbb96d97a8a2b3f18a4.jpg

Makutano ya barabara ya ubungo kuelekea Buguruni ikiwa ni sehemu ya kupunguza tatizo
la foleni. picha kwa hisani ya Mwananchi.co.tz


Vilevile yapo mafanikio mengi katika wizara ya utalii ukilinganisha na miaka sitini (60) nyuma ambapo imechochea kwa namna moja au nyingine katika kukuza uchumi wa nchi.

Tanzania imejaliwa kuwa na maeneo ya hifadhi za wanyamapori, misitu, nyuki na malikale yenye mchango mkubwa katika uhifadhi wa mazingira, ustawi wa wananchi na ukuaji wa uchumi wan nchi yetu.

Katika kipindi cha miaka ya karibuni Tanzania imeshuhudia ongezeko la watalii hasa watu mashuhuri kutoka mataifa mbalimbali ya kigeni. Hii inaonesha ni kwa kiasi gani ukuaji wa sekta ya utalii umezidi kuongezeka kwa kasi. Sekta ya utalii imeendelea kujitangaza kupitia vyombo vya habari ndani na nje ya nchi - kwa mfano, TBC1, ITV, Clouds TV, BBC Swahili, na Doutche Welle Ujerumani; mitandao ya kijamii.

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan alitangaza utalii kupitia filamu ya Royal Tour ambayo utakubaliana nami filamu hiyo imekua chachu ya ukuaji wa sekta ya utalii nchini. utangazaji wa vivutio vya utalii umeendelea kuonesha matokeo chanya ambapo kwa mujibu wa Naibu waziri wa maliasili na utalii, Mhe. Mary Masanja (MB) amesema mwaka 2021 Tanzania ilipokea watalii 48,537 kutoka Marekani ikiwa ni ongezeko la asilimia 55 ikilinganishwa na watalii 31,211 kwa mwaka 2020.

Watalii-Tz-1-1.jpg

Baadhi ya Watalii wakiwa katika mbuga ya serengeti inayopatikana Tanzania.
picha na Bongo5.com

Lakini pia kwa upande wa sekta ya elimu na mafunzo , kwa mujibu wa dira ya maendeleo ya taifa 2011/2012 hadi 2024/2025 inatarajiwa kuleta maendeleo ya haraka ya rasilimali watu kwa kutayarisha idadi ya kutosha ya watanzania walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ili kulifanya taifa lipate maendeleo na kua lenye uchumi wa kati na shindani ifikapo mwaka 2025.

Hivyo kupitia mipango na mafanikio haya ya serikali za awamu mbalimbali tunaona kwamba kwa kipindi chote cha miaka sitini serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa sana ya kiuchumi katika Nyanja mbalimbali ikiwemo katika sekta ya utalii, fedha nishati elimu na hata kilimo pia.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom