Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
TANZANIA INAYO ORODHA YA MASHUJAA WAKE?
Ili Tanzania iweze kuwaenzi mashujaa wake inabidi kwanza kabla ya yote inahitajika iandike historia yake upya.
Kutokana na historia hii ndipo itaweza kuwajua mashujaa wake.
Kwa miaka mingi Tanzania imekuwa taifa lisilokuwa na mashujaa wake.
Sababu ya hali hii ni kukosekana kwa historia ya kuaminika ambayo ndani yake wapo waliojipambanua katika kuipigania nchi yao kwa njia mbalimbali.
Hadi leo historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya uhuru wa Zanzibar na mapinduuzi yake bado iko katika matatizo ingawa imetafitiwa na kuandikwa na waandishi wa kizalendo.
Watawala wengi Afrika wanaogopa historia za nchi zao.
Wanapenda wao ndiyo wawe historia ya taifa.
Msukumo wao katika kuwa na historia za nchi zao ni kuwa na historia rasmi.
Historia hii isiguswe.
Tatizo kubwa la historia hizi ni kutaka nani awemo na nani asiwemo.
Bilal Rehani Waikela ametambulika kuwa alipigania uhuru wa Tanganyika akiwa bega kwa bega na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa yuko kwenye kitanda cha umauti na mzee wa miaka 90.
Serikali ikagharamia matibabu yake na ikafika mazikoni na kusoma rambirambi.
Paul Bomani alipofariki magazeti yameandika kifo chake lakini wahariri hawamjui Paul Bomani alikuwa nani katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Paul Bomani alikuwa katika orodha ya Hamza Mwapachu (1913 - 1962) ya vijana wadogo wenye uwezo kuongoza mapambano dhidi ya ukoloni wa Waingereza ambao yeye aliwaperemba waingie katika siasa waikomboe Tanganyika.
Katika orodha hii alikuwamo Julius Nyerere, Paul Bomani na Abdul Sykes kwa kuwataja wachache.
Historia ya Hamza Mwapachu inasisimua kuisoma na kuisikia ikihadithiwa.
Dr. Vedasto Kyaruzi kaueleza ubongo wa Hamza Mwapachu na subra yake katika mswada wa kitabu alichoandika, "The Muhaya Doctor."
Ndani ya mswada huu kuna madaktari watano mashujaa wa uhuru: Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Luciano Tsere, Dr. Wilbard Mwanjisi na Dr. Michael Lugazia.
Wote hao wamepigania uhuru.
Turudi kwa Paul Bomani.
Paul Bomani alikuwa mtu wa kujiweza na mfuko wake ulikuwa wazi kwa TANU.
Mwalimu Nyerere alipata kusema kuwa kuna watu TANU imeundwa imewakuta na fedha zao hawakutajirika ndani ya chama.
Mwalimu akasema TANU imemkuta Paul Bomani na fedha zake.
Halikadhalika Paul Rupia, Dossa Aziz na Abdul na Ally Sykes hawa ndiyo walioasisi TANU fedha zao.
Leo ukifika ofisi ya CCM, Mwanza hakuna kumbukumbu yoyote ya Paul Bomani wala CCM Lumumba hakuna kumbukumbu yoyote ya mashujaa hawa.
Jambo la kusikitisha ni kuwa Hamza Mwapachu mwenyewe aliyekuwa akiwakamulia Waingereza ndimu historia ya uhuru bado haijamtambua.
Leo ukifika nyumbani kwa Ali Msham Magomeni Mapipa utawakuta wanae wanapiga pasi barazani kujitafutia riziki iliyo halali.
Nyumba hii ndipo lilipokuwa tawi kubwa la TANU na Ali Msham akamfungulia duka la mafuta ya taa Mama Maria ili amsaidie mumewe aliyekuwa kaacha kazi ya ualimu apiganie uhuru wa Tanganyika.
Mwalimu na Mama Maria wakiishi si mbali sana na nyumba ya Ali Msham, Magomeni Maduka Sita.
Ukiambiwa kuwa Mama Maria alikuwa akishinda nyumba hiyo kutwa nzima akiuza duka lake na kufuma sweta utakataa.
Nyumba imeinama mkao wa kuanguka.
Hawa ndiyo mashujaa wetu.
Hadi leo tuko huru zaidi ya nusu karne hatujawaadhimisha.
Jana ndiyo Rais Samia Suluhu Hassan anaahidi kuwaenzi mashujaa wetu.
Tulikuwa wapi miaka yote?
PICHA: Bilal Rehani Waikela, Hamza Mwapachu na Paul Bomani.