- Feb 10, 2006
- 4,324
- 13,967
Wadau nashukuru atleast nimepata ka mwanga kidogo. Kang nathamini sana mchango wako. Umenifungua kiaina. Mimi natumia simu ya mkononi ku connect kwenye net through USb cable ila inakula sana sijui ni huu mtandao wa voda uko expensive au ni vipi.
Baada ya kumsoma Kimori nimefikiria ni vema nikatoa mawazo yangu katika mada mpya ambapo sintovuruga mjadala aliouanzisha. Naamini wengine watakuja na mawazo yao tofauti ama yanayoshabihiana na yangu hivyo kutoa mwanga kwa watumiaji wa Internet Tanzania.
Ninapoongelea speed ya download (uploads wanaohitaji ni wachache sana) namaanisha bila kutumia Download Accelerators.
VodaComa as an ISP:
VodaCom kama hauna package maalum basi gharama yake ni kubwa sana, ni zaidi ya Tshs 300/= per MB. Ni vema kama umedhamiria kutumia VodaCom internet (speed yao sijaridhika nayo ingawa nilinunua bundle ya 5GB toka kwao kwa majaribio) basi jaribu kununua bundle ili kupunguza gharama. Devices (modem) za connection kwa VodaCom ni bei nafuu (170,000/=) hivyo unaweza kununua na kutumia kirahisi. Ukiweka bundle ya walau laki 2 unaweza kuitumia mpaka itakapoisha ndani ya kipindi cha miezi mitatu, uzuri wake ni kuwa una-recharge kwa vouchers za kawaida kabisa. Inafaa kwa normal users wasio na downloads wala uploads kubwa. Statistics za downloads na uploads utaziona kwenye software ya modem yako. Download speed yao haizidi 100kb/s pamoja na kuwa unaweza kuwa na modem yenye uwezo wa 7.2MB/s
Kuna Zantel:
Hawa nimekuwa nao kwa muda sasa na mimi ni Postpaid Customer wao, hawa nao nalipia bundle ya 10GB kwa mwezi. Nimekuwa nikitumia service yao kwa zaidi ya miezi 6 sasa na naweza kusema pamoja na kuwa nilishakumbana na matatizo nao lakini mara zote wametoa ushirikiano wa karibu. Hawa download speed yao ni nzuri na kuna wakati inafikia 250kb/s. Kwa bundle hii ya 10GB, nanunua 1MB kwa Tshs 26/= na inakuwa ina VAT ndani yake. Haya matangazo wanayoweka barabarani na kudai wana UNLIMITED Internet service ni lugha ya kibiashara ambayo inamaanisha 3GB kwa 90,000/= wakiwa wamewa-target normal users. Kwa mtu kama mimi ambaye per month najikuta nina zaidi ya 20GB siwezi kukubaliwa kuwa na hiyo ya Tshs 90,000/= per month. Hawa ukikumbana na tatizo na service zao naweza hata kukusaidia endapo utakosa msaada wa haraka kwani modem zao nimezitumia karibia zote na kuna device ambayo ukiichukua kwao hata kama una PC 20 ofisini kwako bado unaweza kutumia modem moja kwa PC zote.
Kuna Benson Online (BoL):
Hawa achana nao kabisa, nimetumia service yao kwa miezi 6 hivi, kwa mobile zao ambazo walizitangaza kuwa unalipia 180,000/= kwa miezi 3 na unapewa UNLIMITED (uwongo tu kwani wanakubana kwa speed), lakini mobiles zile zikipata joto tu kwishnei! Aidha, connection ya nyumbani kabisa niliyokuwa nayo speed yake ilikuwa inabidi niache nimefungua page nikazunguke wee ili kukuta page imemaliza ku-load. Internet speed yao haizidi 60kb/s (download speed). Hawafai kwa mtu mwenye kuzoea internet ya kasi. Labda wabadilike!
Kuna hawa Raha.com:
Nimekuwa mteja wao zaidi ya miaka 2 sasa, kuna kipindi internet yao ilikuwa speed kubwa sana (3months ago) lakini sasa sijui wameelemewa au ni vipi, imekuwa slow SANA kiasi inakatisha tamaa hata kutumia. I do not recommend them to any of my friends. Bahati mbaya zaidi hawana internet ambayo itakuwezesha mtu kuwa mobile. Labda wabadilike!
Kuna hawa wageni SasaTel:
Hata kabla ya kutumia service yao niligundua matangazo yao ni tofauti na walicho nacho, bei zao ziko juu ingawa nilitarajia walivyo wageni wameisoma market ya Tanzania hivyo ni rahisi kwao kuja na package za kueleweka. Hawakujipanga vema, lazima ununue devices za kwao kupata services zao, wamekosea labda warekebishe mapema kabisa.
Kuna SimbaNet:
Hawa connection yao ya nyumbani (isiyo mobile) ni nzuri, bado niko kwenye majaribio yake. Pia SimbaNet wapo njiani kuja na modem ambazo ni sawa na za Zantel/VodaCom, nina bahati kuwa nimeichukua moja naifanyia majaribio ili baadae niweze kujua kama watafaa kwenye market yetu. Mpaka sasa speed yao ni nzuri, atleast 120kb/s kwa downloads inaweza kufikiwa. Nina wiki 3 tangu niichukue hii connection yao na bado sijaona tatizo kubwa katika kuunganisha, matatizo mawili ambayo nadhani kwa customers wa Tanzania wanaweza kuyaita matatizo ni kulazimika kutumia password, na kutumia username iliyo complicated kitu ambacho ni rahisi kurekebishwa ndani ya dakika chache (labda walifanya makusudi kwa wateja wa kwanza).
TTCL Broadband:
Hawa TTCL ni mwisho wa matatizo! Nina wateja karibia 6 hivi (makampuni) ambapo mimi ndiye naangalia internet services za makampuni haya, wengi nilikuta walishakata tamaa tokana na huduma mbovu za ISP wengine na kuwa na suppliers wasiotoa ufumbuzi wa matatizo yao. Tangu nimeingia makubaliano nao niliamua kutumia TTCL na Zantel kama ISP kwa wateja wangu na wote wawili hawa wameonekana kutatua matatizo ya wateja hawa. TTCL Broadband ina packages mbalimbali lakini ukichukua kama 10GB unalipia Tshs 360,000/=. Hii kwa kampuni ya kawaida inatosha kabisa lakini unahitaji kuwa na mtu au kampuni maalum ya kukufanyia hivyo, ukiwaacha TTCL wenyewe wakufanyie kazi basi ukiritimba wake unaweza kuuchukia kabisa kwani service itakuwa haifurahishi na unaweza kujuta hata kuwa nao. Kinachosaidia kwa wateja wangu ni kuwa nimechukua liabilities zote na kuwa na-deal moja kwa moja na TTCL.
TTCL wana bundles za aina nyingi, 500MB - 50GB per month. Download speed ni kubwa na inafikia hata 256kp/s bila kutumia download accelerators, ukitumia accelerators inakwenda mpaka 2MB/sec. Kinachofurahisha zaidi TTCL wana Upload speed kubwa tu, inafikia hata 516kp/sec.
Matatizo ya TTCL Broadband ni mengi kidogo:
- Hakuna Post Paid service, ikifika mwisho wa mwezi wanakukatia tu! Yani hawakupi hata dakika ili uka-recharge. Kama una mteja ambaye ana service muhimu unaweza kubeba lawama zisizo zako.
- Huduma kwa wateja ni very poor, unaweza kupoteza siku nzima na hela yako mkononi bila kupata service ya kueleweka
- Baadhi ya maeneo haifanyi kazi (ndani ya Dar) hivyo unaambiwa subiri walau miezi miwili lakini ukweli ni kuwa hata ikiisha hiyo miezi miwili ukirudi unaambiwa miwili tena!
- Wakati mwingine unalipia gharama zaidi ya ulivyotumia, statistics zote unaziangalia online hivyo ukishakatikiwa service huwezi kujua mpaka uende kwenye kituo cha TTCL kujua nini kilitokea na kivipi... Wanakatisha tamaa sana!
Nilikuwa natumia service hii lakini niliiweka chini na modem yake kuigawa BURE kwa mtu aliyeonekana kuipenda. Iko slow na haiwezi kuhimili mikikimikiki.
Zain as an ISP:
Zain inafaa katika Blackberry (Tshs 35,000/=) tu. Ninayo Blackberry 9000 Bold na service ni nzuri kwa kiasi chake! Lakini, services nyingine hawana tofauti na VodaCom. Ukitumia Blackberry kwa VodaCom hutotamani kurudia isipokuwa Zain. Kwa Blackberry hapo Zain wamefanikisha!
ISP wengine kama CATS-Net, iWay Africa n.k nitatoa feedback baadae kwani ndio bado natafuta connections zao ili niweze kutoa comment.
NB: Haya ni mawazo yangu kwani wengine yawezekana wanapata service tofauti na ninavyoipata. Nimekwishajaribu ISP hao juu na naweza kuwa na mawazo tofauti nikiwarudia mmoja baada ya mwingine kuangalia kama kuna mabadiliko yoyote.