Nitainunua this week, tuonane basi mkuu mbona kimya sana wewe?
Halafu kama ni $42 kwa 2GB basi hao ndio watakuwa Cheapest ISP in Tanzania kwa sasa mkuu....
TCRA wafanye kazi yao na kuacha kuzembea hali wananchi wanaongopewa kwenye mabango. Kama matangazo yao yanaongopa, waondoe hayo mabango barabarani. Na ikiwezekana wapatiwe faini pia.Kuna Zantel:
Hawa nimekuwa nao kwa muda sasa na mimi ni Postpaid Customer wao, hawa nao nalipia bundle ya 10GB kwa mwezi. Nimekuwa nikitumia service yao kwa zaidi ya miezi 6 sasa na naweza kusema pamoja na kuwa nilishakumbana na matatizo nao lakini mara zote wametoa ushirikiano wa karibu. Hawa download speed yao ni nzuri na kuna wakati inafikia 250kb/s. Kwa bundle hii ya 10GB, nanunua 1MB kwa Tshs 26/= na inakuwa ina VAT ndani yake. Haya matangazo wanayoweka barabarani na kudai wana UNLIMITED Internet service ni lugha ya kibiashara ambayo inamaanisha 2BG kwa 90,000/= wakiwa wamewa-target normal users. Kwa mtu kama mimi ambaye per month najikuta nina zaidi ya 20GB siwezi kukubaliwa kuwa na hiyo ya Tshs 90,000/= per month. Hawa ukikumbana na tatizo na service zao naweza hata kukusaidia endapo utakosa msaada wa haraka kwani modem zao nimezitumia karibia zote na kuna device ambayo ukiichukua kwao hata kama una PC 20 ofisini kwako bado unaweza kutumia modem moja kwa PC zote.
Aisee tunangojea feedback ya CTV tujitume....what the feedback max?
Mara ya mwicho nilipotumia CTV ilikuwa wanapitisha waya kutoka kwao hadi kwenye computer yako, so inabidi uwe maeneo ya mjini. Speed slow, lakini ndo hivyo cheap. Hii ilikuwa miaka 2-3 iliyopita.
Mbu,
Labda wakwambie wengine. Mi kwa sasa sijui
Ukifuatilia kwa rates hizi za Vodacom utagundua kuwa kadri unavyochukua bundles kubwa zaidi ndipo na matumizi yake yanakuwa cheap kwa mfano anayechukua 50GB kwa sh. 1000,000/= ni sawa na sh. 20 tu kwa kila MB. Na hizi ni kwa miezi mitatu (3)Internet Bundle za Vodacom
10MB=2,000/- 200.00Tsh/MB
20MB=3,700/- 185.00Tsh/MB
100MB=15,000/- 150.00Tsh/MB
250MB=25,000/- 100.00Tsh/MB
500MB=40,000/- 80.00Tsh/MB
1GB = 70,000/- 70.00Tsh/MB
2GB =95,000/- 47.50Tsh/MB
4GB = 190,000/- 47.50Tsh/MB
5GB =200,000/- 40.00Tsh/MB
10GB =360,000/- 36.00Tsh/MB
20GB =450,000/- 22.50Tsh/MB
50GB =1000,000/- 20.00Tsh/MB
Nothing UNLIMITED! Ni lugha za kibiashara mkuu.
Halafu kama una kampuni unajua unataka kuwa hustle free unaweza kununua 20GB ya TTCL kwa Tshs 450,000/= kwa mwezi na speed nakuhakikishia ni ya kueleweka. Tatizo ni kama nilivyosema awali, usi-deal na TTCL moja kwa moja, kama unaweza kupata mtaalam ambaye ni mwaminifu akakusaidia ku-deal nao basi inakurahisishia mambo na kukusahaulisha kero za internet.
Ukifuatilia kwa rates hizi za Vodacom utagundua kuwa kadri unavyochukua bundles kubwa zaidi ndipo na matumizi yake yanakuwa cheap kwa mfano anayechukua 50GB kwa sh. 1000,000/= ni sawa na sh. 20 tu kwa kila MB. Na hizi ni kwa miezi mitatu (3)
Mimi binafsi juzijuzi hapa nimeweka IGB kwa sh.70,000 kwa hiyo nakamuliwa 70sh/MB.
Halafu hawa Vodacom kuna modem yao inakuwa na speed kali sana na wakati mwingine inakuwa low speed. Lakini hata hivyo kama na-download file kubwa kuna wakati speed yake inafika 150Kbs/sec na wakati mwingine inakuwa ndogo sana hadi 5Kbs/sec. Lakini bado nawakubali japokuwa gharama zao bado zinaonekana kuwa kubwa.
Kama bado upo Dar na nakumbuka tuliwahi kukutana then tunaweza kuwasiliana via email nami nikakuunganisha na mtu wa ndani Zantel akakupa device flani hivi ukaunganisha kwenye Router yako ili kuweza kuunganisha pc zaidi ya 1 (hata 12 inafanya kazi).Nimekuwa nikitumia TTCL broadband kwenye internet cafe yenye PC 12, huwa nanunua 20 GB kwa 450,000 na inanisuit vizuri. Sasa nataka kufungua branch nyingine sehemu ambayo TTCL hawana cable network yaani nyaya zao za landline hazijafika. Mkuu Melo unanishauri nitumie kampuni gani? Zantel itaweza kunisaidia? i'll appreciate ur help!!
if you go to Speedtest.net - World Results.