Tanzania is leading in East Africa.

mulisaaa

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2017
Posts
6,969
Reaction score
7,027
Tanzania yatajwa kuongoza Afrika Mashariki

JUMAPILI , 2ND SEP , 2018
NA ISMAEL MOHAMED
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tanzania inaongoza kwa kupokea uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki.

Bendera ya Tanzania​
Majaliwa ameyasema hayo leo Jumapili, Septemba 02 ,2018 wakati akihutubia kongamano la biashara kati ya Tanzania na China kwenye Hoteli ya Winstin jijini Beijing nchini China.
Aidha, Waziri Mkuu amesema Tanzania imethibitika kuwa ni Taifa lililodhamiria kwa dhati kujenga uchumi wa viwanda, pamoja na kulinda na kudumisha amani na utulivu.
"Mtiririko wa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja nchini umeongezeka kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita na sasa wawekezaji wameipa kipaumbele Tanzania kama kitovu cha uwekezaji barani Afrika", amesema Majaliwa.
Waziri Majaliwa amesema ripoti ya uwekezaji duniani iliyotolewa mwaka 2018, inaonesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kupokea uwekezaji katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na imepokea kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.2 mwaka 2017.
"Tanzania inafanya juhudi kubwa ili iweze kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, hivyo imeweka mkazo mkubwa katika kujenga msingi imara wa viwanda. Ili kufanikisha hilo tumeandaa Ukanda wa kuzalisha kwa ajili ya mauzo ya nje na ukanda maalum wa kiuchumi tukilenga kutimiza mkakakati wetu wa kukuza uchumi wa viwanda na biashara", amesisitiza Majaliwa.
Akizungumzia kuhusu sekta ya fedha, Waziri Mkuu amesema Tanzania inawakaribisha wawekezaji kuanzisha taasisi za kifedha kama vile benki kwa ajili ya kutoa mikopo midogo midogo, benki za uwekezaji, benki za kilimo na benki za biashara.
Katika miaka ya hivi karibuni nchi ya Tanzania imekuwa ikipokea wawekezaji wengi kutoka nchi za nje, kutokana na utendaji kazi mzuri wa Rais Dkt. Magufuli pamoja na hamasa zake anazozitoa kwa mabalozi mbalimbali wanaokwenda kuwakilisha taifa nje ya nchi kupigania uwekezaji wa ndani uongezeke nasio kwenda kukaa maofisini tu.

http://lit360.africa/wisdom-from-kr...tm_medium=referral&utm_medium=referral=wisdom
 
Taarifa inakinzana na uhalisia wa ukusanyaji kodi nchini. Msituchanganye
 
Kuna watu wameanza kupanick baada ya kuona Jiwe amekuwa anti-social kupindukia na amekomalia huko huko ikulu. Nyuma ya pazia lazima kuna kiza. [emoji1].....sijui kama bado wanapimana mkojo? Naona kama inanihusu. [emoji38]
 
Habari imekuwa mbaya sana jirani. Naona kiroho mapigo yamepanda.😂😂😂
 
Investment na ukusanyaji wa kodi ni vitu viwili tofauti. Halafu mapato hayatokani na kodi pekee. Nenda shule usijiaibishe humu.
Ni kwel kaka, Kodi sio njia pekee, ila Kodi ndio njia kubwa ya mapato. Naamini wawekezaji wanalipa Kodi, kwa hiyo hapa uwekezaji lazima uendane na mapato yatokanayo na Kodi, hebu tudadavulie hapa, maana ww utakua umeenda vidato sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Investment na ukusanyaji wa kodi ni vitu viwili tofauti. Halafu mapato hayatokani na kodi pekee. Nenda shule usijiaibishe humu.

Hawa ndiyo wale wanaodandia gari kwa MBELE. Hana analojua lkn anataka tu naye achangie. Hawa ni wa kuwapuuza tu.

CC: kawoli
 
Kuna kitu kinaitwa PPP. Public sector na private sectors zinafanya investments za pamoja. Revenue zinatoa huko.
 
Investment na ukusanyaji wa kodi ni vitu viwili tofauti. Halafu mapato hayatokani na kodi pekee. Nenda shule usijiaibishe humu.
huhitaji shule kubwa kujua kodi ndio chanzo kikuu cha mapato Kwa nchi. Vyanzo vingine ni vya ziada. Pia uwekezaji Mkubwa unapaswa uendane sambamba na ukusanyaji mapato. Uhalisia wa Tz kwasasa unaujua kwamba makusanyo yameshuka ustake kujitia ujinga. You can't just speak with mere words that we lead in investment whilst makusanyo hayasadifu!!!!
 
Huwa siongei na mbumbumbu kijana.
Hapa tunaongea investment na siyo kodi na ushuru. Bahati mbaya uwezo wako wa kuwaza ni mdooooooooogo.
 
Hawa ndiyo wale wanaodandia gari kwa MBELE. Hana analojua lkn anataka tu naye achangie. Hawa ni wa kuwapuuza tu.

CC: kawoli
eliakeem ni nini usichokijua?? Inahitaji shule ipi kubwa kujua kodi ndio chanzo kikuu cha mapato ya nchi? Thamani ya mwekezaji kwa serikali yoyote makini duniani ni ulipaji wake wa kodi. Kama makusanyo ya serikali yameshuka ina mana either serikali haikusany kodi ipasavyo ama uwekezaji umepungua. That's why we need to see high investment also increases our gvt revenue.
 
Hicho alicho kisema majaliwa kina kuwa backed na real data! Hapo amesema hayo mbele ya Dunia, Taasisi za kimataifa zime kua zikionyesha FDI za Tz zimekua juu ya nchi zote za E.A kwa miaka zaidi ya 5 sasa. Wewe umejuaje kwamba mapato yameshuka, njoo na data au report ya utafiti wako ambao uta disapprove taharifa za TRA kwamba mapato yapo kwenye all time high now.
Kuna mtu ametoka kuniambia by 2025 Tz itakua kama S.A ki uchumi ila sija muamini kwa sababu hana Data za ku back up claim yake kama wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Investment na ukusanyaji wa kodi ni vitu viwili tofauti. Halafu mapato hayatokani na kodi pekee. Nenda shule usijiaibishe humu.

Hahaha...mzee umemtandika moja ya uso..safi
 
You are right. But we need time for recovery as the country was in high TIME to get rid off bandit enterprises or businesses in the economy. The emerging investments are pure. Let wait and see.
 
Mtashinda mkirudia hii kitu kama wimbo wa chekechea? Ni kama hamujiamini. Mkiongoza kwa jambo lolote tu, mnapiga makelele kama paka yenye inataka kuzaa.
 
Kuna watu wameanza kupanick baada ya kuona Jiwe amekuwa anti-social kupindukia na amekomalia huko huko ikulu. Nyuma ya pazia lazima kuna kiza. [emoji1].....sijui kama bado wanapimana mkojo? Naona kama inanihusu. [emoji38]
Pepo la Vasco Da Gama limehamia kwenu!
Mmekwisha kabisa walahi!
That’s all
 
Hongera MAMA TANZANIA WALAHI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…