SoC04 Tanzania itasimama, Tanzania tuitakayo

SoC04 Tanzania itasimama, Tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

BROADCASTER GIDEON

New Member
Joined
Jun 8, 2024
Posts
2
Reaction score
2
Tanzania ikiwa ni moja ya nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, ni nchi ambayo imebarikiwa maliasili mbalimbali ikiwa ni pamoja na madini, mbuga za wanyama, Mistu, ardhi yenye rutuba ya kutosha, watu, maji ya kutosha na mimea ya asili pamoja na wanyama asilia wanaolipa sifa kubwa taifa letu. Kama vile twiga na tembo. Mbali ya utajiri huu mkubwa ambao Tanzania inao lakini bado watu wake ni masikini hali kadhalika bado nchi hii ni maskini kwa upande wa miundombinu na uchumi ukilinganisha na baadhi ya mataifa ya Ulaya, Amerika na Asia. Juhudi za Tanzania kuwa Taifa imara na linalojitegemea kiuchumi na kiutawala zilianza punde tu baada ya kupata uhuru wake mwaka 1961 na ziliendelea kukua baada ya Tanganyika kuungana na Zanzibar na kuunda Tanzania moja mwaka 1964.

Leo hii nimeona ni vyema nitoe mawazo yangu ni jinsi gani Tanzania tunaweza kuwa imara kwa miaka ijayo tofauti na sasa, katika nchi yoyote ile kuna sekta mbalimbali ambazo zinapaswa kuzingatiwa lakini kwangu mimi naona kuna sekta tano kwanza ambazo kama zitazingatiwa basi Tanzania itasimama na kuwa taifa kubwa sana Afrika na Duniani kote, ambapo sekta hizo ni kilimo na viwanda, Elimu na teknolojia, Afya, Siasa zenye manufaa na Manzingira.

Sekta za kilimo na viwanda ndio sekta muhimu zaidi, katika nchi yoyote. Ili iweze kuendelea kwa kasi inabidi iwe na chakula cha kutosha ili iweze kujitegemea, sambamba na viwanda vya kutosha ili iweze kutegemea bidhaa zake badala ya bidhaa za nje. Kuhusu kilimo leo nakuja na mawazo tofauti kabisa na yale yaliyozoeleka. Maana yangu ni kwamba mbali na wananchi kulima kwa juhudi na serikali kutoa vifaa vya kilimo kama vile mbolea na trekta za kilimo, pia serikali inapaswa kutenga na kuanzisha mashamba makubwa sana yatakayo limwa na serikali, ambapo mazao mbalimbali yatalimwa na hivyo serikali ya Tanzania itakuwa na chakula cha kutosha hivyo Tanzania na njaa itakuwa imekwisha na kutakuwa na mzunguko mkubwa wa fedha za ndani na fedha haitakuwa tatizo tena katika nchi yetu.Mbali na kutegemea wananchi walime kwa ajili ya chakula cha Tanzania nzima ndio maana mpaka leo tunashuhudia misaada kutoka Marekani kuja Tanzania, jambo ambalo sio zuri kabisa kwa taifa letu lenye rutuba na ardhi ya kutosha.

shamba-la-mpunga.jpg

Jumanne, Oktoba 29, 2013 — updated on Februari 13, 2021(MWANANCHI)

Sambamba na kilimo pia serikali inapaswa kurudi kwenye mfumo wa kushughulikia viwanda, nchi yoyote yenye uchumi imara, viwanda ndio kitega uchumi kikubwa.Nchi zote duniani zenye uchumi imara zina viwanda vya kutosha, hii ni kwa Sababu viwanda hufanya taifa husika kutegemea bidhaa zake ya ndani na hii hufanya fedha ya nchi kuwa na thamani maana mzunguko utakuwa ni mkubwa sana, hivyo Tanzania fedha zetu zitakuwa na thamani kubwa sana ukilinganisha na sasa kama utategemea bidhaa zetu na viwanda vyetu. Tanzania kwanza tunapaswa kuwekeza katika viwanda vikubwa kama vile viwanda vya chuma, ambavyo vitatusaidi kutengeneza magari na vifaa vingine vya chuma. Hivyo viwanda vinapaswa kuzingatiwa sana. Sio kuwekeza kwenye viwanda vya chakula na vinywaji tu ambavyo havina matokeo makubwa katika maendeleo yetu.
HC1700-new-type-Pendulum-Raymond-Mill.jpg

pic-viwanda.jpg

Viwanda vikubwa vya China kutoka (BBC-swahili)


Sekta ya elimu ni sekta muhimu kabisa katika maendeleo ya nchi yetu, maana vitu vingi na sekta nyingi sana Tanzania chanzo chake ni elimu. Wataalamu wengi sana kama madaktari, waalimu na wahandisi hutokana na elimu kumbe mfumo wa elimu unapaswa kuboreshwa sana, mfano sasa Elimu ya teknolojia, ufundi na vitendo, sasa inapaswa kuanzishwa na kuboreshwa zaidi, ambapo serikali inapaswa kuwekeza pia kwenye masomo ya sayansi tangu elimu ya msingi. Katika suala elimu, nguvu kubwa inapaswa kuwekwa kwenye mafunzo ya elimu ya kati na ufundi ili kuimarisha uzoefu na ujuzi kwa vijana hii itafanya vijana wawe wajuzi na waweze kujitegemea wenyewe mbali na kutegemea ajira za serikali. Kumbe kama Serikali itafanya hivyo kufikia mwaka 2050 kero ya Ajira itabakia historia. Katika sekta ya elimu ni vyema Kiswahili kitumike katika viwango vyote vya elimu. Lengo ni kujenga weledi na kujitegemea wenyewe.
SHULE YA SEKONDARI IHUNGO_0001_IMGM9130.jpg
SHULE YA SEKONDARI IHUNGO_0003_IMGM9092.jpg

Shule Bora ya sekondari ya ihungo picha kutoka (michuzi brog 2020)

Vile vile uwekezaji katika teknolojia ya habari na miundombinu nayo ni siri kubwa sana katika maendeleo ya taifa letu, Shughuli nyingi zinakwama kwa sababu ya miundombinu mibovu katika taifa letu. Mfano jiji la Dar es Salaam kumekuwa na foleni kubwa sana hali inayofanya shughuli nyingi za uchumi kusimama, zaidi ya reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro bado huduma hii inapaswa kufika Tanzania nzima ambapo sasa huduma ya usafiri itakuwa ya haraka na ya uhakika kabisa, kwa namna hiyo Tanzania itasimama na kuwa bora kwa miaka ya hapo baadae.Teknolojia na elimu ni vitu vinavyo endana kabisa kumbe iwapo elimu itaboreshwa hata teknolojia itakuwa. Lakini pia serikali inapaswa kutuma wataalamu mbalimbali hasa wanasayansi katika mataifa yaliyoendelea kama vile China, Marekani na Israel ili kujifunza teknolojia zaidi.
2344_4-696x406.original.jpg

Barabara ya juu ya mfugale(picha kutoka mwananchi 2021)


Sekta ya afya nayo ni sekta muhimu kabisa katika maendeleo ya nchi yetu. Hii ni kwa sababu magonjwa yapo siku hadi siku, sio magonjwa tu hata mama wajawazito nao wanahitaji huduma za afya. Huduma za afya ni mhimili wa maendeleo katika nchi. Mfano, kama hakuna huduma bora za afya watu watakufa na nguvu kazi ya taifa itapungua. Kumbe sasa huduma afya kama vile hospitali,vituo vya afya na vituo vya kliniki vinapaswa kujengwa na kuboreshwa.
image.jpeg

Hospitali ya taifa mhimili (picha kutoka google mwananchi)

Mazingira yanapaswa kutunzwa kwa nguvu kubwa sana, wakati dunia inataabika na kuhangaika kuzuia mabadiliko ya tabia nchi hata sisi Tanzania tunapaswa kuhakisha kwamba tupo salama. Serikali kwa kushirikiana na wananchi wanapaswa kutunza vyanzo vya maji, mbuga za wanyama, hifadhi za wanyama na taifa, uoto wa asili, na hii itakoma kwa kuacha kukata miti ovyo na kupanda miti mingine mingi, pia ni vyema adhabu kali itolewe kwa wote wenye kuharibu mazingira ovyo na kuua wanyama pori.
g-1-660x400.jpg

Madhara ya mabadiliko ya tabia nchi Burundi (BBC-swahili 2023)

Mwisho,Siasa zenye tija Tanzania zinapaswa kuboreshwa. Tanzania tunataka siasa itakayo hubiri na kusisitiza amani.,upendo,mshikamano, ushirikiano na umoja siasa za chuki hazitakuwa na msaada kwetu. Ni vyema baada ya uchaguzi kila mtu ajikite katika kuleta maendeleo na sio kupandikiza chuki na vita miongoni mwa wananchi. Zawadi pekee Mungu aliyotupa ni amani. Mataifa mengi yameshindwa kuilinda amani lakini Tanzania tumeweza naomba tuilinde, na ninaamini amani italindwa kama viongozi tutakuwa na siasa za amani. Wakati huo tukiimarisha jeshi letu juu ya uvamizi wowote unaoweza kujitokeza kutoka mataifa mengine
headlineimage.adapt_.1460.high_.south_sudan_idp_032714.1455302226956-860x484.jpeg

Madhara ya vita wakimbizi Sudan picha toka(BBC-swahili2024)

Ikumbukwe kwamba yote haya yatatimia kama wananchi hasa viongozi wenye dhamana ya kuliongoza taifa watakuwa wawajibikaji, wakweli, wawazi na waaminifu. Maoni haya kama yatafanyiwa kazi ni matumaini yangu kuwa sasa Tanzania itasimama na kuwa taifa imara Afrika, lenye uchumi imara, jeshi imara, viwanda imara, baada ya hayo sasa Tanzania tunaweza kuboresha mambo kama vile, utamaduni wetu, katiba na ajira kwa vijana. Tanzania ni moja, sisi ni wamoja, amani iwe nasi watanzania. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika.
 

Attachments

  • pic-viwanda.jpg
    pic-viwanda.jpg
    136.1 KB · Views: 6
Upvote 2
Back
Top Bottom