SoC04 Tanzania itumie takwimu za mifugo kudhibiti mafuriko

SoC04 Tanzania itumie takwimu za mifugo kudhibiti mafuriko

Tanzania Tuitakayo competition threads

Samwel Ndoni

New Member
Joined
Aug 28, 2022
Posts
1
Reaction score
2
Nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania zimeingia kwenye historia ya kukumbana na athari mbaya za mafuriko ambazo hazijawahi kushuhudiwa kwa miongo mingi iliyopita.

2023 hadi 2024 baadhi za nchi za Afrika hususani kusini mwa jangwa la sahara zimepoteza mamia ya watu, makazi, mifugo na miundombinu kutokana na athari za mafuriko.

Tanzania peke yake katika kipindi cha mwezi mmoja (Aprili hadi Mei 3, 2024) ilipoteza watu 161 kutokana na mafuriko, huku wengine 250 wakijeruhiwa kutokana na maafa hayo yaliyoathiri takribani nchi nzima.

Pia katika kipindi hicho cha mwezi mmoja, kaya 52,000 zikiwa na watu Zaidi ya 210,000 ziliathirika (chanzo. Msemaji wa serikali, Mei 3,2024 jijini Dodoma).

Ikumbukwe maafa hayo yameripotiwa ndani ya mwezi mmoja, ukiachana na yale maporomoko ya tope wilaya ya Hanang na maafa ya mafuriko kwinginepo nchini.

Ili nchi iwe stahimilivu ni lazima iwe na rasilimali watu wenye afya na uwezo wa kufanya kazi, kunufaika na rasilimali zao kwa ajili ya ustawi wao na taifa kwa ujumla.

Kitendo cha kupoteza idadi kubwa ya watu, miundombinu, makazi na mifugo kutokana na athari za mafuriko kinaiacha nchi njia panda katika kuhakikisha inatoa huduma za kijamii na dharula kwa waathrika wa mafuriko kutokana na uwezo wa nchi zetu za Kiafrika.

Hakuna ubishi yote hayo licha ya kuwa ni majanga ya asili na yapo juu ya upeo wetu lakini kuna namna ikifanyika basi tunaweza kudhibiti au kupunguza athari za maafa.

Sote tuna uelewa wa pamoja kwamba kwa sasa Dunia inakabiliana na changamoto ya mazingira hasa mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo kimsingi kila sekta ina mchango wake kwenye utatuzi.

Ukataji wa miti kwa ajili ya shughuli mbalimbali hasa kutumia kama nishati ya kupikia majumbani na kwenye taasisi umepelekea athari za mabadiliko ya tabianchi na kusababisha mmomonyoko wa udongo ambao umekuwa chanzo cha mafuriko.

Tunawezaje kutumia takwimu za mifugo kuthibiti mafuriko?

Tanzania tunayoitaka kuanzia sasa hadi miaka 25 ijayo ni lazima tutumie takwimu za mifugo kuthibiti athari za mafuriko ambayo yamekuwa tishio kwa usalama wa watu na mali zao.

Tunaweza kutumia takwimu za sensa ya kilimo 2019/2020 kupata idadi ya mifugo iliyopo nchini kuiwezesha serikali pamoja na wadau kuja na mkakati wa kutumia mifugo hiyo kudhibiti mafuriko.

Kwa sababu serikali inatumia fedha nyingi kugharamia zoezi la sensa ni muhimu kwamba taarifa za hizo zikatumike kwenye mipango ya jamii kama ilivyokuwa lengo la lake.

Takwimu za sensa ya kilimo kitaifa 2019/2020 inaonesha kuwa Tanzania ina jumla ya Ng’ombe milioni 33.9, mbuzi milioni 24.5,kondoo milioni 8.5 na kuku milioni 87.7, takwimu hizo zinaifanya Tanzania kuwa nchi ya pili barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo ikitanguliwa na nchi ya Ethiopia.

Tunaweza kutumia fursa ya kuwa na mifugo mingi kwa kuanza kuzalisha umeme wa ‘Biogas’ kwa ajili ya matumizi ya kupikia majumbani, migahawani au kwenye taasisi kama vile shule, magereza na maeneo yanayohusisha mikusanyiko ya watu.

Biogas ni teknolojia inayotumia kinyesi cha wanyama kuzalisha nishati ambayo inaweza kutumika kwa ajili ya kupikia na mwanga majumbani au kwenye taasisi pia inatajwa kuwa ni rafiki wa mazingira.

Tukiwa na teknolojia hiyo bunifu kwa ajili ya kutoa nishati basi tabia ya kukata miti kwa ajili ya kuni na mkaa itakoma na tutaokoa mazingira yetu hivyo kuliepusha taifa la Tanzania na athari za mafuriko ambayo inachangiwa na ukataji miti holela.

Katika utekezaji wa mkakati huo serikali inapaswa kutumia takwimu zilizopo kufanya utafiti wa kina na kuona maeneo ambayo yana idadi kubwa ya mifugo ili kufunga mitambo ya ‘Biogas’ ya mfano kwa ajili ya kuzalisha nishati ya kupikia kwenye taasisi kama zilivyozitaja hapo juu.

Ni muhimu kuitumia tume ya taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika mpango huo hasa wakilenga yale maeno ambayo yameathiriwa sana na ukataji wa miti hovyo mfano halmashauri ya wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Aidha, pia serikali kwa kushirikiana na wadau wengie watoe elimu na hamasa kwa wananchi na taasisi kuona umuhimu wa kuwa na mtambo wa ‘Biogas’ ikiwemo kuwaunganisha na wataalam kwa ajili ya kufanya tathmini na elimu ya matumizi.

Kwa kuzingatia hilo serikali itumie hamasa ya mikopo ya asilimia kumi kwa ajili ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kuwashawishi kufuga mifugo na kuanzisha shughuli nyingine kama vile migahswa ambapo wataweza kutumia kinyesi cha mifugo yao kama nishati ya kupikia hivyo kuokoa gharama za kutafua nishati nyingine.

Kwa kufanya hivyo tutaikoa nchi yetu kwenye athari za mafuriko kwa kuwa watu hawatakata miti tena, pia tutaongeza thamani kwenye ufugaji wetu kwa kuwa zao la kinyesi halitatupwa tu au kusubiri iwe samadi msimu wa kilimo bali litatumika kama nishati ya kupikia.
 
Upvote 6
Biogasi,

Hivi hii kitu haina version yake potabo kama sola hivi?

Halafu nnaomba kuuliza, hivi kimradi kidoogo cha biogas kinagharimu kiasi gani? Cha nyumbani tu kiwashia taa na kupikia kwako mtaalamu.
 
Back
Top Bottom