SoC04 Tanzania izaliwe upya 2025

SoC04 Tanzania izaliwe upya 2025

Tanzania Tuitakayo competition threads

Zakayo miho

New Member
Joined
Feb 18, 2020
Posts
1
Reaction score
2
Nimushukuru mwenyezi mungu Kwa kunipa afya njema nami niwakaribishe watanzania wenzangu katika #storyofchange na jamii forums.

Kama ambavyo bendera yetu ikiwakilisha rangi zake nne blue(bahari na mito), nyeusi(watu), kijani(uoto) na njano(madini) .
Picsart_24-06-21_21-53-02-118.jpg
picha na wikipedia.
Rasilimali hizi zimekuwa zikifumika kawaida Sana na so Kwa kiwango kile nachoona katika Tanzania niitakayo 2025.

Tanzania ambayo nahitaji yafuatayo.

I) Matumizi sahihi ya rasilimali watu, ambapo serikali Kwa kushirikiana na asasi za kiraia na pamoja na sekta binafsi ningeomba kushirikiana katika suala la ukusanyaji Kodi ambayo ungeleta mabadiliko makubwa Sana katika sekta zote afya, elimu, mawasiliano, na nyinginezo, ningependekeza ukusanyaji wa Kodi katika sekta ya simu au laini angalau 1000 Kwa mwezi mfano tigo Wana wateja 20 milioni ambapo tungepata Hela nyingi mno, uhamishaji wa bandari ambapo wateja wa Tanzania wanaenda kuchukua Mali Uganda au kenya na na kujipatia faida hivyo kupoteza mapato, ushuru wa pikipiki ambapo kama Kila leseni ingelipiwa tu shilingi 2000 Kwa mwezi tungekusanya pesa nyingi Sana

Ii) Rasilimali madini

Katika sekta hii ningependekeza Tanzania mpya ijikite katika uboreshaji wa miundombinu zaidi ya kisasa ambapo Kila Senti inayopatikana katika biashara ya madini ingesomeka kwenye mfumo ili tujikite kwenye kupata pesa zaidi ili kuboresha miundombinu yetu kwani Hela zinazopotea ni nyingi kuliko tunazokusanya

III) Rasilimali bahari,
Katika kitega uchumi hiki haaa sekta ya uvuvi Kuna Hela nyingi Sana kwanza ingefungwa mitambo ya kisasa Kwa akili ya kukusanya mapato ilihali wavuvi wangeboreshewa maeneo Yao naona tutapata ajira na pesa nyingi Sana pia tuongeze Kodi ya shilingi 1000 Kwa Kila kichwa Cha mvuvi ili tupate Hela nyingi zaidi

iv) Ardhi au kilimo. Kama takwimu zisemavyo kuwa 80% ya watanzania ni wakulima hivi basi ningependekeza Kodi ya ya shilingi 500 Kwa Kila debe liuzwalo ili kutoa mapato zaidi ila kuboresha maisha ya wakulima ikiwemo kupata mbolea Kwa bei nafuu na mbegu bola ivyo irahisishwe mikopo hasa Ile ya asilimia 10 wasijimilikishe vigogo wa serikali Bali iwafikie vijana ili walime na kujipatia ajira na vyama vya ushirika vianzishwe upya ili kupata solo la pamoja.

Vikwazo vya Tanzania inayozaliwa upya inabidi viuliwe ni kama ifuatavyo.
I)Ufisadi, wakati tukipambana kukusanya Kodi za walalahoi Kuna watu Kwa maksudi wanadhoofisha mapambano haya wanaitwa wezi au mafisadi,pendekezo ni kufunga vifaa vitakavyofatilia pesa za serikali ikiwe CCTV na mifumo mingine ili Kila kitu kiwe wazi .

II) Rushwa,adui mkubwa kabisa ni huyu kwani huleta vitu visivyo na weledi Kwa maana ya viongozi na watendaji wa hovyo kwani huacha wenye haki na kuchukua waso na haki na huwa ni chanzo Cha kuua maendeleo.hivyo basi tanzania ili izaliwe upya tungezingatia utoaji wa mifumo yetu kama vyeti na kazi ili wapite wenye haki tu

Machache ni hayo tu ni Mimi. Zakayo miho
 

Attachments

  • Picsart_24-06-21_21-53-02-118.jpg
    Picsart_24-06-21_21-53-02-118.jpg
    99.1 KB · Views: 1
Upvote 2
Back
Top Bottom