Thony Rweich
New Member
- Jan 5, 2022
- 1
- 0
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizomo katika Ushirikiano wa Kusini-Kusini (South South developing countries). Ushirikiano huo unaashiria ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni kati ya nchi zinazoendelea Kusini mwa Dunia, lengo likiwa ni kupunguza utegemezi wa nchi hizo kwa Kaskazini mwa Dunia na kupinga ukandamizaji wa Magharibi (nchi zilizoendelea) katika mahusiano ya kimataifa. Ushirikiano huu pia unahusu kuleta changamoto za pamoja, na maslahi ya pande zote kati ya nchi za Kusini.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa India, Jawaharlal Nehru (1946), alihimiza nchi zinazoendelea kushirikiana ili kupambana na changamoto zao za pamoja na kufikia uhuru wa kiuchumi. Aliamini kwamba nchi za Kusini zingeweza kujifunza kutoka kwa uzoefu wa nchi nyingine na kufanya kazi pamoja kupinga utawala wa nguvu za Magharibi.
Kwa muktadha huo, aliyekuwa rais wa Tanganyika na baadae muasisi wa taifa la Tanzania, mwal. J. K. Nyerere, hakuwa mbali katika kuipaisha Tanzania kiuchumi. Kwa siasa na sera zake za ujamaa na kujitegemea aliyetaka mshikamano wa nchi zinazoendelea dhidi ya ukoloni na ukoloni mamboleo. Kuanzia uongozi wa hayati J K Nyerere, kufuatia hayati sheikh Ali-hassan Mwinyi, kisha; hayati, Benjamin Mkapa, akifuatiwa na marais Jakaya kikwete, na hayati; John magufuli na sasa rais Samia Suluhu Hassan, Tanzania imepitia katika sera mbalimbali na mipango mingi ya maendeleo. Kiuchumi mipango hiyo iliweza kufanikiwa kwa kiasi fulani lakini bado Tanzania inajumuishwa katika nchi za ulimwengu wa tatu wakati nchi nyingine kama vile India, china, Korea ambazo miaka ya 1960 zilikua sawa kimaendeleo zimepiga hatua kubwa kuliko.
Kama inavyoonekana, ushirikiano wa Kusini-Kusini (nchi zinazoendelea) umepata sura mpya na kupata muelekeo mpya kutokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa. Tanzania inatakiwa kuiga mfano kutoka nchi zinazoinuka ambazo miaka ya nyuma zilikua sawa kimaendeleo, kama vile China, India, Brazil, na Afrika Kusini, lakini kwa sasa zipo mbele Zaidi kuliko Tanzania hususan kiuchumi.
Mfumo wa kisiasa Tanzania: Sekta au eneo la kisiasa linabaki kuwa eneo muhimu Katika kuleta maendeleo. Tanzania kama nchi inayoendelea, inakabiliwa na tatizo la mfumo mbovu wa kisiasa ikilinganishwa na mataifa mengine. Hii inaweza kuwa kutokana na historia ya ukoloni na pia kutokana na sababu za ndani kama vile, ubovu wa katiba, kutokufuata sheria na hivyo kusababisha kukithiri kwa rushwa na uongozi dhaifu. Tanzania, inapaswa kujiboresha kisiasa kwa kufanya marekebisho na mageuzi makubwa katika mfumo wa kisiasa na kuhakikisha masuala ya utawala bora, kuhuishwa kwa miundo ya kisiasa, na kuhakikisha mazingira ya kidemokrasia yanayosababisha upatikanaji wa haki za binadamu ni muhimu kwa maendeleo.
Ushirikiano wenye tija na mashirika binafsi; Tanzania kuna mashirika mengi yasiyo ya kiserikali ambayo yanafanya kazi pamoja na serikali kukuza maendeleo kwa taifa na kwa mtu mmoja mmoja. Lakini,kwa bahati mbaya mashirika mengi hususan mashirika binafsi kutoka nje ya nchi yamekua ni ya kinyonyaji kwa asili. Mengine yameingizwa Tanzania kwa mfumo mbovu wa kisera hivyo uhalali wake upo ndani ya mikataba mibovu tena ya muda mrefu. Wakati mwingine mikataba hiyo haiwekwi wazi kwa maelezo kamili au kutokujulikana kabisa. Mfano, mkataba na hati za makubaliano juu ya bandari, mbuga za wanyama na baadhi ya maeneo tengefu. Kwa hali hiyo inasababisha hasara kubwa kwa taifa, hivyo lazima kuwe na ushirikiano wenye tija kati ya taifa na haya mashirika binafsi.
Rasilimali watu na sera za idadi ya watu; taifa la Tanzania kwa kuwezesha watu wake kutambua uwezo wao kamili wa vipaji na ubunifu na maarifa mbalimbali, na kwa kuboresha mfumo wa ajira na kazi zisizo rasmi kutapelekea taifa hili kupiga hatua kubwa kimaendeleo. Sensa zinazofanyika kila baada ya miaka kumi zinapaswa kutumika vizuri kupanga mipango mikakati ya maendeleo. Suala hili la rasilimali watu halipaswi kufanywa wala kuchukuliwa kisiasa. Dosari iliyopo ni kuwa, Tanzania haifanyii kazi idadi ya watu inayotolewa wala serikali haonekani kujali katika kupanga mipango mikakati mbalimbali.
Matumizi na mikakati sahihi ya sayansi na teknolojia kwa ajili ya maendeleo; taifa la Tanzania linapaswa kuwa bunifu na kuhamasisha maendeleo sayansi na teknolojia kupitia taasisi mbalimbali kama vile COSTECH. Tanzania inapaswa kujifunza kwamba haitakuwa rahisi kuchukua teknolojia mpya kwa njia inayofanana na kuunga mkono mwelekeo mpana wa baadaye. Kwa mfano, mwezi uliopita kulikua na utambulisho wa roboti Eunice. Teknolojia ile ya roboti kwa mfano ule wa Eunice ni kiashiria kimojawapo cha kuonesha kufeli kwa taifa hili katika nyanja ya teknolojia. Haiwezekani kuanza kwa maroboti wakati sekta muhimu kama vile kilimo, elimu, nk hakuna teknolojia bora inayotumika kuinua taifa katika sekta hizo muhimu.
Kwa kuhitimisha; Uchambuzi wa kina unaonyesha kwamba nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania zinakabiliwa na changamoto nyingi zinazokwamisha maendeleo ya kiuchumi. Kwa hivyo serikali ijikite zaidi katika kupambana na matatizo ya ndani ya nchi kuliko kuwa tegemezi kwa mikopo kutoka nje ambayo italigharimu taifa hapo baadae.

Upvote
0