Tanzania kama nchi tujipange kurekebisha uchumi wetu

Tanzania kama nchi tujipange kurekebisha uchumi wetu

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Kila kukicha uchumi wetu unaporomoka. Leo hii Dollar moja ya Kimarekani kwa ubadilishaji(exchange rate) inakimbilia kuwa T.shs.3,000. Wenzetu wa Kenya juzijuzi fedha yao ilikuwa inabadilshwa kwa Dollar moja ya Kimarekani (exchange rate) Ke 163 na sasa imeshuka mpaka Ke 143 kwa Dollar moja.

Kwa taarifa yao wanasema kuwa ifikapo Septemba, 2024 Dollar moja ya Kimaarekani itabadilishwa kwa Ke 100 kama ilivyokuwa hapo zamani. Sisi Tanzania badala ya fedha yetu kupanda kwa thamani kila kukicha shillingi yetu inaporomoka. Tunaye Waziri wa Fedha na tunaye Gavana wa Benki Kuu. Ninauliza tumekosea wapi?. Je hatuna watalaam wa uchumi?.
 
subiri waje kujibu kisiasa tena kirahisi kabisa.

Watakuja kukwambia ni tatizo la dunia nzima linasababishwa na vita ya Ukraine Vs Russia, Houthis Vs Israel/USA/EU nk, Israeli Vs Palestine na tension between Israel and Iran, na mwisho kabisa watakujibu it's due to COVID crisis, hujakaa sawa watakwambia shida ni
marehemu JPM.

Kazi ya kiongozi ni kutafuta suluhu ya matatizo na sio kuleta malalamiko, kazi ya kiongozi ni kuleta suluhu ya matatizo magumu na sio issue nyepesi nyepesi ambazo kila mtu leo hii mwenye akili ya kawaida anaweza kutatua.

Tunahitaji watendaji mahili kwenye public sector wabobezi na wenye exposure yakupambana na mambo magumumagumu nakuyaletea suluhu na kuleta matokeo chanya yenye impact kwa kila mwananchi na Taifa kwa ujumla.

Tuna homework nyingi sana za kufanya zitakalofanya Taifa liwe na uchumi imara na hali Bora za maisha ya watu - Homework hizi zinahitaji watu Bora wenye extra heads na sio akili za kawaida ambazo kila mtu anazo.
 
Wizara yetu itatwambia tunahitaji miezi sita kuweka mambo sawa plus research juu
 
Pale juu ndio tatizo, ameteua waziro wa fedha anayekubali madudu anayoyataka. Kama ilovyokuwa awamu ya nne tu. Nidhamu ya matumizi ni zero.

Uchumi wa nchi unachezewa kwa anasa za viongozi na maslahi ya wafadhili wao kwenye mabiashara yao.

Kwahiyo namna pekee ya kuuokoa uchumi wa nchi hii ni kifanya mabadiliko pale juu.
 
Nimekuelewa na uko sawa. Kila mara ni kupiga magoti kuomba mikopo na mikopo yenyewe ni ya kutisha. Hivi sasa fedha zote wanazosema Mama ameleta kwenye Vijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mikoa na hata Taifa ni fedha zilizotokana na mikopo. Ni lini tukajisimamia hata kwa asilimia 60 kwa fedha zetu wenyewe.
 
Back
Top Bottom