Tanzania kama Ulaya

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Kuna ukweli gani, naona tunazidi kudidimia kiuchumi kwa hali ya mmoja mmoja, watu wapo taabani bin hoi na shida ya mlo mmoja kwa siku inazidi kukuwa, wananchi wanaishia mihogo kwa chai mkate na jam ni nyumba zile tu, kwengine ni kauzu inayoliwa kidogo kidogo.

Kwanini Serikali haianzishi mfumo wa kuwalipa wananchi? wasio na kazi japo laki moja kwa mwezi? Kama kianzio na kwa mfumo wa wale waote wenye passport na kadi ya Uraia? Malipo kwa wananchi yaliwahi kuvuma katika sera za CUF miaka iliyopita kuwa wakishika hatamu za nchi basi wananchi wote watapata sehemu katika tunda la Taifa kwa maana watakuwa kuna malipo flani wanalipwa kila mwisho wa mwezi, yalihabarishwa katika mikutano ya CUF ya wakati huo kule Zanzibar na ndio ukaona wananchi wa Zanzibar wanailaza CCM kila uchaguzi ila kama tunavyojua mageuzi ya uchaguzi yanawachelewesha katika kuindea fikra ya kulipwa kwa mwananchi.

Hivi CCM haiwezi kuivaa sera hii na kuianzisha kimkoa ,ijulikane raia wa mkoa fulani hulipwa 5000/ shilingi kila mwezi ,kama kianzio cha mfumo huu.

Uhuni ukahaba unaokuwa kila siku hapa Tz ni kwa wananchi kukosa hela ya kupata mlo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…