Tanzania, Kenya, Uganda zaomba kuandaa AFCON 2027 kwa ushirikiano

Tanzania, Kenya, Uganda zaomba kuandaa AFCON 2027 kwa ushirikiano

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
TFF.jpg


Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limepokea maombi kutoka nchi sita zinazowania uenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 ikiwemo Tanzania.

Jumla ya waombaji sita wamefanikiwa kuwasilisha maombi yao ambao ni Algeria, Botswana na Misri huku Kenya, Uganda na Tanzania zimewasilisha maombi ya kuandaa fainali hizo kwa pamoja.

Hatua inayofuata ni kuwasilisha zabuni ya mwisho ifikapo Mei 23, 2023 ikijumuisha nyaraka zote (makubaliano ya uenyeji, makubaliano ya miji mwenyeji, dhamana ya serikali, na nyinginezo).

Ukaguzi utaanza kufanyika Juni 1-15, 2023 na uamuzi wa nani atakuwa mwenyeji wa fainali hizo utafanywa na Kamati ya Utendaji ya CAF.
 
Bid itafeli sababu timu zote tatu hazina kawaida ya Ku qualify...

Zikipewa kuandaa ina maana zitapewa nafasi ya kushiriki kama wenyeji ...Kwa timu zote tatu....

Hawatakubali
 
Tuombee Ombi letu likubaliwe, najua fainali za AFCON zitachochea Uchumi wetu kupitia Utalii na biashara za Hotel n.k
 
2019 tulienda wote mbona
Bid itafeli sababu timu zote tatu hazina kawaida ya Ku qualify ...
Zikipewa kuandaa ina maana zitapewa nafasi ya kushiriki kama wenyeji ...Kwa timu zote tatu....
Hawatakubal
 
Uganda wale wale ambao leo hawana uwanja hata mmoja wenye viwango vya CAF, wanahangaika tu huku na huko kucheza mechi zao, leo wako Misri kesho wanachezea Cameroon.

Kenya hawa hawa ambao walikuwa wamefungiwa kwa muda mrefu na wamefunguliwa tu hivi karibuni.

Tanzania hii hii ambayo tuna uwanja mmoja tu uliokuwa na viwango na ambao tumeonekana hatuna pesa za kuukarabati uendane na viwango vyao hadi CAF wametupa msaada na favour za Simba waliojitolea kukarabati sehemu ya uwanja.

Tumekurupuka na hatuko serious. Watu wanatafuta sifa za kisiasa waonekane wamejaribu na wanajali.
 
Hii bid tutafeli. Bora hata maombi yangekuwa ya nchi moja.
 
Back
Top Bottom