Tanzania, Kenya zaingia kwenye mvutano

Prisoner

Senior Member
Joined
Jan 26, 2010
Posts
119
Reaction score
0
Hii habari niliipata kwenye VOA sasa nashindwa kuelewa kwa nini Tanzania na Kenya zimeingia kwenye Mvutano au wanataka huu ushirikiano ufe kwani Tazania inataka kuuza Pembe za Ndovu nje ya Nchi na huku Kenya ikikataa Tanzania kujihusisha na Biashara hiyo kwani ukiangalia nyuma ya Pazia Kenya inaongoza East Africa kwa kuuza Nje Pembe za Ndovu tena wanakuja kuwinda Tanzania sasa wanaona Tanzania nayo ikiingia kwenye hiyo biashara itakosa mapato JE tuishauri vipi Serikali ya Tazania au Kenya? na je tukiwashauri wote wakae kimya atakaye pata soko sawa na sisi tulinde mipaka yetu wasije kuwinda kwetu.? Je ushirikiano utakuwepo?
 
nani aliwaruhusu kuja kuwinda? kwani sisi hatuwezi? elimu ndogo jamani.
 
Aha!! Wewe Tanzania Elewaneni na Jirani kisha endelea kufanya biashara je itakuwa kwa faida ya nani??
 
-Hivi sisi ni kitu gani kinachotufanya tuwe wanyenyekevu kwa wenzetu hawa? Tanzania iaangalie jinsi ya kujibu hizi move za wakenya.

_sijui viongozi wetu wakoje,i really doubt their patriotic spirit...sasa huku kwenye common market tumeingia na still tunachezeana rafu kibao.

-Tanzania tuwe makini sana isije ikawa tutakuja fanyiwa mambo kama ambayo India wanafanyia Nepal baada ya kuruhusu free movement of labour accros border na matokeo yake wahindi ndiyo wanaongoza kumiliki properties,and Emplyment in Nepal.

-Tanzania tuwe more agressive katika hili tuache masikhara.
 

Hii issue ni ndogo na imekwisha kuwa discussed na wala hakuna mgogoro wowote. Suala lenyewe ni kuhusu pembe za ndovu zilizo vunwa au kukamatwa Tanzania sasa Tanzania wanataka wauze pembe hizo lakini Kenya na nchi nyingine wanasema zikiuzwa zitachochea uwindaji haramu wa ndovu ndo maana Kenya wanasema kama Tanzania haina mahali pa kuhifadhi hizo pembe za ndovu basi wawape Kenya wawahifadhie lakini siyo kuziuza kwa sasa.

Kwa hiyo mtoa mada hakuna mgogoro hapo isipokuwa serikali ya Tanzania inaangalia kama ikubaliane na ushauri wa kenya na nchi zingine au la.
 

Hakuna sehemu ya kuhifadhi pembe za ndovu Tanzania? duh!

Kwa unahitaji nini kuhifadhi hiyo mali ya nchi mpaka wapewe manyang'au?

Itafika siku tutasema hatuna pa kuhifadhi Dhahabu na Almasi za nchi yetu..really are we serious?
 
Hakuna sehemu ya kuhifadhi pembe za ndovu Tanzania? duh!

Kwa unahitaji nini kuhifadhi hiyo mali ya nchi mpaka wapewe manyang'au?

Itafika siku tutasema hatuna pa kuhifadhi Dhahabu na Almasi za nchi yetu..really are we serious?


Kumbe wewe ni ......... ok.
 
Hakuna sehemu ya kuhifadhi pembe za ndovu Tanzania? duh!

Kwa unahitaji nini kuhifadhi hiyo mali ya nchi mpaka wapewe manyang'au?

Itafika siku tutasema hatuna pa kuhifadhi Dhahabu na Almasi za nchi yetu..really are we serious?

Mbona unapenda kukurupuka kila mara bila kusoma vyema na kutafakari??
 


Tuwekee source kwamba hakuna mgogoro. Then unasema zihifadhiwe ili iwe nini? Tanzania wanataka kuuza labda useme Kenya wanataka kununua?
 
Sijawaelewa wachangia mada nidadavulieni kiduchu.. Tanzania haina sehemu za kuhifadhia hizo mali za nchi???? au
 
Wana JF naona mnataka kidogo kupotosha mada kwani mpaka source nimewapa sasa mnakuwawagumu nini kuelewa? Msichanganye na zile zilizokamatwa kule Vietinam na Uphilipino Hapana hii ni ishu ingine kabisa au niwape maaelzo ya zile zilizokamatwa katika nchi nilizotaja?? kwani zile zilizokamatwa kulikuwa na agreement katika ya Tanzania, Kenya and Zambia, na hii ni Ishu Current kabisa fuatilia VOA
 
hakuna sehemu ya kuhifadhi pembe za ndovu tanzania? Duh!

Kwa unahitaji nini kuhifadhi hiyo mali ya nchi mpaka wapewe manyang'au?

Itafika siku tutasema hatuna pa kuhifadhi dhahabu na almasi za nchi yetu..really are we serious?

yale yale ya samaki wa maghufuli. Wanatafuta mhindi wa kuzitunza hizo pembe
 
Wacha1 mkubwa weka source basi tujiridhishe kwani unajua hili suala ni nyeti sana sio kulichukulia kimzaha mzaha
 
Haya mambo ya kuungana ungana ndiyo yanaleta matatizo yote haya, kwani Mungu aliyetenganisha kila mtu na sehemu yake alikuwa hana akili????!!! acheni hizo
 
Hapa ni Comperative kwa kila Nchi hivyo kuhusu biashra ni lazima kuacha kila Nchi ifanye vile inavyojua kuliko kuwa hivi Tanzania endelea kuuza na kuunza kufanya biashra hiyo bila ufisadi katik yake
 
Wacha1 mkubwa weka source basi tujiridhishe kwani unajua hili suala ni nyeti sana sio kulichukulia kimzaha mzaha

Hii story ipo kuna member moja anasema hakuna mgogoro wowote pengine yeye ni Mkenya au ana sababu maalum.

Links hapa chini:


http://www.thecitizen.co.tz/newe.php?id=17114

Another one ... ...

2nd February 10

Namibia backs Tanzania in ivory sale row with Kenya



THE GUARDIAN
http://www.ippmedia.com/frontend/fun...le.php?l=13112

Aliyesema hakuna utata atwambie wapi walipokubaliana .... ..
 
-Hawa Kenya waache zao,hawa wanakuaga na mbinu chafu sana.Kama siku moja nitakua rais wa hii nchi ni kuhakiksha naingiza mashushu huko kenya kupata dataz na nitawachukulia hatua kali za kibiashara ktk propaganda na sekta ya utalii
 
'Enyi Wadanganyika ..., ambao mkataba na Sheria ya EAC imeweka wazikwamba Tanzania haina tena mamlaka ya kujiamulia mambo yake yenyewe kwenye utalii, wanyamapori na maliasili NYINGINE ZOTE, kwa vile, kama ambavyo imekabidhi sovereignty yake to EAC, maliasili na utalii si tena mali ya Tanzania pekee :

Sioni kwa nini mnapiga kelele wakati Tanzania inapozuiwa kuuza pembe za ndovu! Kwa sababu Tanzania imesaini kwamba kila kitu ilichonacho si mali yake pekee tena! See those reported quotes.

Surely, reading the actual Act may yield even more surrender of what used to be our very own Republic of Tanzania.

As the British say, 'Put up or shut up' -- either let's get out of this mess *NOW* or let's just in a docile way watch our country crumble unceremonially...
 
So, the news media give unwarranted credit to Tanzania as to mean there has been any row... which row? Tanzania has accepted that *ALL* natural resources are no longer Tanzania's, but EAC's. Last time I checked out, elephants and their tusks are a subset of wildlife which we cannot manage alone...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…