Tanzania Kinara wa Uwekezaji Mkubwa wa Madini kwa Kampuni Kutoka Australia

Tanzania Kinara wa Uwekezaji Mkubwa wa Madini kwa Kampuni Kutoka Australia

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

TANZANIA KINARA WA UWEKEZAJI MKUBWA WA MADINI KWA KAMPUNI KUTOKA AUSTRALIA

-Asilimia 21 ya uwekezaji wa Kampuni kubwa za Madini za Australia Barani Afrika ni nchini Tanzania

-Kampuni zaingia mikataba ya uwekezaji wa zaidi ya Trilioni 10

-Miradi mipya kuongeza Mapato,Ajira na ushiriki wa watanzania

-Rais Dkt. Samia apongezwa kufungua uwekezaji

-Waziri Mavunde asisitiza manufaa ya uwekezaji huu kwa maendeleo ya Watanzania

Perth,Australia

Tanzania imetajwa kuwa nchi kinara kwa Bara la Afrika ambayo kampuni za Madini za Australia zimewekeza kwa asilimia 21% ya uwekezaji wote wa kwenye sekta ya madini.

Hayo yameelezwa leo Perth,Australia wakati wa mkutano wa Africa DownUnder(ADU) unaowashirikisha wadau wa madini kutoka Australia na Nchi za Bara la Afrika.

Akihutubia mkutano huo kwa niaba ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan,Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema mikataba ya madini iliyoingiwa kwa miaka miwili iliyopita baina ya Kampuni za Madini za Australia na Serikali ya Tanzania ina thamani ya zaidi ya Shilingi Trilioni Kumi na hivyo utekelezaji wake utasaidia kuongeza mapato ya nchi,kuongeza nafasi za ajira,ushiriki wa watanzania(Local Content) na kuchochea ukuajinwa sekta ya madini.

Aidha,Waziri Mavunde alizitaka kampuni hizo kuheshimu mikataba waliyoingina na serikali na hasa katika kunufaisha watanzania kupitia wajibu kwa jamii(CSR),utoaji huduma na usambazaji wa bidhaa migodini na ulipaji wa kodi na tozo stahiki ili rasilimali hizo zitoe mchango katika maendeleo ya uchumi wa nchi na watu wake.

Wakitoa mawasilisho yao Watendaji wa Kampuni za Chief , Walkabout Resources,Peak Rare Earths ,Black Rock Mining na Eco Graf kwa pamoja wameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na hivyo kuvutia uwekezaji huu mkubwa nchini ambao utachochea kukuaji wa kasi wa uchumi wa Tanzania.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.12.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.12.jpeg
    137.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.12(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.12(1).jpeg
    90.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.13(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.13(1).jpeg
    96.8 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.14.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.14.jpeg
    178.9 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.15.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.15.jpeg
    74.5 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.15(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.15(1).jpeg
    41.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.16.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.16.jpeg
    80.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.18.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.18.jpeg
    152.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.18(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-04 at 19.02.18(1).jpeg
    147.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom