Tanzania – Korea kuendelea kuwekeza katika kukuza biashara

Tanzania – Korea kuendelea kuwekeza katika kukuza biashara

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Kim, Sun Pyo ambapo ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania na wadau inaendelea kuweka jitihada katika kuboresha mazingira ya biashara baina ya Tanzania na Jamhuri ya Korea ili kuendelea kuinua kiwango cha biashara na uwekezaji baina ya nchi hizi mbili.

Dkt. Tax amemuhakikishia Balozi Kim kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Jamhuri ya Korea ili kuwezesha biashara baina ya pande hizo mbili inaendelea kushamiri zaidi tofauti na ilivyo sasa.

Dkt. Tax pia ameeleza baadhi ya hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania ni pamoja na kuendelea kutekeleza na kubuni programu zinazolenga kuongeza mwingiliano wa watu (people to people exchange) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea.

Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) za mwaka 2020, Korea iliagiza bidhaa zenye thamani ya shilingi za Tanzania bilioni 340.3 kutoka Tanzania, huku Tanzania ikiagiza bidhaa zenye thamani ya shilingi bilioni 290.3 kutoka Jamhuri ya Korea.

Untitled design (18).jpg
 
Back
Top Bottom