Tanzania kuandika historia siku ya leo kwenye bwawa la umeme la Nyerere

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Leo December 22 Rais Samia Suluhu atazindua hatua ya kwanza ya kuanza ujazaji maji katika bwawa la Nyerere (JNHPP) Ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 78.68.

Tanzania tunaandika historia ya kuwa na bwawa kubwa zaidi lenye uwezo wa kujaza maji lita Bilioni 32 na bwawa hili ni kubwa kuliko ziwa Rukwa, baada ya kukamilika kwa mradi huu mkubwa unaoshika nafasi ya pili barani Afrika watanzania tutaondokana na adha ya umeme maana bwawa hili litakua na uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115.

Rais Samia Suluhu alisema hakuna mradi uliosimama na kweli tunaona anaendelea kukamilisha miradi ya kimakakati yenye faifa nyingi kwa watanzania moja ya faida ni katika sekta ya kilimo, uvuvu, maji safi na salama pia kupitia bwawa hili miundombinu imeboreshwa na bwawa hili litakuza utalii.
 
Wacha wee!! pia kwa atakayekuwa maeneo ya huko leo mimi naomba atusomee nyuzi joto inasoma ngapi?
 
Pongezi kwa Rais wetu kwa kazi kubwa anayo ifanya ya kuhakikisha nchi inazidi kusonga mbele kimaendeleo.

wapo walio beza na kudhihaki kuwa asingeweza!!!
lakini leo hii wamebaki midomo wazi na sasa kazi yao iliyobaki ni kupotosha na kuziriba mambo makubwa na mazuri anayo fanya Rais wetu.

Tunamuomba Rais wetu na watendaji wake wasibabaishwe wala kuyumbishwa na makelele ya wazandiki ambao lengo lao ni kuona ana feli.

Kazi iendelee tusisikileze kelele za wazandiki.
 
Leo December 22 Rais Samia Suluhu atazindua hatua ya kwanza ya kuanza ujazaji maji katika bwawa la Nyerere (JNHPP) Ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 78.68...
Nenda na wakati badala ya kukimbilia kusifu, kwa taarifa yako huko kwenye bwawa la kwanza kwa ukubwa hivi sasa kuna mgao wa umeme, fulustopu.
 
Leo December 22 Rais Samia Suluhu atazindua hatua ya kwanza ya kuanza ujazaji maji katika bwawa la Nyerere (JNHPP) Ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 78.68...
Wazee wa kuandika historia bila kujali kitakachozalishwa

Sisi kila kitu ni kuandika historia na yanayofuata huwa worse
 
Leo December 22 Rais Samia Suluhu atazindua hatua ya kwanza ya kuanza ujazaji maji katika bwawa la Nyerere (JNHPP) Ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 78.68...
eti bwawa kubwa kuliko ziwa Rukwa....unaposifiwa kitu jitahidi uwe unatumia hata common sense hata kidogo tu
 
Kuna watu wanateseka sana wakiwa sehemu tofauti za Tanzania na duniani kwa ujumla.

SSH anafanya kazi kubwa kwa umahiri yale yale waliyomdharau kuwa hawezi kuyatimiza.
 
Bwawa linafanyika tukio la kisiasa
Zaidi uccm mwingi tu hapo na familia
Zao

Ova
 
Leo December 22 Rais Samia Suluhu atazindua hatua ya kwanza ya kuanza ujazaji maji katika bwawa la Nyerere (JNHPP) Ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 78.68.

Tanzania tunaandika historia ya kuwa na bwawa kubwa zaidi lenye uwezo wa kujaza maji lita Bilioni 32 na bwawa hili ni kubwa kuliko ziwa Rukwa, baada ya kukamilika kwa mradi huu mkubwa unaoshika nafasi ya pili barani Afrika watanzania tutaondokana na adha ya umeme maana bwawa hili litakua na uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115.

Rais Samia Suluhu alisema hakuna mradi uliosimama na kweli tunaona anaendelea kukamilisha miradi ya kimakakati yenye faifa nyingi kwa watanzania moja ya faida ni katika sekta ya kilimo, uvuvu, maji safi na salama pia kupitia bwawa hili miundombinu imeboreshwa na bwawa hili litakuza utalii.
Umeme wenyewe mmekata sasa watu watatizamaje hiyo shuguli yenu

Ova
 
Ngoja tuone wale wachezaji wa Pingapinga FC watakavyo shambulia Goli lako.
 
Pongezi kwa Rais wetu kwa kazi kubwa anayo ifanya ya kuhakikisha nchi inazidi kusonga mbele kimaendeleo.

wapo walio beza na kudhihaki kuwa asingeweza!!!
lakini leo hii wamebaki midomo wazi na sasa kazi yao iliyobaki ni kupotosha na kuziriba mambo makubwa na mazuri anayo fanya Rais wetu.

Tunamuomba Rais wetu na watendaji wake wasibabaishwe wala kuyumbishwa na makelele ya wazandiki ambao lengo lao ni kuona ana feli.

Kazi iendelee tusisikileze kelele za wazandiki.
Hakuna mradi mkubwa aliouanzisha kwa karibia miaka miwili ya uongozi wake ukiachana na miradi ya pesa za COVID
 
Mpaka sasa wapinga maendeleo wameshindwa hawana jipya Rais Samia Suluhu anaendelea kuwa prove wrong
 
Hakuna mradi mkubwa aliouanzisha kwa karibia miaka miwili ya uongozi wake ukiachana na miradi ya pesa za COVID
Miradi iliyoachwa yote anaikamilisha pia Rais Samia Suluhu ndani ya huu mwaka mmoja amejenga shule Elf 15 kuna miradi mingi sana ametekeleza fatilia utaona
 
Back
Top Bottom