joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Baada ya kuiongoza Afrika katika vita vya kulikomboa bara la Afrika, sasa hivi Tanzania imeanza kuiongoza tena Afrika katika vita vya kiuchumi, kuhakikisha kwamba, bara la Afrika linakoma kuwa sehemu ya kutajirisha mataifa ya nje.
Tanzania imetoa masharti mazito kwa China kama inataka kuwekeza katika bandari ya Bagamoyo. Ikumbukwe kwamba huwa wawekezaji ndio wanaotoa masharti, ila Tanzania imeanza kutumia mfumo mpya kabisa kutumika hapa Afrika, kwamba muwekezaji anakutana na masharti tayari, akikubaliana nayo ndiyo aweze kuwekeza.
Ni matumaini yangu kwamba jirani wetu atajifunza na ikiwezekana akapitie upya ule mkataba wa SGR.