BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema Benki ya Dunia imeitengea Tanzania Dola za Marekani Bilioni 2.1 (Trilioni 4.9) katika mzunguko wa 20 wa IDA (Julai 2022-Juni 2025) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayokusudia kukuza uchumi wa Nchi pamoja na kupunguza umasikini.
Waziri Mwigulu amesema hayo wakati akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia Nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Victoria Kwakwa wakati wa Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoendelea Mjini Washington DC, Marekani.
Kati ya kiasi hicho kinachotolewa na Benki ya Dunia kama mkopo nafuu kwa Tanzania, jumla ya Dola za Marekani Milioni 535 sawa na 25% ya mgao tayari zimeshaidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Kusambaza Umeme Vijijini (Dola za Marekani Milioni 335) na Uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi (Dola za Marekani Milioni 200).
Aidha, Bodi hiyo inatarajiwa kuidhinisha Dola Milioni 150 hivi karibuni kwa ajili ya utekelezaji wa mradi maji safi na usafi wa mazingira vijijini.