JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Pichani ni nakala ya fomu ya maombi ya kurudisha namba ya simu iliyopitea. Hata hivyo nyaraka hiyo iliyosheheni taarifa nyeti za mteja wa Kampuni hiyo ya mawasiliano ilitumika kutengenezea bahasha katika Duka la Dawa
Nyarahiyo yenye jina, namba ya simu na miamala ilitumika bila ya kufutwa kwa taarifa hizo ambazo zinaweza kutumia vibaya dhidi mhusika
Sheria za #UlinziWaData katika Mataifa mengine huwataka watoa huduma kulinda taarifa za Wateja wao na kuzihifadhi kwa usahihi
Aidha, taarifa ambazo matumizi yake umekwisha basi sheria huwataka Watoa huduma kuziharibu kwa kuzingatia usalama wa mteja
Picha hii ni karatasi ya maombi ya namba ya simu ya mteja wa Kampuni ya Airtel iliyojazwa mnamo 21 Desemba 2016
Upvote
1