kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kiongozi wa kitaifa hapaswi kufikiria na kutenda kikabila, kijimbo, kidini, kijinsia au kikanda maana watu wote (makabila, dini, majimbo, wilaya, mikoa, jinsia, kanda) kwenye taifa wanamtegemea. Unapomsikia na kumuona kiongozi wa nchi anafikiria, anatenda, anaagiza na kupeleka maendeleo kwa kufuata kijiji chake, mtaa wake, kabila lake, jimbo lake, mkoa wake, jinsia yake, dini yake au kanda yake alikotoka huyo hana tofauti na Gashangwa, aliyekuwa Naibu Rais wa Kenye alitimuliwa kwa kutaka kuwapendelea wa kwao wa Mlima.
Tanzania maendeleo yatapelekwa kwa kuangalia kiongozi yupi na ukubwa gani anatoka wapi, kabila gani, jimbo lipi na jinsia ipi. Jimbo la kiongozi lazima umeme uwake haraka, maji yapelekwe haraka, barabara za lami zijengwe haraka, hospitali ijengwe haraka, uwanja wa ndege ujengwe upesi na hata mbuga za wanyama zisikose.
Hatuwaoni? hatujui? au hatuwezi?