Chani Mohamedi
Member
- Jul 13, 2021
- 5
- 6
Mazingira ya biashara ni nini? Ni yale mambo yote ambayo yanaweza kuchochea biashara kukua au kudidimia katika muktadha tofauti tofauti. Katika suala zima la kujua ni yapi mazingira mazuri ya kibiashara ni vyema kujua kile unachotaka kufanya katika biashara yaani ni biashara ipi unataka kufungua. Tanzania kuna mazingira mbalimbali ya kibiashara ambayo mtu anatakiwa kuyafahamu na namna yanavyoweza kumsaidia kuyatumia kukuza biashara yake.
mazingira ya kibiashara nchini Tanzania
1. Mazingira ya kiteknolojia
Tanzania ni nchi ambayo jamii kubwa kwa ujumla inapambana kuendana na ukuaji wa kiteknolojia. Na vile vile serikali ikiwa katika mikakati ya kuboresha miundo mbinu ya kiteknolojia kupitia uhamasishaji sera ya viwanda. Kupitia teknolojia ya mitandao watu wengi wapo katika mitandao ya kijamii ambayo kwasasa mtu huweza kuitumia kama furusa ya kutangaza biashara.
2. Mazingira ya kiuchumi
Uchumi pia ni sehemu ya mazingira katika biashara. Uchumi unaweza kuhamasisha uanzishaji na uchocheaji wa biashara. Nchini Tanzania kuna sera mbalimbali ambazo hushawishi mtu kuchagua aina fulan ya biashara na pia ukuaji wa biashara kiujumla. Mfano sera ya uboreshaji wa miundo mbinu ambayo lengo lake ni kurahisisha usafirishaji hii itamsaidia mtu kurahisisha biashara yake katika kuwafikishia huduma wateja wake popote walipo. Sera ya fedha katika udhibiti wa mfumuko wa bei katika bidhaa nchini pia humsaidia mfanyabishara kujua bidhaa ipi inaweza kuwa na soko zuri hivyo kuchagua biashara itakayomfaa.
3. Mazingira ya eneo la bishara kwa upande wa washindani wako wa biashara unayotaka kuifungua eneo fulani. Unaweza kutumia wafanya biashara ambao wanafanya biashara hiyo unayofanya kujua kipi cha kuongeza katika biashara unayotaka kufanya. Mfano kama unataka kufungua biashara ya nguo na eneo unalotaka kufungua biashara hiyo wapo watu wa aina hiyo hiyo wanaouza nguo ni vyema kufanya ubunifu utakaokufanya utofautiane na wao ili kuwavutia wateja zaidi.
4. Idaidi ya watu katika eneo la kuanzisha biashara. Mazingira mazuri ya kibiashara ni yale yenye wateja wengi ambao wataweza kununua bidhaa yako kwa uwingi. Mfano hapa Tanzania wengi wetu hutoka vijijini kuelekea mjini kwa lengo la kutafuta furusa za kibiashara na hii ni kutokana na uwingi wa watu ambao wapo maeneo ya mjini.
5 Mabadiliko ya hali ya hewa ambayo hubadilisha muelekeo wa masoko. Ni vyema mfanya biashara kuangalia namna anayoweza kuendana na ubadilikaji wa hali ya hewa na muelekeo wa soko. Mfano uwepo wa korona umefanya biashara nyingi kufungwa kutokana na biashara nyingi kuweza kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya masoko. Mfanya biashara inabid kuwa na mikakati madhubuti kwa ajili ya kuweza kubadilika kulingana na mabadiliko ya mazingira ya kibiashara
KIVIPI MAZINGIRA NI FURUSA YA KIBIASHARA HAPA TANZANIA
Mazingira ni furusa kulingana na utakavyoyatumia katika kuanzisha na kuendesha biashara yako. Hapa nchini Tanzania kuna furusa ambazo zinapatikana katika mazingira mbalimbali mfano
1 Mazingira ya mjini . Miji kama vile Dar es salaam , Mwanza na sehem nyinginezo ina furusa mbalimbali kutokana na uwingi wa watu. Mtu huweza kutumia uwingi wa watu kufungua biashara anayohisi inaendana na mtaji wake na akapata wateja. Kama vile uuzaji wa nguo. Uzaji wa vyakula na bidhaa mbali mbali
2. Utumiaji wa Teknolojia. Mfanyabiashara anaweza kuitumia furusa ya kiteknolojia kukuza biashara na pia kujiongezea kipato kwanjia ya teknolojia. Teknolojia hapa nchini imesaidia watu wengi hasa wajasiriamali kukuza biashara kupitia mbinu mbalimbali za kuwasiliana na jamii iliyopo katika mitandao ya kijamii. Sasa hivi watu wengi hutumia mitandao ya kijamii kama instagram, twitter, facebook na mingineyo katika kutangaza biashara, na ubunifu wao kwa ujumla. Mitandao ya kijamii huchochea ukuaji wa kibiashara na pia humfanya mtu mwenye ubunifu kupata furusa ya kiajira kama vile wenye talanta mbalimbali huitumia youtube kujipatia fedha.
3 Mabadiliko ya mwenendo wa masoko kulingana na matukio na muktadha mbalimbali. Katika mabadiliko mjasiriamali anaweza kutatumia vyema katika kubuni biashara mpya ama kukuza biashara mfano kuzuka kwa ugonjwa wa corona wajasiriamali baadhi yao nchini wameitumia nafasi hii vyema kutengeneza barakoa na hata kubuni huduma mbadala kama vile huduma za usafirishaji bila gharama kwa watu waliopo ndani ya mkoa wa mfanya biashara (free delivery within business region) kwa ajili ya kuongeza idadi ya wateja hata wale ambao hawataki msongamano wa kufika eneo la biashara kuepuka maambukizi . Ubunifu ni muhimu katika kujiandaa na mabadiliko ya kibiashara kwa wenye kuanzisha biashara na wale wenye kuendeleza biashara.
4. Ukuaji wa uchumi. Hapa nchini Tanzania katika swala la uchumi kwasasa sio kama miaka mitano kurudi nyuma kutokana na maboresho ya sekta mbalimbali mfano miundo mbinu ya usafiri ambayo inaweza kuchochea mtu kufanya huduma za kiusafiri kama vile bajaji, bodaboda na hata usafiri wa daladala kutokana na maboresho ya barabara hasa mijini. Vile vile huchochea huduma ya usafirishaji wa bidhaa kutoka mjini hadi mkoani. Uboreshaji wa mzunguko wa fedha ambapo serikali ina mpango wa kuongeza mzunguko wa fedha kuufanya uweze kusawazisha tatizo la tozo katika mfumo wa utoaji na uwekaji pesa kwenye simu hii itasaidia upatikanaji wa pesa katika wananchi na kusaidia kuwepo kwa riba na fuu kwa wenye kuhitaji mikopo ya kibiashara.
HITIMISHO;
Watu wengi hasa wajasiriamali wadogowadogo hushindwa kutambua aina ya mazingira na biashara anayotaka kuanzisha au wapi biashara yake inafaa kuanzisha na kupelekea biashara yake kudumaa au kufa. Ni vyema kujua mazingira halisi yatakayosaidia kukuza biashara yako.

Upvote
5