Kuna upande mwingine usioujua, sikiliza :
Siasa ni Rufaa ya Sauti ya Watu
Source: Kwanza TV
Wana bodi ni ukweli kwamba serikali na kundi lake wameamua kutudanganya kwamba miradi inaendweshwa kwa fedha za ndani bila hata aibu.
Tunapo sema fedha za ndani tuna maana kwamba ni zile tunazo kusanya kupitia TRA, taasisi za serikali kama TCRA, polisi , mahakama etc.
Wakati mawaziri wa africa na nordic walipotembelea ujenzi wa SGR waziri wa mambo ya nje wa nigeria alisema si vibaya kusema tumejenga kwa mkopo kwa sababu bado ni mradi wenye nia njema kwa nchi na africa kwa ujumla baada ya kusikia tunasema tunajeng kwa fedha za ndani kitu ambacho hata mtoto mdogo hawezi kukubali.
Nirudi kwenye issue ya deni la taifa.
Nimejiuliza sijapata jibu deni hili linakuzwa na ahughli zipi?
Mfano
SGR inagharimu TR 7
Ndege zimeghatimu tr 2
Rufiji nayo kama Tr7
Haya ndio mambo ninayo yajua kwamba yametumia fedha nyingi.
Zingatia pia hakuna mradi ambao umeisha ukiacha ndege.
Ongezeko la tr 20 kwa miaka minne kuna uwalakini sana yamkini tunalishwa maneno ya uongo wakati hata mishahara inalipwa kwa fedha za mikopo kutokana na matumizi mabaya ya fedha.
Kwa nchi maskini kama hii mtu anapata wapi udhubutu wa yeye na mke wake kutembea na viburungutu vya mil tano tano na kugawa na njugu?
Watanzania tutadanganywa hata lini?
Mwenye uelewa zaidi wapi fedha hizi tr 20 zimika atujuze.