Tanzania Kuna vituKo, Wema Sepetu azua Timbwili

Tanzania Kuna vituKo, Wema Sepetu azua Timbwili

Lugano5

R I P
Joined
Jul 15, 2010
Posts
4,520
Reaction score
757
HOVYOOO! Wema Isaac Sepetu aliye pia Miss Tanzania 2006, amejitoa fahamu kwa kupandisha mzuka na kutinga makao makuu ya Kampuni ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar na kuzua timbwili la aina yake kisa kikiwa ni kuandikwa kwa habari zake na mpenziwe, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz'.
Wema akiwa ndani ya ofisi za Global na sura ya 'kuua mtu', mkononi akiwa na gazeti la Ijumaa Wikienda lenye stori: DIAMOND ATAMANI USHOGA. Kushoto ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.

Tukio hilo la kumchoresha staa huyo mwenye vituko kila kukicha, lilijiri Jumatatu iliyopita kwenye ofisi za Global ambao ni wachapishaji wa gazeti hili (Amani), Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Risasi majira ya mchana kweupe hivyo kufunga mtaa huku wapita njia wakimzodoa kwa maneno ya kejeli.
ATINGA NA WAPAMBE DHAIFU
Akiwa na kundi la wapambe dhaifu na goigoi wakiongozwa na meneja wake, Martin Kadinda waliosimama nje ya ofisi hizo, Wema alifika kwa upole akionekana mkarimu kwa mlinzi ambapo aliomba kuonana na mwandishi nguli wa magazeti pendwa, Imelda Mtema.
Mlinzi alimruhusu kwa vile Global ni mjengo wa mastaa na watu wasio mastaa, huwa hawakauki kuingia na kutoka kwa mambo mbalimbali.
Wema alipofika mapokezi, pia aliomba kuonana na mwandishi huyo lakini tofauti na utaratibu ambapo huwa mgeni akifika huulizwa kama ana ‘apointimenti' ili aitiwe anayemhitaji, Wema alipitiliza kwa nguvu hadi chumba cha habari akifuatana na kijana aliyekuwa akimrekodi.
Wema akiwa ndani ya News Room akimtafuta mwandishi wa Global Imelda Mtema, huku akisema yeye ni chizi!
Akiwa ndani ya chumba cha habari, Wema aliuliza kwa sauti ya juu na ya kujiamini: "Imelda yupo wapi? Nauliza Imelda yupo wapi?"


WEMA NA IMELDA
Katika kumtafuta Imelda kwa macho kwa sababu chumba cha habari ni kikubwa huku akionywa na wahariri kwamba atulize mzuka kisha aeleze shida yake, Wema alimuona Imelda akitoa maelezo kwa Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka kuhusu habari aliyokuwa ameifuatilia.
Cha kushangaza, Wema alimfuata Imelda mpaka kwenye meza ya mhariri huyo kisha kuanza kufoka kwa sauti ya juu.
MSIKIENI WENYEWE
"Kwa nini mnafuatilia maisha yangu? Kila siku mnaniandika na Diamond. Kwa nini Imelda unaniandika kuwa mimi msagaji?"

ATULIZWA, AGOMA
Katika kuhoji huko, mhariri kiongozi alijaribu kumtuliza Wema ambaye alikuwa kama amewehuka: "‘Wema tuelewane, eleza shida yako kwa utaratibu kwani hakuna ofisi isiyokuwa na utaratibu."
Pamoja na kuambiwa hivyo bado Wema aliyekuwa ameshika Gazeti la Ijumaa Wikienda toleo la Jumatatu iliyopita, aliendelea kumng'ang'ania Imelda ambaye alikuwa akijaribu kumtuliza:
"Wema twende tukakae pale kwenye meza ya mkutano uwaeleze viongozi wangu tatizo lako. Hiyo stori kuwa wewe ni msagaji mbona haipo, ni gazeti gani?"
"Hivi mnajua mimi ni chizi? Kwa taarifa yenu mimi ni chizi zaidi ya machizi wote, ohooo!"


MLINZI ATONYWA, ATIA TIMU
Baada ya hali kuwa tete, mlinzi wa geti kuu alipigiwa simu ya mezani na kujulishwa juu ya Wema kusababisha kazi kusimama ambapo alifika haraka tayari kwa kumtoa nje kwa hiyari yake au lazima.

Ndipo kukatokea timbwili kubwa, wapambe wake ‘goigoi' nao waliingia wakitaka kufanya vurugu ili kumteka mwandishi huyo lakini kikosi imara cha Global kikiongozwa na Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally kilijiimarisha na kutuliza fujo hizo huku kikiwa makini kuhakikisha Wema na timu yake hawajeruhiwi hata kidogo.

WEMA ATUMIA GAZETI KAMA SILAHA
Katika purukushani hiyo, Wema alionesha udhaifu wa kumudu varangati pale alipotumia gazeti aliloshika kumpiga nalo mwandishi Imelda, jambo lililodhibitiwa kama Waasi wa M23 wa Kongo walivyodhibitiwa na Majeshi ya Umoja wa Mataifa, akatolewa nje.

MBALI NA WEMA
Ukiachia mbali Wema kutulizwa kwa kutolewa nje kwa nguvu, vijana wake walegevu nao waliwekwa chini ya himaya ya Global kwa kunyang'anywa kamera ya video iliyokuwa ikitumika kuchukua matukio huku nao wakipigwa picha za kutosha na wapiga picha wetu.

VITA KUBWA, WEMA AVUA VIATU
Nje ya ofisi, ‘vita' kubwa kati ya Wema na walinzi wa Global (alifika mwingine kutoka lindo la mbali) ilizuka ambapo staa huyo alivua vile viatu vyake virefu vya rangi ya bluu bahari na kuanza kumpiga navyo mmoja wa walinzi hao akiamini anamkomesha lakini pia akadhibitiwa!Wema akiwa anarandaranda kwenye geti kuu akiwa peku, alidondosha matusi ya nguoni ambayo hayaandikiki gazetini kwa namna yalivyokuwa makali. Ilikuwa si rahisi kuamini kuwa yeye ni kioo cha jamii.
Timbwili la Wema na wapambe wake akiwemo Petit Man, ambao hawakufua dafu kwa walinzi na vijana wa Global nje ya ofisi hizo, lilichukua zaidi ya nusu saa huku likikusanya kadamnasi na kusababisha mtaa kujifunga wenyewe.
POLISI HAO
Hata hivyo, uongozi wa Global uliwasiliana na Polisi wa Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini', Dar ambao walifika na kumkuta Wema na timu yake wakiwa wamepoa mlangoni, wakaambiwa timbwili limetulia hivyo wakatimua zao.

APEWA KAMERA, KADI NOOOO!

Baadaye Wema aliomba kupewa kamera yake ambapo zoezi hilo lilifanyika lakini ‘memori kadi' yenye picha walizoanza kurekodi, ilitolewa ili kupisha maridhiano kwanza. Waliambiwa kadi hiyo ilitolewa kwa sababu walirekodi bila idhini au kibali cha Kampuni ya Global.

WEMA AGOMA KUONDOKA
Baada ya kugundua kadi ya kamera ipo chini ya ulinzi wa Global, Wema alitaka kulianzisha tena akidai hawezi kuondoka hadi apewe kadi hiyo lakini uongozi uliweka ngumu. Baadaye aliondoka kimyakimya. Wakati huo wapambe wake walishaondoka kitambo.

vitendo vya usagaji.

Jameni hata Wabongo fanyeni yenyu mtupunguzie highlight za media. Wanahabari wameweka hema hapa kwetu Kenya maana hatuishi vituko kila siku. Haya hapa kafanya yake malkia wa kibongo huko Dar. CC kadoda11

 
Last edited by a moderator:
Mwandishi: Nakumbuka ulipoondoka nchini kwenda Marekani ulikuwa na mapenzi na Chaz Baba, lakini uliporejea ikasikika kwamba upo na Diamond, nini kilitokea Wema?Wema: (kicheko) yeah! Ni kweli kabisa, baada ya kuachana na Jumbe mwaka 2010 kama nilivyosema ndiyo nilianzana na Chaz Baba, nilimpenda, alinipenda. Na yeye ilikuwa tuoane, lakini nimeshasema nikiwa Marekani nilikuwa nasikia leo Chaz alikuwa na huyu, kesho alikuwa na yule, nikamwambia mimi na wewe basi.

Mwandishi: Kwa Chaz Baba mama yako alimkubali awe mumeo?
Wema: Kusema ukweli hakuwa muwazi kwa Chalz Baba, kwamba anamkubali au hamkubali. Lakini ikawa hivyo, tukaachana.
Mwandishi: Baada ya kuachana na Chalz ukajikuta upo kwa Diamond, nini kilikuvutia kwake?
Wema: Nasibu (Diamond) ilitokea kama nilivyokwishasema. Kwa hiyo mtu unajikuta umezama kwake. Wakati mwingine ni vigumu kusema mtu uliyenaye alikuvutia kitu gani!

KUHUSU KIINGEREZA CHA DIAMOND
Mwandishi: Wema, ni kweli Diamond amejua Kiingereza kwa ajili yako?
Wema: Kwanza niweke sawa hapo. Nasibu si kwamba amejua Kiingereza kwa ajili yangu, bali amejua kuzungumza Kiingereza vizuri. Ina maana tangu awali alikuwa anakijua lakini si kivile.
"Mimi na Nasibu tumekaa pamoja mwaka mzima kama mke na mume baada ya mimi kutoka Marekani mwaka ule 2011. Sasa si unajua mimi kidogo nakijua vizuri. Kwa hiyo kwa miezi kadhaa ya nyuma katika kuishi kwetu alikuwa akipata tabu kidogo.
"Ila nataka kukwambia kwamba, Nasibu ni makini sana. Hakuna mtu makini kama yeye. Akiwa hajui kitu lazima akuulize, hakai kimya."
Mwandishi: Pamoja na sifa zote hizo, lakini mwisho wa siku wewe na Diamond mlimwagana kwa awamu ya kwanza, ilikuwaje?

ALIVYOMFUMANIA JOKATE
Wema: Tuliachana baada ya yeye kunisaliti na Jokate (Mwegelo). Unajua nilimwamini sana na sikuwahi kuwa na shaka naye hata siku moja, nilimwamini kupitiliza nikijua ni wangu na mimi ni wake.
"Lakini nadhani haya mambo ya kumwonesha mtu kwamba unampenda sana ndiyo tatizo. Hasa baadhi ya mwanaume.
"Siku moja nakumbuka nikiwa sina hili wala lile, nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi pale Piccolo, baada salamu akaniambia ‘unajua kama Diamond na Jokate wako hapa na wanapigana mabusu?'
"Nilichanganyikiwa sana, nikachukua teksi, nikaenda.
Kufika, kitu cha kwanza nililiona gari lake likiwa kwenye maegesho. Niliingia ndani, nikawakuta wamewekeana miguu. Niliwasalimia lakini hawakuitika.
"Kwa vile niliona kila kitu niliaga na kuondoka huku nikilia. Usiku Nasibu aliporudi alinikuta napanga nguo kwenye begi niondoke zangu, abaki mwenyewe. Hakutaka kuongea na mimi na mimi sikutaka kuongea naye, tukachuniana. Niliamua kutoondoka lakini mimi na yeye hatukulala kitanda kimoja kwa wiki moja. Alijua naumia lakini hakutaka kuanza.

AMWAGANA NA DIAMOND
"Siku moja isiyokuwa na jina, niliamka nikapanga nguo zangu kwenye begi nikaenda kwa dada yangu, Sinza. Ndiyo ikawa kimoja, nikamwacha yeye aendelee na maisha yake na mimi nikaendelea na maisha yangu. Lakini mimi na Jokate kwa sasa tuko vizuri tu.
Mwandishi: Oke, hiyo ilikuwa awamu ile ya kwanza, si ndiyo?
Wema: Yeah!

VIPI KUHUSU HARTMANN?
Mwandishi: Iliwahi kusemekana kuwa kuna wakati uliangukia kwenye penzi la mjasiriamali anaitwa Hartmann Mbilinyi, ni kweli?
Wema: Yale yalikuwa maneno ya watu. Unajua Hartmann nilikuwa nafanya naye kazi za filamu, wakati ule alikuwa na kampuni yake inaitwa Hartmann Production, watu wakadhani ‘nadate' naye, si kweli bwana.

BAADA YA DIAMOND, NANI ALIFUATA?
Mwandishi: Wema, unaweza kutuambia mwanaume gani alifuatia baada ya wewe kuachana na Diamond akawa na Jokate?fuatilia FOR IT,WEB-HOSTING AND NEWS You are welcome maswa exclusive blogspot.
 
Jameni hata Wabongo fanyeni yenyu mtupunguzie highlight za media. Wanahabari wameweka hema hapa kwetu Kenya maana hatuishi vituko kila siku. Haya hapa kafanya yake malkia wa kibongo huko Dar. CC kadoda11

 
Last edited by a moderator:
:A S 465:......hata kama mnauza kwaajili ya majina yao...basi muwatendeee haki, kila toleo wapo FRONT PEGI....basi ikibidi muwape share ya umiliki........KAMA USUPA STAAA NDIO HIVYO BASI KAAAAAAZI KWELII......:A S 465:
 
Jaman napenda niione hii video,kwa mwenye nayo atuwekee
 
Background ya shigongo ina ufedhuri mwingi ambao binadamu mwenye hofu ya Mungu hakupaswa kuishiriki.
 
Hata youtube ipo (wema azua timbwili global)
 
Back
Top Bottom