souljah meditater
JF-Expert Member
- Oct 15, 2012
- 2,146
- 2,098
Kwa mara nyingine tena Tanzania kwenda kushiriki kwenye mashindano makubwa ya michezo mbalimbali duniani ambayo mwaka huu 2016 Summer Olympics itafanyika huko Rio de Janeiro nchini Brazil, kuanzia tar 5 mpaka 21 August 2016.
Tanzania itawapeleka washiriki saba tu ambao watashindana katika riadha, Judo na Kuogelea, tofauti na nchi nyingine zilizoonekana kujiandaa na mashindano hayo zimepeleka zaidi ya washiriki 300 hadi 500 ambao watashindana michezo mbalimbali ambayo inatambulika duniani.
Ikumbukwe kupeleka washiriki wengi ni kujiongezea nafasi ya kushinda medali mbalimbali, katika hafla ya kuwaaga wachezaji SERIKALI imeitaka timu ya Tanzania itakayoshiriki Michezo ya 31 ya Olimpiki kuhakikisha inarejea na medali kutoka katika michezo hiyo nchini Brazil.
Michezo hiyo itaanza Ijumaa ya wiki hii hadi Agosti 21 ambapo timu hiyo yenye wachezaji wa riadha (4), kuogelea (2) na judo (1), iliagwa jana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura kwenye Uwanja wa Taifa. Wambura katika hafla hiyo alisema kuwa anatambua changamoto walizopitia wanamichezo hao wakati wa maandalizi ya kushiriki michezo hiyo mikubwa inayoshirikisha zaidi ya mchezo mmoja duniani.
Kwa upande wangu bado naona tunahitaji maandalizi ya muda mrefu ili kuwa na washiriki wa kutosha na walioiva ili kwenda kuliwakilisha taifa katika michezo mingi zaidi ya hii mitatu iliyoenda kushindaniwa mwaka huu.