Tanzania kupeleka washiriki 7 tu kwenye mashindano ya Olympics 2016

souljah meditater

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2012
Posts
2,146
Reaction score
2,098
Kwa mara nyingine tena Tanzania kwenda kushiriki kwenye mashindano makubwa ya michezo mbalimbali duniani ambayo mwaka huu 2016 Summer Olympics itafanyika huko Rio de Janeiro nchini Brazil, kuanzia tar 5 mpaka 21 August 2016.

Tanzania itawapeleka washiriki saba tu ambao watashindana katika riadha, Judo na Kuogelea, tofauti na nchi nyingine zilizoonekana kujiandaa na mashindano hayo zimepeleka zaidi ya washiriki 300 hadi 500 ambao watashindana michezo mbalimbali ambayo inatambulika duniani.

Ikumbukwe kupeleka washiriki wengi ni kujiongezea nafasi ya kushinda medali mbalimbali, katika hafla ya kuwaaga wachezaji SERIKALI imeitaka timu ya Tanzania itakayoshiriki Michezo ya 31 ya Olimpiki kuhakikisha inarejea na medali kutoka katika michezo hiyo nchini Brazil.

Michezo hiyo itaanza Ijumaa ya wiki hii hadi Agosti 21 ambapo timu hiyo yenye wachezaji wa riadha (4), kuogelea (2) na judo (1), iliagwa jana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura kwenye Uwanja wa Taifa. Wambura katika hafla hiyo alisema kuwa anatambua changamoto walizopitia wanamichezo hao wakati wa maandalizi ya kushiriki michezo hiyo mikubwa inayoshirikisha zaidi ya mchezo mmoja duniani.

Kwa upande wangu bado naona tunahitaji maandalizi ya muda mrefu ili kuwa na washiriki wa kutosha na walioiva ili kwenda kuliwakilisha taifa katika michezo mingi zaidi ya hii mitatu iliyoenda kushindaniwa mwaka huu.
 
Na viongozi wangapi?
Kuhusu viongozi bado sijapata idadi yao kamili ila nawasiwasi wanaweza kuwazidi hata wachezaji wenyewe... Kwa upande wa makocha watakaoongozana na timu hizo ni Francis John (riadha), Alexander Mwaipasi (kuogelea) na Zaid Hamisi (judo) wakati daktari wa timu ni Nassoro Matuzya.
 
Ukweli ni mchungu,lakini Tanzania haijawahi shinda medal ya Gold,katika Olympic games- hii ni aibu kubwa-tuna so called majina makubwa katika michezo but they all went missing when it came to the biggest stage of all
 
Ukweli ni mchungu,lakini Tanzania haijawahi shinda medal ya Gold,katika Olympic games- hii ni aibu kubwa-tuna so called majina makubwa katika michezo but they all went missing when it came to the biggest stage of all
sure mkuu bado tuna kazi kubwa ya kukuza washiriki watakaoweza kushinda Gold
 
Ni mkoa wa singida pekee kati ya hao wanariadha uliotoa wanariadha watatu.Lakini ja ajabu kambi yao huwa ni kilimanjaro.
 
Hao wa Ethiopia mnawaona ni jamii ya warimi(wanyaturu) ambao wapo hata hapo Kenya.Tz singida haina uwekezaji wowote wa riadha wakati ndio yenye wanariadha.Tutasindikiza sana tu!
 
Nimemsikia Mpoki kwenye redio sasa hivi anasema kaona timu ya Olimpiki ya Tanzania inasafiri washiriki wake wote wanaonekana wana majonzi. Anasema haya mambo ya kuwapeleka watu kwenda kuogelea Brazil huku hawajaacha hela ya Kula nyumbani wanaweza kuzama kwa ajili ya mawazo...
 
Hao wa Ethiopia mnawaona ni jamii ya warimi(wanyaturu) ambao wapo hata hapo Kenya.Tz singida haina uwekezaji wowote wa riadha wakati ndio yenye wanariadha.Tutasindikiza sana tu!
Duh kumbe wanyaturu wamesambaa hivyo... tatizo tz hatutengenezi mazingira ya ushindani ndo maana tunaishia kusindikiza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…