Tanzania kupitia shirika la TTCL yaingia mkataba wa kupeleka intaneti Burundi

Tanzania kupitia shirika la TTCL yaingia mkataba wa kupeleka intaneti Burundi

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Dar es Salaam. Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesaini mkataba na kampuni ya mawasiliano ya mkongo wa Taifa ya Burundi (BBS) kwa ajili ya kupeleka huduma ya intaneti nchini humo. Mkataba huo wa Sh13.8 bilioni utatekelezwa katika nchi ya Burundi kwa kipindi cha miaka 10.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo Jumanne Oktoba 22, 2019 nchini Tanzania na mtendaji mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba na ofisa mtendaji mkuu wa BBS, Elie Ntihagowumwe.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Kindamba amesema TTCL itatoa mawasiliano ya uhakika katika nchi hiyo.

Amebainisha kuwa kupitia mkataba huo Serikali imeongeza mapato na wigo wa biashara katika nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc).

"TTCL itatoa huduma ya mawasiliano ya mkongo wa Taifa nchini Burundi kupitia vituo vyetu vya mpakani katika miji ya Kabanga na Manyovu na kuiunganisha nchi hiyo na dunia kupitia mikongo mikubwa ya baharini.”

“Makubaliano haya yametanua wigo wa kutoa huduma na tunategemea kuongeza huduma kutoka 2.5 GBPS ya sasa mpaka kuwa 10GPS,” amesema Kindamba.
Kindamba ameainisha huduma za mawasiliano zitakazotolewa na TTCL kupitia makubaliano hayo kuwa ni data na intaneti.

Nyingine ni utunzaji wa kumbukumbu mbadala kupitia kituo cha kimataifa cha kutunza kumbukumbu kilichopo nchini, kubadilishana wataalamu na wahandisi, kuwajengea uwezo wa kitaalamu katika nyanja za mawasiliano.

" Pia tutabadilishana wateja wakubwa wenye matawi na ofisi za biashara mfano benki ya CRDB, kupeana ushauri wa kitaalamu kuhusu watoa huduma na watengenezaji wakubwa wa vifaa vya mawasiliano vinavyotumika katika mawasiliano,” amefafanua.

Mpaka sasa TTCL imewafikia wateja zaidi ya milioni 2 huku wanaotumia huduma ya T Pesa wakifikia 600,000 nchi nzima.

"Pia tuna mawakala 19,000 nchi nzima na miamala ya takribani Sh5 bilioni imeshatolewa,” amesema.

Naye Ntihagomumwe amesema huduma hiyo itawanufaisha wananchi kwa kuwawezesha kutekeleza vizuri shughuli zao zinazohusu Tehama.

" Mbali na wananchi wa Burundi kunufaika na huduma hii, pia BBS itajifunza vitu vingi kutoka TTCL,” amesema.

===
Chanzo: Mwananchi
 
Wawape vijana wao vifaa vya kusajilia kwa fingerprin,mitandao yote vijana wao wanavyo vifaa vya kusajilia kwa fingerprint
 
Kwani majizi chadema wanateseka na hili?

Mzee wa tutashiatakiwa MIGA je anasemaje?
 
Hapa nyumbani walishafunikwa, ngoja wajaribu burundi
 
Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Tanzania TTCL imesaini makubaliano na kampuni ya BBS ya Burundi kuhusu kutoa huduma za mtandao wa Internet.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya TTCL Bw. Waziri Kindamba amesema, Makubaliano hayo yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 6 yatatekelezwa nchini Burundi kwa miaka 10 ijayo.

Amesema TTCL itatoa huduma za ngazi ya juu kwa Burundi kwa kupitia vituo vyake vya Kabanga na Manyovu, Mkoa wa Kigoma.

Bw. Kindamba amesema utoaji wa huduma za Internet utarahisisha na kuboresha biashara kati ya nchi hizo mbili.
 
Back
Top Bottom