Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,112
- 34,951
Juhudi gani hizo? kulinda mgongo auJuhudi za BICHWA KOMWE zimeanza kuzaa matunda sasa.
Itabandikwa picha za naniAidha, makubaliano hayo yanahusisha Urusi kuisaidia Tanzania katika kuanzisha shirika lake la kitaifa la anga (National Space Agency), kujenga uwezo wa wataalamu na kuendeleza miundombinu ya kupokea taarifa kutoka angani.
Hii ni hatua muhimu katika safari ya Tanzania kuelekea kujenga uwezo wake katika teknolojia ya anga za juu.
WapigajiSasa satelite za nini wakati kwa sasa ziko zaidi ya 10000 duniani zinaizunguka dunia na kutupatia taarifa mbalimbali za dunia.
Yametushinda na uku chini kama barabara nzuri, shule nzuri na zenye vifaa, hospitali bora na zenye vifaa, maji na umeme bado ni changamoto. Tutaweza hayo ya uko juu na hizi siasa mbovu kwenye hii nchi. Naona ni siasa kama zingine. Embu Tupe na link tuone woteView attachment 3703131
TANZANIA KURUSHA SATELAITI YAO MWAKA 2027
Tanzania huenda ikaingia katika hatua mpya ya maendeleo ya teknolojia ya anga kwa kushirikiana na Urusi kupitia shirika lake la anga la Roscosmos, katika mpango unaohusisha uwezekano wa kurusha satelaiti ya kwanza ya Tanzania kwa kutumia roketi za Urusi.
Hatua hiyo inalenga kuongeza uwezo wa Tanzania katika matumizi ya teknolojia ya satelaiti, mawasiliano, ufuatiliaji wa mazingira na ukusanyaji wa taarifa za kisayansi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Roscosmos, uzinduzi huo umepangwa kufanyika mwezi Machi 2027, na utakuwa wa satelaiti ya uchunguzi wa Dunia (Earth Observation Satellite).
Satelaiti hiyo inatarajiwa kusaidia katika ufuatiliaji wa mabadiliko ya tabianchi, kilimo, misitu, rasilimali za maji na ramani za maeneo mbalimbali.
Aidha, makubaliano hayo yanahusisha Urusi kuisaidia Tanzania katika kuanzisha shirika lake la kitaifa la anga (National Space Agency), kujenga uwezo wa wataalamu na kuendeleza miundombinu ya kupokea taarifa kutoka angani.
Hii ni hatua muhimu katika safari ya Tanzania kuelekea kujenga uwezo wake katika teknolojia ya anga za juu.
Dennis Robert ShughuruZote hizo ni juhudi zilizofanywa na rais wa Jf Denis kisaye Robert Shughuru
Jina lilikuwa haliji mkuu ahsante
Hatari sana sana! π€£πππ π€Juhudi za BICHWA KOMWE zimeanza kuzaa matunda sasa.
Ww ni lijinga tena sana kurusha setelite ata ww unaweza kurusha maana ni pesa tu na kuna makampuni kibao yanayo fanya kaz ya kurusha setelite iyo uloweka kwa picha ni rocket inayo tumika kurusha setelite
Kila nchi au kila mtu anaweza kurusha setelite sabu ni uduma inalipiwa ila sio kila nchi inaweza kumiliki rocket kwajiri kurishia setelite au kupeleka watu mwezini