Tanzania kusafirisha Dizeli kwa bomba kwenda Zambia

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mawaziri wa nishati wa Tanzania na Zambia, wamekubaliana taratibu za namna ya kuimarisha ulinzi katika bomba la TAZAMA litakalosafirisha mafuta ya dizeli kutoka nchini kwenda katika Taifa hilo jirani.

Miongoni mwa masuala hayo ni kuongeza askari katika njia ambazo bomba hilo linapita, kuhamasisha wananchi kuwa walinzi namba moja na kutumia teknolojia ikiwemo ndege zisizo na rubani (drones).

Hayo yamelezwa leo Jumanne Disemba 6, 2022 na Waziri wa Nishati, January Makamba katika kikao cha siku mbili cha pamoja kati ya mawaziri na makatibu wa nchi hizo mbili kilichojadili namna ya kuimarisha ulinzi katika bomba la Tazama.​
 
Zambia ndio wanasafirisha mafuta yao kupitia bomba hilo linaloanzia bandari salama TZ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…