Tanzania kutoshiriki Miaka 50 AFCON

Tanzania kutoshiriki Miaka 50 AFCON

python1

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Posts
307
Reaction score
186
Ndio hatuta shiriki tena Miaka 50 ijayo.Ngoya tusubiri tuone wabunge walienda kufanya nn misri.Hapo ndo tutajua ,Hiii nchi tunasafari ndefu sana.

Sijapata kucheza mpira katika ngazi ya ligi kuu ila nimecheza mpira katika academy (FOYSA) Pale Mbeya na ngaz ya wilaya so idea ya mpira ipo.

Swali jepesi UMISETA NA UMITASHUNTA lengo lake nn katika dira ya michezo ya Tanzania ,ok! Kuibua vipaji then vikisha ibuliwa vipaji vinaenda wapi???zaidi zaidi ya kusifika mtaani , mashuleni na wilayani kuwa Fulani anajua mpira au anajua kukimbia.
watoto waishio mazingira magumu walichukua kombe la Dunia wako wapi,??? Serengeti ya Miaka ile iliyosumbua kule brazili ipo wapi ??

Samahani kwa nitakao wakwaza Sina sehemu ya kutolea pove zaidi ya Jamii Forums ambako hata sisi maskini ambao kwenye vikao vya Familia hatuulizwi tunakunywa soda gani tunaletewa mirinda nyeusi tunapata fursa ya kuwasilisha maono yetu.

Kiukweli bila kubadilisha mifumo yetu na kuachana na mipira ya kwenye kahawa kiukweli tutaendela kuwa kichwa cha mwenda wa zimu.

Eti watu wamekaa kwenye vijiwe vya kahawa "LEO SENEGAL ANAKUFA TATU Niongeze kikombe kingine"

Eti AFCON tunaenda kufanya maajabu,tunafika robo.

Hivi mnajua SENEGAL wamewekeza kiasi Gani toka walivyopotea kwenye kile kizaz Cha wakina DIOF, halaf mnataka tuwafunge, kweli??
Wakati nasoma advance Kuna jamaa yeye alikuwa Hasomi kitabu kingine zaidi ya review zile za Necta na kukalili majibu na alikuwa anafaulu kuliko sisi ambao tulikuwa tunakomaa kuelewa kwenye CHAND na NELCON,"msuli kikombe matokeo jaba" matokeo yake ndo hawa viongozi ambao hawa amini katika kuweka Sera bora na kuweka mipango iliyo sahihi ilikufikia malengo.

kwa wanaojua mpira wanaweza kuelewa nn nazungumzia .

Ni ukweli usiofichika ya kwamba Mambo mengi yanakwama katika nchi yetu kutokana
1.kuchanganya siasa na utendaji
2.ukosefu wa uzalendo
3.Rushwa na ufisadi
4.mipango na Sera mbovu
5.Elimu ya kikoloni

Kuna umuhimu wa kustructure elimu yetu kulingana na mahitaji ya kileo, elimu yetu bado imekaa kikoloni inamuanda mtu kuwa mtumwa tu.

Mfano:
Tukachagua Shule tano hizi hizi tulizo nazo
Mwanza ambayo itakocollect vibaji kutoka Kanda ya ziwa ,Arusha itacollect kaskazini ,mbeya ambayo itacollect kusini magharibi,mtwara ambayo itacollect kusini mashariki then Dodoma Kanda ya Kati na ambayo itakuwa na vibaji Bora zaidi .vipaji vikioneka kwenye mashindano Kama UMISETA na UMITASHUNTA vipelekwe huko kwenye hizo shule . Na hizi shule naaamini baada ya Miaka 15 zitakuwa na uwezo wa kujiendesha na zitaweza kufanya vijana wengi wakajiajiri katika michezo, anaweza asicheze Simba au Barcelona but akawa mwalimu mzuri wa michezo kwa kizazi kijacho.

Hiyo ni video ya academi ndogo sana ya Senegal

Raisi wangu mtukufu usiwape pesa hao tena za kwenda kuwekea kambia ulaya hamna kitu wanatia hasara tu hao the way ulivyo amua kulivalia njuga suala la mafisadi na ujenzi wa miundo mbinu ndivyo tunaomba utusaidie upande wa michezo ,tulasmishie shule ziwe kwa ajili ya michezo ,tutengenezee miundombinu tutafutie walimu naamini utatengeneza ajira zaidi ya 50000 ifikapo mwaka 2035
 
Mkuu shukrani kwa mawazo chanya.

Naunga mkono hoja
 
Kwanza ile mechi ya na Uganda tulibebwa ambayo ni rushwa kwenye mpira kwa Ug kucheza maksudi chini ya kiwango, Inabidi tupigwe Ban kama miaka 50 hivi
 
Waruhusu watu binafsi wanaotaka kuwekeza kwenye michezo wapatiwe ardhi na Vivaldi. Mfano mtu anaejenga tennis courts na kufundisha junior Team Jumamosi na wakubwa wanaopenda wafundishwe jioni.
 
Wazo zuri, tatizo wa kuyafanyia kazi haya mawazo ndo hawana mpango wowote
 
Mnaumiza vichwa bure, serikali ya ccm haijawahi kuwa na nia ya kuendeleza michezo ndyo maana walifuta michezo mashulen japo wameirudisha kiunafiki . Wamehodhi viwanja vya michezo na kuvigeuza vyao huku vikiwa vimegeuka magofu . Chuo pekee cha michezo cha mallya kina hali mbaya kimiundombinu serikali ya ccm wala haijali.
Juzi kati hpa tff wameandaa mashindano ya u 17 ya africa kwa hali ya kawaida ungetegemea serikali itoe sapoti ya kutosha kwenye maandalizi ya timu yetu mwisho wa siku tff wameandaa proposal ya kuipeleka timu ya vijana sweden serikal ikagoma kutoa hela
Timu ikawa km ya watoto yatima wakaishia kupelekwa arusha na kucheza na timu za daraja la pili.

Hii ndyo hali halisi ya ccm linapokuja suala la michezo ni wanafiki hatari
 
Kwanza ile mechi ya na Uganda tulibebwa ambayo ni rushwa kwenye mpira kwa Ug kucheza maksudi chini ya kiwango, Inabidi tupigwe Ban kama miaka 50 hivi
Tukishinda mnasema tumebebwa na tukifungwa mnatukejeli na kutuponda ila hamtaweza kutukwamisha. Kila laheri Star's.
 
.....huko afcon hatupawez
Tunapaweza mkuu ndio maana tulifanikiwa kufuzu na kuhusu kufungwa hio ni kawaida kwenye mashindano ya soka ili mshindi apatikane lazima wa kufungwa awepo hata kombe la dunia kuna kufungwa pia.
 
Back
Top Bottom