NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,587
- 13,425
Hongera mtani! Hongera mtani kwa kutwaa/kutimiza ndoto yako uliyokuwa ukiiota kwa muda mrefu kwamba "Utamfunga mtani (Yanga), ingenishangaza endapo Simba ingedondosha point 3 mbele ya Yanga, sijui furaha ya mashabiki ingetoka wapi.
Twende kwenye point tajwa hapo juu kama kichwa cha habari kinavyojieleza, NALIA NGWENA nimejikita kuandika maoni yangu haya kama mdau wa mpira baada ya kuona wachezaji wa kigeni wakiimbwa sana kwenye redio, magazeti na social media lakini wachezaji wetu wa ndani ya taifa wanapofanya vizuri husikii miluzi ya kuwapa sifa.
Mchezo wa derby ya kariakoo nani hakuona kazi ya kiungo punda Mzamiru? Nani hakuona kazi ya winga yenye nguvu na kasi Kibu Denis? Nani hakuona kazi ya kijana Mzanzibari Yahya Mudathiri?
Hakika vijana wetu wanastahili sifa kama wanazopewa akina Mayele, Baleke Chama nk. Hakika sipati picha Mayele au Baleke wangefunga, magazeti na wachambuzi wangeimba na kusifu kama walokole wanavyomsifu Mungu aliyejuu, social media zote kila mtu angesifu kwa fijo na nderemo utadhani kimetokea nini.
My take; wachezaji wetu wazawa nao wapewe sifa kama tunavyowasifu na kuwapamba hao akina Sakho na akina Azizi Ki, hakika italeta hamasa kubwa sana kwa vijana wetu katika kupambania namba zao.