Tanzania kuwa kama Uganda!

Tanzania kuwa kama Uganda!

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Museveni anatawala UG tangia 1986, ameweza hilo ingawaje anatoka kundi dogo ambalo ni minority Uganda, sababu kubwa ni kwamba ana Jeshi, anamiliki Jeshi kama ukipenda na ndio maana anaongoza majority hata kama hawamkubali hakuna kitu watafanya sababu hawana Jeshi, uchaguzi ni zoezi tu lkn hauamui chochote.

Mkoloni alitumia mbinu hiyo hiyo kutawala wengi ingawaje Wazungu walikuwa wachache, lkn Mzungu alimiliki Jeshi, na mwenye Jeshi anaongoza wote.

Hivyo mwenye Jeshi atatawala milele waliowengi hata kama hawataki hakuna kitu watafanya, ndiyo maana jeuri na kiburi kila mahali, hakuna anayetaka kusikiliza shida za watu, mkilalamika mnajibiwa hameni nchi, ni kwa sababu ya power, imeshatoka hiyo, Tanzania ishaenda tena, haitarudi tena, bye bye, …
 
Back
Top Bottom