kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Tanzania ina kila aina ya utajiri. Katika ardhi yake kuna madini ya dhahabu, Tanzanite, makaa ya mawe, gesi, na sasa watafiti wamebaini kuna madini mengi ya urani.
Madini ya urani yanatajwa kupatikana kwa wingi kwenye Mkoa wa Dodoma na Ruvuma wilayani Namtumbo ambako madinihayo yanatarajiwa kuchimbwa hivi karibuni.
Kazi ya kutafiti kuwapo kwa madini ya urani imekamilika chini ya Mradi wa Mkuju River wilayani Namtumbo na wataalamu wamesema pia wataendelea na utafiti.
Kilometa 54 kufika mgodini
Madini hayo yanapatika wilayani Namtumbo ikiwa ni kilometa 54 kutoka Kijiji Cha Likuyu Sekamaganga ambako ni makazi yawananchi mpaka kufika kwenye eneo ambako madini hayo yamegundulika.
Madini hayo yamegundulika kwenye Pori la Akiba la Selous ambalo linajumuisha zaidi ya mikoa mitano.
Baada ya shughuli za uchimbaji wa madini ya urani kuanza, kutaifanya Tanzania kuwa nchi ya tatu barani Afrika kwa uzalishaji wa madini baada ya Niger na Namibia.
Kwa mujibu wa Mwanajiolojia Mwandamizi wa mradi huo James Magweiga mgodi huo una akiba ya tani 54,000 za madini hayo ya urani.
Madini yaliyopo sasa yatadumu kwa kipindi cha miaka 12 ijayo baada ya kuanza shughuli za uchimbaji, ingawa utafiti bado unaendelea ili kupata madini mengizaidi, anasema mtaalam huyo.
Mradi huo unaomilikiwa na Kampuni ya Mantra Tanzania na kuendeshwa na Kampuni ya Uranium One Inc unatarajiwa kuvutia Uwekezaji wa Kigeni (FDI) unaofikia Sh1.6 trilioni (sawa na dola 1 bilioni za Marekani).
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Uranium One Chris Sattler anasema utendaji kazi katika uchimbaji huo utazingatia viwango vya Kimataifa vilivyowekwa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki sambamba na sheria na taratibu za nchi na kikanda.
Kama ilivyo kwa miradi mingine ya Urani duniani, mradi huu wa Mkuju utazingatia taratibu zote za kiusalama za Kitaifa na Kimataifa, anasema Sattler.
Pia Kama malengo yote yatatimizwa kama yalivyopangwa na uthibitisho unaotakiwa utapatikana haraka kutoka mamlaka inayohusika serikalini, basi ujenzi wa mradi utaanza katikakipindi kijacho cha kiangazi na utakamilika baada ya miaka miwili ijayo.
Anabainisha kwamba kabla ya ujenzi huo kuanza katika kipindi cha miezi tisa, wahandisi na wabunifu watakuwa wamekamilisha program zao.
Mkurugenzi huyo wa Mantra anasema kuwa bado kuna mambo mawili yamebaki kutoka serikalini kabla ya kuanza kwa ujenzi huo.
Anasema mwaka uliopita Serikali yaTanzania ilipitia mwongozo wa kamati inayohusu masuala ya urithi wa dunia kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni(Unesco) kwa ajili ya kupunguza mpaka wa eneo la Hifadhi ya Taifa ya Selous ambayoni moja ya maeneo ya urithi wa dunia.
Mwaka huu serikali imeipa Mantra leseni maalum ya uchimbaji madini, sasa tunaangalia namna ya kusaini Mkataba wa Maendeleo ya Madini (MDA) na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini baada ya hapo tunatarajia kupata taratibu zinazotakiwa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, anasema.
Sattler anasema madini ya urani yatakayochimbwa yatatumika kuzalisha umeme. Madini ya Urani yanatumika tu kuzalisha nishati ya nyuklia katika nchi ambazo zimesaini mkataba wa kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia(IAEA), anabainisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Matra, Asa Mwaipopo anasema kwamba watu 1,600 wanatarajiwa kuajiriwa wakati wa ujenzi wa mradi huo na katika hao, 750 watapewa ajira za kudumu.
Mwaipopo anafafanua hivi sasa kuna waajiriwa 120 kwenye mradi huo ambao wanaendelea na tafiti mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Abdula Lutavi anasema wananchi wilayani humo na wilaya za jirani wana matumaini makubwa ya kukuza fursa za kibiashara ambazo zitawaletea maendeleo.
Watu wana mtazamo chanya kuhusu mradi huu japokuwa wanafikiria kuwa utachukua muda mrefu kuanza, fursa nyingi zinatarajiwa kuwa wazi anasema Lutavi.
Wilaya ya Namtumbo ina watu 201,000 ambao wanategemea kilimo kama njia pekee ya kiuchumi huku tumbaku ikiwa ni zao pekee linalotegemewa kuwapatia kipato.
Siku za hivi karibuni Waziri Mkuu Mizengo Pinda alizindua machinjio ya kisasa ambayo mkuu huyo wa wilaya anasema yatatumika kusambaza nyama kwenye mgodi huo.
Licha ya kuwa machinjio haya ni ya kisasa, lakini bado hajafikia lengo na tunatarajia kwamba kiwango cha kuuza nyama kitapanda baada ya mgodi kufunguliwa, anasema Lutavi.
Wananchi Namtumbo
Kutokana na kuwapo kwa fursa hiyomaofisa kilimo wa wilaya hiyo wanawafunda wanavijiji kuhusu kilimo cha mbogamboga na ufugaji wa kuku ili wawauzie wafanyakazi wa mgodi huo.
Tunataka watu wetu wanufaike namradi huu na hili litafanikiwa kwa kuwawezesha kuuza bidhaa zao mgodini, anasema mkuu huyo wa wilaya.
Mbali na hayo Mantra ina uhusiano mzuri na wananchi na imekuwa ikiwapatia huduma za kijamii kama elimu, afya na uhifadhi wa mazingira.
Meneja wa Usalama wa Afya, mazingira na ubora Cornelius van den Berg wa kampuni hiyo kwa kushirikiana na serikali wamezindua mpango wa kudhibiti ujangili katika eneo hilo la hifadhi.
Mpango huo unasaidia kutoa fedha na mafunzo kwa askari wa hifadhi wapatao 20 na kuwapatia magari na nyenzo nyingine.
Kampuni ya Mantra Tanzania Ltd ndiyo inayomiliki mgodi huo ikiwa ni mshirika wa kampuni ya Urani ya Urusi (ARMZ) wakati Uranium One ndiyo waendeshaji wa mgodi huo.
© 2013 MCL