hivi cash economy tz itaisha lini jamani? mtu anaenda dukani na milioni tano, milioni kumi anaenda kufanya shoping na mihela kwenye begi! kwanini tz tusiweke mipaka, mfano: kuanzia manunuzi ya laki tano kwenda juu malipo yafanyike electronically, sheria itungwe na hapo ndipo hata kodi itakatwa vizuri bila kukwepa (pamoja na kwamba hata ufanyeje wabongo hupenda uchochoro na shortcuts na udanganyifu). SHERIA itungwe jamani!