SoC04 Tanzania kwenye G20 2050

SoC04 Tanzania kwenye G20 2050

Tanzania Tuitakayo competition threads

sultan kihamba

New Member
Joined
Dec 28, 2018
Posts
1
Reaction score
0
Tunahusiana jamii ya watanzania wenye bahati ya vitu vingi ikiwa ni pamoja na kuwa na hamu ya serikali zenye usikivu hawamu zake zote, Kuna sehemu tumekosea tokea Uhuru hasa katika swala la kuwa na mahamuzi ya haraka kwenye fursa tulizo nazo. Hatuna tena sababu ya kusingizia ukoloni kama sababu ya kukwama kiuchumi, tuko na miaka zaidi ya 60 ya Uhuru sawa na taifa la China lenye miaka 68+ tunatamani kuharakisha mipango ya kimaendeleo ili ifikapo mwaka 2050 tuwe taifa shindani kiuchumi duniani na ikiwezekana Africa tuwe kwenye nafasi tano za juu. Kufikia hayo lazima sababu za makisudi zichukuliwe kwenye mambo ya fuatayo;

1. Elimu yenye manufaa,, tunaitaka Tanzania yenye vijana shindani katika soko la ndunia wasiyo tembea na bahasha za kakti mitaani. Hatutaki tena wimbi la wahitimu wasiyo na maarifa, vyuo vya VETA vipewe nguvu zaidi ili kuzalisha watu huru kifikra.

Tunataka kuzalisha vijana wabunifu, wenye uwezo wa kupamabana na hali za mazingira yanayotuzinguka. Wingi wa vijana wenye elimu na maarifa itaipa taifa faida katika nyanja nyingi.
Serikali itenge maeneo ya kimikakati katika kila ukanda ili hayo maeneo yatumike kukuza sehemu nyingine mfano kasikazini ukanda wa kitalii, ukanda wa kusini nyanda za juu na ukanda wa ziwa uwe ukanda kilimo na mifugo, na viwanda ukanda wa kati na mashariki kwamaana ya pwani ya bahari ya Hindi uwe ukanda wa viwanda na biashara.

3. Kutunza amani na kuidumisha, hii inamaana kuwa shughuli zote za kijamii na kiuchumi zinategemea sana Hali ya utulivu wa nchi. Nchi nyingi zenye maendeleo makubwa zimejidhatiti katika swala la amini usalama ili kuvutia wawekezaji na kuhakikisha usalama wa mali na kurahisisha utendaji kazi. Kwa amani ambayo bado tunayo kama tunu yetu bado hatujaitendea haki miaka 60 ya uhuru.

4. Serikali kuongeza wingo mpana kupitia taasisi zote husika katika maswala ya kidigitali na utandawazi ili kwenda haraka sana sawa na kasi ya ulimwengu na watu wake, iweke mifumo rasimi kwa watu wake na sheria za makusudi na wezeshi kwa raia. Taifa linaipokeaji taarifa ya crypto currency na mifumo yote ya kidigitali, tuangalie mifano kwa mataifa kama Singapore nasisi tujifunze.

5. Sekta ya kilimo inaweza kutusaidia kuajili vijana wengi sana hata ikiwezekana taifa zima kwasababu idadi kubwa ya watanzania tunatokana na jamii ya wakulima, kwahiyo kilimo nikitu kinachoweza kueleweka haraka na kufikia kila mtanzania kwa haraka. Mikopo teknolojia na utashi wa serikali uelekezwe kwenye sekta hii kwa nguvu zaidi ili kupunguza wimbi la vijana wasiyo na kazi. Kilimo imekuwa kazi ya wazazi wetu kwa miaka mingi kwasababu haivutii na haina hamasa kwa vijana serikali inaliendea swala hili kwa kasi yakawaida huku tukiwa tunajichelewesha wenyewe. Tuitaka Tanzania yenye vijana wenye uhuru kiuchumi.

6. Kwa hatua za kwanza kabisa wahitimu wote wanao hitimu waruhusiwe kukopa mabenki kwa dhamana ya mzazi au mlezi au vyeti vyake vya shule ili kuhakikisha kila kijana akimaliza asiwaze kukimbilia kuajiliwa. Tukisha kuwa na wazalishaji wengi katika jamii yetu tutapata walipa kondi wengi na kulipa Kodi nchi itakaimalika kiuchumi na hii itasaidia kupunguza mikopo ya mashariti magumu.
Watanzania inabidi tuendelee kuwa na ufahamu wa kulipa Kodi kwa hiali na kwa uaminifu na serikali isaidie zaidi kuongeza vyanzo vingine vya mapato iache kutegemea sana Kodi tu mfano kuongeza vyanzo vya ufuaji umeme kwa makaa ya mawe na nuclear power, ili tuuze nchi jirani, ili tupunguze bei ya umeme kwa wananchi, itasaidia kupunguza matumizi ya mikaa na kuni.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom