Tanzania, Malawi na Msumbiji waingia makubaliano mto Ruvuma

Tanzania, Malawi na Msumbiji waingia makubaliano mto Ruvuma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso waziri mwenyeji wa umoja wa nchi tatu zinazonufaika na Mto Ruvuma Tanzania, Malawi na Mozambique ameongeza Mkutano na Hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano ya Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za maji za Mto Ruvuma kwa nchi za Tanzania, Malawi na Msumbiji.
IMG-20240731-WA0010.jpg

Mkutano huu umehudhuriwa na Waheshimiwa wa Maji wa nchi hizi tatu Waziri wa Maji Tanzania Mhe Jumaa Aweso mwenyeji, Mhe Abida Sidik Mia Waziri wa Maji Malawi, na Mhe Carlos Mesquita Waziri wa Maji Msumbiji Leo tarehe 31 Julai 2024 Four Points by Sheraton Hotel Dar Es Salaam Tanzania.

Wakizungumza katika nyakati tofauti Mawaziri wa Maji wa nchi hizi tatu wamesema usimamizi na uendelezaji wa Rasilimali za Maji hususani mto Ruvuma ni kipaumbele cha viongozi wakuu wa nchi zao.
IMG-20240731-WA0009(1).jpg

Aidha Waziri Aweso akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano amesema amewasilisha salam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambae katika nyakati tofauti amesisitiza na kuhamasisha mashirikiano mema katika utunzaji na uendelezaji wa Rasilimali za Maji.
 
nchi ya hivyo hiii !! yaan ukienda mwanza kuna maeneo maji ya shida na ziwa lipo mlangoni afu bado wanahangaika na mto utafikiri maji yameisha
 
Hatujajibana sisi wenyewe kwenye huo mkataba?

Maana kuingia mkataba mzito kama huu huku ukiwa na aina ya wanasheria waliotuingiza ktk mkataba wa bandari inabidi ustuke kidogo
 
kwenye picha Mchina haonekani, btw chinese military imetia timu on tanzagizas soil, wakati enzi za ukoloni miaka 100 iliyopita Wajerumani na Waingereza walitandikana tukaingizwa kwenye vita isiyotuhusu ndoo maana askari monument likajengwa mt. Samora kukumbuka tulivyokufa kwenye vita isiyotuhusu, leo more than 100 years later USA military kaingia Kenya mpinzani wake China military naye kaingia TZ kucounter US influence in EA, some things never change …
 
Back
Top Bottom