Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,887
- Thread starter
-
- #21
Maeneo Mengine ya Kukuza Uchumi na Ujenzi wa Msingi wa Uchumi wa Viwanda
4.6.1 Viwanda
4.6.1 Viwanda
- Kupanua na Kuimarisha Shughuli za Shirika la Viwanda Vidogo – SIDO: Mapendekezo yamelenga kuifanya SIDO kuwa ndiyo chombo muhimu katika kuleta mageuzi ya viwanda nchini;
- kuendelea kujenga viwanda vinavyotumia malighafi kutoka nchini ikiwemo kilimo, madini na gesi asilia;
- kuendeleza viwanda vitakavyozalisha bidhaa mbadala wa zile zinazoagizwa kutoka nje ya nchi;
- viwanda vitakavyotoa ajira kubwa kwa makundi yote ya jamii;
- kuhakikisha upatikanaji wa mitaji ya kuendeleza viwanda kupitia Benki ya Rasilimali na Benki ya Maendeleo Kilimo na mifuko ya wajasiriamali wadogo;
- Kuanzisha na kuendeleza maeneo ya viwanda (Industrial parks) na maeneo ya Teknolojia (Technological Parks);
- Kuimarisha uanzishwaji na uendelezaji wa kongane za viwanda vinavyotumia malighafi za mazao ya kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi
- Kuimarisha na kuzitumia taasisi za umma katika kuleta mageuzi ya viwanda nchini. Taasisi hizo ni pamoja na: NDC, STAMICO, TPDC, TIRDO, CARMATEC, TEMDO, COSTECH, na Nyumbu na Mzinga.