Tanzania - Mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka 2018/19

Miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP)
  1. mradi wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam;
  2. kiwanda cha kuzalisha madawa muhimu na vifaa tiba;
  3. Dar es Salaam – Chalinze Toll Road.
 
Nashangaa pia! Mbona mleta mada asiweke Uzi huu kwa Tanzania news section. Huko ndiko anaweza hamazisha wenzake na mipango ya viwonder ili wajipange.

Haisaidii Mkenya hii.
This guyz kwani kila kitu hua wanafanya sababu ya kenya?......sababu hata wakijenga barabara ya 2km wanatuletea hapa tuone
 
This guyz kwani kila kitu hua wanafanya sababu ya kenya?......sababu hata wakijenga barabara ya 2km wanatuletea hapa tuone
Je, umeona mpango wa maendeleo wa Tanzania wa 2018/2019?
 

Tupe na ile ya Mlonganzila. Imeanza kufanya KAZI?
 
Miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP)
  1. mradi wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam;
  2. kiwanda cha kuzalisha madawa muhimu na vifaa tiba;
  3. Dar es Salaam – Chalinze Toll Road.
Annael naona unazidi kutunyoosha aiseeeeeh!
 
Annael naona unazidi kutunyoosha aiseeeeeh!
Hapa mambo tuyaweka hadharani. Mtu akitaka kumeza ameze au ateme
Umeiona hiyo Dar es Salaam – Chalinze Toll Road. Imo kwenye mpango
 
4.7.4 Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu

Mkazo utawekwa katika kuendeleza na kuanzisha viwanda vitakavyotoa ajira kwa wingi katika maeneo ya pamba hadi nguo, ngozi na bidhaa za ngozi, na kuongeza thamani ya mazao. Ili kuhakikisha makundi haya yanapata ajira katika maeneo hayo, Mpango utazingatia mambo yafuatayo:-

  1. Kuimarisha upatikanaji wa mitaji ili kujiajiri kwa kuimarisha mfuko wa maendeleo ya vijana;
  2. Kukuza ujuzi na stadi za kazi katika viwanda, kilimo, biashara, utalii, usafirishaji, TEHAMA na madini;
  3. Kutambua ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo.
 
Ninaanza kwenda detailed sasa

Eneo Maalum la Uwekezaji la Bagamoyo
Lengo la mradi ni kujenga bandari ya kisasa ambayo itaiwezesha Tanzania kupokea meli kubwa na kupunguza msongamano wa mizigo katika bandari ya Dar es salaam sawa na lengo la kuiwezesha kuwa lango kuu la biashara za kikanda na kimataifa na kuanzisha eneo maalum la viwanda (Portside Industrial Zone) na ujenzi wa miundombinu wezeshi (barabara,reli, maji, nishati na mawasiliano) na utoaji wa huduma. Katika mwaka 2018/19, mradi unalenga:-

  1. kupata hati miliki ya eneo;
  2. kuanza utekelezaji wa mradi;
  3. ujenzi wa miundombinu wezeshi ya barabara na umeme;
  4. kuanza ujenzi wa kituo cha teknolojia (Technological park).
 
Miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP)
  1. mradi wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam;
  2. kiwanda cha kuzalisha madawa muhimu na vifaa tiba;
  3. Dar es Salaam – Chalinze Toll Road.
BRT ingeweza kabisa yote ikafanywa kama PPP, kuanzia ujenzi, ni mradi ambao uko economical viable.
 

Kituo cha Viwanda cha Kurasini (Industrial Park)

Lengo la Mradi ni kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Mataifa mengine kupitia uwekezaji katika miundombinu ya biashara na ujenzi wa viwanda. Awamu ya kwanza ya mradi huu itahusisha ujenzi wa kituo cha biashara cha kisasa kwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi na awamu ya pili itahusisha ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini. Mradi huu utatekelezwa katika kata za Kurasini Shimo la Udongo, Mivinjeni na Kiungani kwenye eneo la ekari 63. Katika mwaka 2018/19, mradi unalenga:

  1. kukamilisha ulipaji wa fidia kwa wananchi watatu ambao mali zao hazikuthaminiwa awali;
  2. kuanza ujenzi na uendelezaji wa mradi kwa mfumo wa ubia (joint venture).
 
Maeneo Maalum ya Uwekezaji ya Kigoma

Lengo kuu la mradi ni kuwa na eneo maalum la uwekezaji Kigoma lenye bandari huru, mitaa ya viwanda, kongane za utalii na kituo cha biashara na huduma kuiwezesha Tanzania kutumia kwa ufanisi fursa yake ya kijiografia kuhudumia nchi za Kongo, Burundi, Rwanda na Zambia. Katika mwaka 2018/19, mradi unalenga:-

  1. kukamilisha ulipaji wa fidia;
  2. kupata hatimiliki ya eneo;
  3. kuanza ujenzi wa miundombinu wezeshi.
 
MKUKUTA, MKURABITA, Kilimo Kwanza, BRN nk zipo wapi?
 
Hiyo numba 2 ndio itatutenganisha sisi na wale wengine.
 


" Mkazo utawekwa katika kuendeleza na kuanzisha viwanda vitakavyotoa ajira''

Huu mkazo mtaweka lini? Kila kitu kwenyu ni future tense kama tu Bagamoyu...bure kabisa.
 
Upuzi tu. Huu mradi hewa ulianza kabla ya Lamu port na bado mko kwenye ile stage mashuhuri ya Kuzindua. Tena hio ripoti unaweka hapa ni ya mwaka jana kumaanisha project keshasahaulika kam kawaida yenu.
Hahahaha. Tulia unyolewe dogo. Hasira ya nini? Pilipili usiyoila yakuwashia nini?
 
Soma Development Vision 2025, ambayo ni roadmap ya Maendeleo ya nchi yetu, kama ulikuwa hujui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…