SoC04 Tanzania mpya bila usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa za antibiotiki (Antibacterial Resistance)

SoC04 Tanzania mpya bila usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa za antibiotiki (Antibacterial Resistance)

Tanzania Tuitakayo competition threads

stevenmagere5

New Member
Joined
Apr 22, 2024
Posts
1
Reaction score
0
TANZANIA MPYA BILA USUGU WA VIMELEA VYA MAGONJWA DHIDI YA DAWA ZA ANTIBIOTIKI (ANTIBACTERIAL RESISTANCE)

UTANGULIZI;


usugu wa vimelea ni hali na uwezo wa kimelea kuzidi kukua na kuongezeka dhidi ya dawa kwa kutumia dozi sahihi na muda sahihi wa dawa hiyo kwa kuzuia utendaji kazi wa dawa kwa namna tofauti tofauti.

Katika kuazimisha wiki ya uhamasishaji na utoaji wa elimu kwa jamii juu ya matumizi sahihi ya dawa iliyoanza tarehe 18 mpaka tarehe 24 nov mwaka jana ,serikali kupitia wizara ya afya ilitaja usugu wa vimelea dhidi ya dawa kuwa changamoto kubwa inayoisumbua jamii yetu ya kitanzania na dunia kwa ujumla kwa sasa,

Tatizo hili la usugu wa vimelea limepelekea kushindwa kwa matibabu ya ugonjwa kwa kutumia dawa zilizopo hivyo basi kupelekea kuongezeka usambaaji wa vimelea sugu katika jamii zetu,sambamba na hilo vifo vitokanavyo na usugu wa vimelea dhidi ya dawa pia vimeongezeka kwasababu dawa zilizopo hazina ufanisi wa kutibu magonjwa kutokana na usugu wa vimelea, lakini pia kutokana na usugu huo kumekua pia na uongezeko la gharama za matibabu kwa wagonjwa kupitia kulipia dawa zenye bei ghali pamoja na kuongezeka kwa siku za kukaa hospitalini kwa ajili ya matibabu hivyo basi kuipa mzigo wa kifedha jamii yetu na serikali kwa ujumlana kupelekea kurudisha maendeleo nyuma ya jamii zetu.

Hali ikoje?
Katika jarida lililochapishwa na shirika la afya duniani WHO la mwaka 2019 ,shirika hilo lilitangaza usugu wa vimelea dhidi ya dawa kua tatizo kubwa linaloisumbua dunia nzima kwa sasa na kutokana na tatizo hilo makadirio ya vifo takribani 4.95 milioni yametokea kwa mwaka duniani kote,kati ya hivyo vifo takribani 1.1 milioni vikitokea katika ukanda wa chini wa jangwa la sahara,huku ikitaja matumizi mabaya ya dawa kuwa sababu kubwa ya kusababisha usugu wa vimelea dhidi ya dawa hizo

Katika uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa afya kutoka chuo kikuu shiriki cha afya Bugando kati ya mwaka 2020 mpaka 2021 ilionyesha usugu wa kimelea aina ya klebsiella pneumoniae dhidi ya dawa aina ya ceftriaxone kuongezeka kwa ongezeko la asilimia 38% ukifananisha na miaka iliyopita,

Lakini pia katika jarida hilo hilo kulionekana kimelea aina ya salmonella ambae husababisha ugonjwa wa typhoid usugu wake umeongezeka kwa asilimia 39% ukifananisha na miaka ya nyuma.

Katika uchunguzi uliofanywa na shirika la afya duniani (WHO) mwaka 2019 palonekana kimelea aina ya mycobacterium tuberculosis dhidi ya dawa aina ya isoniazid kuongezeka kwa asilimia 10%

Kimelea aina ya E coli kinachosababisha ugonjwa aina ya U.T.I usugu wake dhidi ya dawa aina ya ceftriaxone umeongezeka kwa asilimia 40% tofauti na miaka iliyopita

Sababu ni nini?

Sababu kutokana na mazingira
, katika hili ongezeko na mikusanyiko ya watu imepelekea usambaaji wa kasi wa vimelea katika jamii kutoka mtu mmoja hadi mwingine hivyo basi kuongezeka kwa maambukizi ambayo yanapelekea kuongezeka kwa usugu wa vimelea, uchafu wa mazingira umepelekea kuongezeka kwa maambukizi ambayo pia yanachangia kuongezeka kwa kasi kwa usugu wa vimelea.

Sababu kutokana na dawa pamoja na wagonjwa, katika hili upatikanaji rahisi wa dawa umepelekea matumizi yasio sahihi ya dawa kwenye jamii bila sababu na hivyo basi kuchangia katika ongezeko la usugu wa vimelea na hili linatokana na kutokuwepo kwa sheria inayomuhitaji mfamasia kuuza dawa pale tu mgonjwa akiwa na cheti kutoka kwa daktari,sambamba na hilo wagonjwa wengi hawamalizi dozi za dawa jambo ambalo hupelekea kutokutibu ugonjwa na hivyo basi kuwapa nguvu vimelea katika kutengeneza usugu wao dhidi ya dawa

Sababu kutokana na watoa huduma za afya , katika hili utoaji wa dawa bila sababu sahihi kwa wagonjwa hupelekea kuongezeka kwa matumiazi ya dawa bila sababu kitu ambacho kinapelekea kuongezeka kwa usugu wa vimelea mfano kutibu mafua yanayotokana na virusi kwa kutumia dawa za antibiotiki,kitu ambacho sio sahihi,lakini pia utoaji wa dawa chini ya dozi hupelekea kutotibu vizuri ugonjwa na hivyo kuongeza usugu wa vimelea.

Nini kifanyike?
Katika kupambana na hili janga ushirikiano wa watu katika nyanja na ngazi mbalimbali za afya ni muhimu kuwepo,yafuatayo ni majukumu mbalimbali ambayo yanatakiwa kufanywa na kila mtu katika nafasi yake ili kupunguza na kuondoa tatizo hili la usugu wa vimelea.

Majukumu ya mgonjwa;
-katika hili mgojwa na jamii kwa ujumla inatakiwa kutumia dawa pale tu ambapo kuna maelekezo maalumu kutoka kwa mtaalamu wa afya na kuhakikisha dozi ya dawa inatumiwa na kumalizika katika muda uliowekwa,lakini pia kuhakikisha mgonjwa anafata ushauri wote uliotolewa na mtaalamu wa afya pamoja na kuepuka kugawa ama kutumia dawa na mtu mwingine,

-kuepuka maambukizi ya magonjwa kwenye jamii kupitia njia tofauti kama kunawa mikono na maji tiririka pamoja na kupaja chanjo za magonjwa mbalimbali.,kwa kufanya hivi tutapunguza kasi ya maambukizi ya vimelea hivyo basi kupunguza usugu

Majukumu ya serikali,
-serikali inatakiwa kutengeneza sera mbalimbali ambazo zitasaidia jamii katika kuepuka na kupambana dhidi ya magonjwa mbalimbali kama kuandaa matangazo ya kuelimisha watu kuhusu usugu wa vimelea kupitia televisheni,redio na vipeperushi lakini pia bila kusahau mitandao ya kijamii.

-Serikali inatakiwa kuboresha miundombinu mbalimbali katika sekta ya afya ili kuleta huduma na ushauri wa kiafya karibu na jamii na kwa kufanya hivyo tutapunguza maambukizi ya vimelea kupitia ushauri wa wataalamu wa afya walio karibu na jamii zetu.

-Serikali inatakiwa kukemea vikali tabia za maduka mbalimbali ya dawa ya kuuza dawa kwa wateja bila cheti maalumu cha daktari,sambamba na hili hatua kali za kisheria zifatwe.

Majukumu ya wataalamu wa afya,
-katika hili mtaalamu wa afya anatakiwa kutoa dawa pale ambapo tu kuna sababu sahihi ya utoaji wa dawa na kuacha tabia ya kutoa dawa kwa mazoea mfano kuacha kutoa antibiotiki kwa wagonjwa wenye changamoto za kikohozi kinachosababishwa na virusi

-kutoa ushauri sahihi kuhusu jinsi ya kujizuia kupata maambuziki mbalimbali kama vile kuvaa kondomu,kunawa mikono na maji tiririka pamoja na kupata chanjo.

Hitimisho

Ili kupambana na umasikini katika jamii zetu ni lazima kuwepo na rasilimali watu,usugu wa vimelea unapelekea vifo vingi katika jamii zetu hivyo basi kupunguza rasilimali watu katika jamii,hivyo basi hatuna budi kuungana kwa pamoja kupambana na umasikini kwa kuondoa tatizo hili la usugu wa vimelea katika jamii zetu za kitanzania.
 
Upvote 2
linatokana na kutokuwepo kwa sheria inayomuhitaji mfamasia kuuza dawa pale tu mgonjwa akiwa na cheti kutoka kwa daktari,
Hii sheria ipo bro, utekelezaji wake kikamilifu tu ndio mgumu.

kuepuka maambukizi ya magonjwa kwenye jamii kupitia njia tofauti kama kunawa mikono na maji tiririka pamoja na kupaja chanjo za magonjwa mbalimbali.,kwa kufanya hivi tutapunguza kasi ya maambukizi ya vimelea hivyo basi kupunguza usugu
Ushauri mzuri, kinga ni bora kuliko tiba.

Katika usugu wa vimelea kuna jambo ninaomba wanasayansi tusaidiane. Ni kwa nini kimelea sugu kwa mgonjwa kisiwe na madhara kwa mtu mzima? Na ni kwa nini usugu hutokea, au kugundulika baada ya kutumia dawa? Je hatuwezi kusema kwamba dawa imeua wapinzani(normal flora) wa wadudu wabaya na ndiyo maana saaa wadudu wabaya wanajitawala kibosi bosii kipedeshee......

Je ni mdudu kama mdudu anaipinga dawa? Au ni mazingira ya mwilini yanayomruhusu kujitawala (kinga, na bila wadudu (sterile body)) Je hatuoni kama ni muda wa kuiingiza sayansi ya micribiome kwenye tiba zetu?
 
Back
Top Bottom