SoC04 Tanzania mpya iondoe dhana ya mfumo dume. Suala la uongozi katika nchi ya tanzania kwa asilimia kubwa dhana yake imejengwa katika mfumo dume

SoC04 Tanzania mpya iondoe dhana ya mfumo dume. Suala la uongozi katika nchi ya tanzania kwa asilimia kubwa dhana yake imejengwa katika mfumo dume

Tanzania Tuitakayo competition threads

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Suala la uongozi katika nchi ya Tanzania kwa asilimia kubwa dhana yake imejengwa katika Mfumo Dume.

Mfumo dume umeanzia katika ngazi ya familia ambayo tangu mtoto anapozaliwa kitu kikubwa kinachoangaliwa ni mtoto gani na endapo atakuwa ni mtoto wa Kiume basi ataitwa ndiye mrithi wa mali na jina la ukoo.

Dhana hii imejengeka katika makabila mengi sana yanayoendeshwa na mfumo huu.

Kwani kuanzia Mtoto anapozaliwa tunauona ubaguzi kwa mtoto wa kike ambae inaaminika kuwa yeye ataolewa na kwenda kwenye koo nyingine kuanzisha familia yake.

Sasa nani wa kumkomboa mtoto wa kike kwenye suala zima la uongozi?

Kwanza lazima Jamii ielimishwe kuanzia ngazi ya chini kabisa kuhusu umuhimu wa mwanamke kupewa nafasi ya kutoa maamuzi kwani wakishirikishwa wanaweza kutoa ushauri mzuri utakaoweza kuisaidia familia.

Hata hivyo mtoto wa kike hajapewa nafasi ya kuendeleza ukoo kama mtoto wa kiume. Nani atabadilisha dhana hii? Jamii lazima ibadilike.

Mtoto wa Kike apewe nafasi tangu anapozaliwa familia ifurahie na ukuaji wake upewe nafasi ya kuongoza na sio wa kuaminishwa kuwa yeye ni wa kuolewa tu na kuendeleza koo za wengine.

Wanawake wana uwezo mzuri wa kuongoza endapo watapewa nafasi.
 
Upvote 5
Back
Top Bottom