SoC04 Tanzania mpya, yenye maendeleo ijengwe katika hali hii

SoC04 Tanzania mpya, yenye maendeleo ijengwe katika hali hii

Tanzania Tuitakayo competition threads

Edson Eagle

Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
30
Reaction score
12
Tanzania ni nchi yenye raia wachapa kazi wenye ubunifu na wanaopambana katika kuleta maendereo ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla isipokuwa kuna mambo yanayowaangusha kila wakati ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi.
Tuyaache hayo twende kwenye mapendekezo ya nini kifanyike sasa.

1. Kuenderea kuboresha nyanja za usafirishaji wa malighafi, bidhaa pamoja na watu. Hapa naongerea bandari, viwanja vya ndege, treni mwendo kasi pamoja na barabara. Serikali ihakikishe maeneo haya yapo katika ubora unaoendana na wakati ili kurahisisha nakuongeza kasi ya uzalishaji na utendaji kazi katika maeneo mbalimbali. Tumekuwa tukiona baadhi ya nyanja za usafiri zikikwamisha shughuri zakijamii ktk maeneo tofauti tofauti hivyo viongozi walifanyie kazi hilo.
Screenshot_20240513-075639.png


2. Niwakati wa serikali kuweka nguvu zaidi katika elimu ujuzi (fani). Ikiwa ni pamoja nakuandaa shule na madarasa yakutosha yenye sifa na vifaa vya fani mbalimbali, bila kusahau walimu waliobobea katika fani mbalimbali ili kuwajenga wanafunzi katika msingi mzuri tangu wakiwa elimu ya msingi kwaajiri yakuja kutatua changamoto mbalimbali katika jamii, bila kusahau wawe na uwezo wa kujiajiri pia. Ikumbukwe kuwa elimu ya vitendo ni bora zaidi kuliko elimu ya nadharia.
InCollage_20240512_223621087.jpg


3. Viongozi bora nasio bora kiongozi. Serikali inajukumu pia lakuhakikisha viongozi wanaosimama katika sekta mbalimbali nchini wanafanya kazi sawasawa na matarajio ya nchi inayohitaji maendereo. Hakuna maana yakuwa nakiongozi katika eneo halafu wananchi wanamiaka mitano wanalilia kituo cha afya, shule au maji kisa yeye kiongozi hawaathiriwi na hizo changamoto. Tuwe na viongozi ambao wanawajibika na pale jambo linapokuwa gumu basi wananchi wawekwe wazi kwamba serikali imeshindwa wajue.
Screenshot_20240513-131049.png


4. Kuhakikisha kunakuwa na uhuru wa vyombo vya habari kwa kuzingatia sheria na wajibu bila kukiuka haki za binadamu wala kuvuka mipaka. Lakini pia kuhakikisha usalama wa waandishi wa habari pamoja na mali zao. Ikumbukwe vyombo vya habari ndio mahara pekee ambapo wananchi wanaweza kupaza sauti nakutoa kero zao ili kuinusuru jamii katika changamoto mbalimbali, lakini pia ndio vyombo pekee vakutuhabarisha juu ya mbalimbali yanayoenderea hapa nchini.
InCollage_20240512_223459181.jpg


5. Kuenderea kuboresha katika sekta ya michezo. Hapa naongerea viwanja vya michezo mbalimbali, shule zakuinua vipaji mbalimbali pamoja na miundombinu ya kisasa mfano taa za kisasa za uwanjani, nyasi bandia, VAR, dronsi n.k itakayoperekea kuleta maendereo makubwa zaidi katika michezo mbaimbali isiwe mpira wa miguu tu bado kuna haja yakufufua nakutia motisha hata katika michezo mingine pia ambayo tunaona kabisa imefifia mfano basketball n.k.
Screenshot_20240513-131539.png


6. Kuweka mazingira yatakayo wafanya watanzania kukutana na watu mbalimbali wa mataifa mengine yaliyoenderea duniani, nakujadiri masuala mbalimbali ikiwemo elimu, siasa, uchumi, viwanda, biashara na kilimo. Lengo nikujenga uhusiano mzuri, kuibua fikira za ubunifu, kujiamini na kujifunza mambo mbalimbali kutoka nje ya Tanzania. Mazingira haya yanaweza kuwa nkutokana na interview, mikutano na matamasha mbalimbali yatakayohusisha uwepo wa watu mbalimbalo kutoka mataifa mengine nje na Tanzania. Vilevile hata kupitia vyuo vikuu vyenye hadhi.
InCollage_20240512_223955938.jpg


NIHITIMISHE KWA KUSEMA PENYE NIA DAIMA PANA NJIA UONGOZI BORA SIASA NZURI NA WATU NDIO NGUVU YA MAENDELEO.
MUNGU AZIDI KUIBARIKI NA BAADA YAKUPENDEKEZA HAYO BASI KAZI IENDEREEE.
 
Upvote 1
Kuenderea kuboresha nyanja za usafirishaji wa malighafi, bidhaa pamoja na watu. Hapa naongerea bandari, viwanja vya ndege, treni mwendo kasi pamoja na barabara. Serikali ihakikishe maeneo haya yapo katika ubora unaoendana na wakati ili kurahisisha nakuongeza kasi ya uzalishaji na utendaji kazi katika maeneo mbalimbali. Tumekuwa tukiona baadhi ya nyanja za usafiri zikikwamisha shughuri zakijamii ktk maeneo tofauti tofauti hivyo viongozi walifanyie kazi hilo.
Nchi nzima iunganike, ifanye kazi kama mnyama mmoja, a single organism.

Kuweka mazingira yatakayo wafanya watanzania kukutana na watu mbalimbali wa mataifa mengine yaliyoenderea duniani, nakujadiri masuala mbalimbali ikiwemo elimu, siasa, uchumi, viwanda, biashara na kilimo. Lengo nikujenga uhusiano mzuri, kuibua fikira za ubunifu, kujiamini na kujifunza mambo mbalimbali kutoka nje ya Tanzania.
Myama huyo anakula vitu vipya tokea pote duniani, na kuachana nq vua kozamani vilivyopitwa na wakati visivyo na manufaa tena
 
Back
Top Bottom