Tanzania, UN Tourism Zasaini Makubaliano ya Kongamano la Kimataifa la Utalii wa Vyakula Barani Afrika

Tanzania, UN Tourism Zasaini Makubaliano ya Kongamano la Kimataifa la Utalii wa Vyakula Barani Afrika

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

TANZANIA, UN TOURISM ZASAINI MAKUBALIANO YA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UTALII WA VYAKULA BARANI AFRIKA

Na Mwandishi Wetu- Madrid, Hispania

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Utalii Duniani la Umoja wa Mataifa (UN Tourism) zimesaini mkataba wa makubaliano utakaoifanya Tanzania kuwa mwenyeji wa Kongamano la Pili la Kikanda la Utalii wa Vyakula la Shirika la Umoja wa Mataifa (The 2nd UN Tourism Regional Forum on Gastronomy Tourism for Africa) linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Machi 11 hadi 13, 2025.

Hafla ya utiaji saini imefanyika kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Zurab Pololikashvili katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika la Utalii Duniani la Umoja wa Mataifa jijini Madrid, Hispania leo Januari 24,2025.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Chana amesema Tanzania inafuraha kuwa mwenyeji wa kongamano hilo linalotarajia kukutanisha washiriki zaidi ya 300 kutoka mataifa mbalimbali duniani na kwamba kupitia kongamano hilo Tanzania itajifunza kutoka mataifa hayo namna wanavyofanya katika kukuza utalii wa vyakula.

“Kupitia Kongamano hili tunataka kuwajengea uwezo wapishi wetu jinsi ya kutengeneza aina tofauti za vyakula ili watalii wanapokuja waweze kufurahia vyakula vya nyumbani kwao lakini pia tunahitaji kuona ni fursa gani zitakazotokana na kongamano hilo ili tuweze kujifunza utangazaji utalii wa vyakula” Mhe. Chana alisisitiza.

Mhe. Chana amefafanua kuwa Tanzania na UN Tourism zimekuwa zikishirikiana katika masuala mbalimbali kwa lengo la kukuza utalii.

“Miongoni mwa maeneo tunayoomba ushirikiano kwa sasa ni katika masuala ya sera na ukuzaji ujuzi, Rasilimali Watu na Mpango Mkakati wa Kukuza Utalii” alisema Mhe. Chana.

Katika hatua nyingine, Mhe. Chana alisema Tanzania inatambua na kuthamini jukumu muhimu la Shirika la Utalii Duniani la Umoja wa Mataifa (UN Tourism) katika kuunda sera za kimataifa za utalii,kukuza utalii endelevu na kukuza ukuaji wa uchumi.

Naye, Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Zurab Pololikashvili alisema kuwa Shirika la Utalii Duniani limelenga kuitangaza Afrika kama sehemu ya utalii inayofikika sambamba na kutangaza utalii wa vyakula.

Katika kufanikisha kongamano hilo, Bw. Pololikashvili amependekeza kwa Tanzania kutumia njia zote za mawasiliano ili kulitangaza kongamano hilo ikiwa ni pamoja na kutumia watu maarufu wenye ushawishi katika jamii na kuwatumia wapishi wa vyakula mbalimbali vya kiafrika.

“ Pia ningeiomba Tanzania kuhakikisha zoezi la upatikanaji wa viza pamoja na usafiri wa anga kwa ujumla linakuwa rafiki kwa waombaji wanaotarajia kusafiri kuja kwenye kongamano hilo” amesisitiza Pololikashvili.

Mkutano huo umehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Mhe. Balozi Ramadhani Dau, Balozi wa Tanzania nchini Hispania, Mhe. Balozi, Ali Jabir Mwadini, Mkurugenzi wa Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Thereza Mugobi, Mjumbe wa Bodi ya TTB, Said Kamugisha na Afisa Balozi, Amos Tengu na sekretarieti ya Shirika la UN Tourism.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-01-24 at 12.32.11.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-24 at 12.32.11.jpeg
    186.1 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2025-01-24 at 12.32.11 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-24 at 12.32.11 (1).jpeg
    179.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2025-01-24 at 12.32.12.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-24 at 12.32.12.jpeg
    187 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2025-01-24 at 12.32.12 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-24 at 12.32.12 (1).jpeg
    214.9 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-01-24 at 12.32.12 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-24 at 12.32.12 (2).jpeg
    204 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-01-24 at 12.32.12 (3).jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-24 at 12.32.12 (3).jpeg
    220.8 KB · Views: 2
  • CAPTIONS-MADRID.docx
    CAPTIONS-MADRID.docx
    13.1 KB · Views: 1
Nchi ya Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Jukwaa la pili la vyakula vya asili kwa ukanda wa Afrika ambalo linatarajiwa kufanyika April 23-25 , 2025 Jijini Arusha.
IMG_1193.jpeg

Akizungumza February 19, 2025 na vyombo vya habari kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa uamuzi wa Tanzania kuwa wenyeji wa Mkutano huo ulikuja baada ya kupitishwa kwenye jukwaa la kwanza.

Amesema kwamba katika Mkutano huo unaoratibiwa na Shirika la Utalii duniani Kanda ya Afrika unatarajiwa kuwapokea wageni zaidi ya 300 kutokea maeneo mbalimbali Duniani hususani mataifa ya Afrika na Umoja wa Mataifa (UN).

Pia amesema Jukwaa hilo litaambatana na matukio mbalimbali ikiwemo mijadala na maonesho ya vyakula mbalimbali vya asili.

Aidha amesema kwamba litakuwa chachu ya fursa mbalimbali kwa watanzania ikiwemo kuonesha namna Tanzania ilivyojaaliwa aina tofauti za vyakula vya asali hususani kutoka kwenye makabili zaidi 120, lakini pia ameongeza kwamba itakuwa fursa ya kuwavutia watalii.

Mkutano huo ni kati ya mikutano mikubwa ambayo itakuwa imefanyika nchini Tanzania katika kipindi kifupi cha miezi minne tokea mwaka 2025 ulipoanza, ambapo itakumbukwa mwishoni mwa Mwezi January 2025 Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nishati Afrika (M300) ambao uliwaleta pamoja wadau mbalimbali.
 
Back
Top Bottom