Tanzania na Africa tunajifunza nini kwa mapinduzi ya Guinea?

August

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2007
Posts
9,327
Reaction score
5,206
Guinea PM Surrenders to Coup Leaders
By Scott Stearns
Dakar
25 December 2008



Guinean Prime Minister Tidiane Souare (file photos)

 
Guys Mr. Camara did the right thing and no one knows his intention but so far he handle the situation very well because guys most of this African Old fashion leaders they want to die in power and that is all they care power power power and the worst part is they don't make any changes to their countries so in a long run Mr.Camara present a hope so far again no one knows his intention and hope a positive change is coming soon.sometime you rather have Mr.Camara lead the country than Grandfather Mugabe and hope someone like him will take over na kule kwa babu Mugabe and send him somewhere in exile.
 
Ahh sie ni nchi ya amani na utulivu.Hayo yanawatokea wenzetu tu sio sisi.Tuna chama tawala imara,kimekuwa kikiwajali wananchi tangu kizaliwe 1977,tuna rais ambaye jitihada zake za kuleta maisha bora kwa kila mtanzania zinaonekana,na watumishi wa umma (including wanajeshi) wanapatiwa mishahara ya kutosha na hawadai malimbikizo yoyote.....wishful thinking,of course.Well,watawala wetu wako busy sana na kuifisadi nchi yetu wala hawajali yanayotokea kwingineko.Wanasahau kwamba wanyonge wakiungana wanaweza kuiondoa dola madarakani kwa njia yoyote ile
 
Guinea junta seeks to allay fears

Capt Camara says he wants to rid Guinea of corruption


HAVE YOUR SAY We need a change, change that will benefit all Guineans. We pray for a good leader
Amara, Nzerekore



Celebrations in Conarky

 
Camara says his ruling council of six civilians and 26 soldiers will organize "free, credible, and transparent" elections in December 2010. He said soldiers have no wish to cling to power and he will not be a candidate in that election.

- I mean so far sijaona all the facts za the whole ishu, lakini I do not like this quote, miaka miwili kuandaa uchaguzi? Somebody please help me Why two years?
 
Another Yahya Jammeh in the making. Akionja utamu hatoki hapo.
 
..lakini Raisi Kikwete si askari mstaafu.

..labda Guinea wangejifunza toka kwetu.
 
Hakuna cha kujifunza kwani hii ni mara ya kwanza kutokea mapinduzi barani Africa?

Kama kuna cha kujifunza basi ni kuwa it's time to move on.
 
Kuna cha kujifunza pale Guinea?, sie tumepita huko siku nyiiingi sana.
Jamaa Conteh kufia kwenye kigoda cha Ikulu si suala ambalo waTanzania tunalielewa kirahisi.
 
- I mean so far sijaona all the facts za the whole ishu, lakini I do not like this quote, miaka miwili kuandaa uchaguzi? Somebody please help me Why two years?

mwaka mmoja wa kujipongeza kwa "risk" aliyochukua, na wa pili kujitayarisha kuachia madaraka (kama kweli nia hiyo ipo).
 
funzo ni kwamba japokuwa "coup d'etat" zimepitwa na wakati na zinapingwa duniani kote bado zinawezekana hususan pale serikali "inapowatelekeza" wananchi wake.
 
Huyu Kamara sii leo amesikika akijitetea kwa Wade ktk simu eti atakaa tu kwa miezi 8 ndo uchaguzi? Na istoshe eti hatagombea uraisi!! Sasa tuamini lipi? la 2 years au 8 months? Hawa jamaa mara nyingi hawaaminiki!
We wait and see!
 
FMES,
Mkuu wangu ina make sense sana tu. Hivi kweli unafikiria yakitokea mapinduzi Tanzania na jeshi likaruhusu uchaguzi baada ya miezi michache, hivi kweli CCM watashindwa uchaguzi huo!..
Kisha kama rais wetu anaweza kupatwa na kifo cha ghafla mrithi wake wa kiti cha Urais anaweza kuzua balaa kama la Guinea.
Kulingana na habari nilivyosikia mimi BBC, huyo Conte mwenyewe alichukua nchi kwa mapinduzi akawaahidi wananchi changes na yote mazuri ya maendeleo kwa watu wote lakini toka ameshika madaraka hakuna changes isipokuwa kuendeleza Utawala wa asili ya mwafrika -Mabavu..
Sasa napokwama ni kuelewa ni pixcha nzima ya Mapinduzi haya walilaumu Utawala ambao wamekuwa wakiutumikia miaka yote hadi kifo chake. Je, Tatizo ni sheria ya nchi yao ambayo kikatiba aliyetakiwa kurithi kiti cha urais ni Speaker wa Bunge!..Na huyu mzee hana washabiki kabisa kwani inasemekana ni sawa na Mh. Six...
 
Mkuu wangu ina make sense sana tu. Hivi kweli unafikiria yakitokea mapinduzi Tanzania na jeshi likaruhusu uchaguzi baada ya miezi michache, hivi kweli CCM watashindwa uchaguzi huo!..

- Mkuu Bob, kama this is the point basi CCM izuiwe kugombea maana hapa nia itakuwa kuinyima ushindi sasa kwa nini uiruhusu kugombea kama wananchi wanaitaka?, lakini ninaamini miezi sita tu inatosha kwa wenye nia njema na taifa,

- Nimesoma all the facts sasa, sawa ilikuwa ni muhimu sana in this case ya Guinea kwa Camara, kuingilia kati lakini hii ya kusubiri miaka miwili haina mshiko hata kidogo, miezi sita tu inatosha.
 
FMES,
Tatizo la Guinea ni sawa na CCM leo kuna mtandao ndani ya uongozi wa nchi ile kwa hiyo uchaguzi unalenga zaidi watu fulani na sio chama kwa ujumla. Wapo wazee asilia ambao hawatakiwi kushika madaraka na kulingana na habari hao wazee ndio kipenzi cha wananchi..
kwa hiyo hata hapa nyumbani huwezi kuzuia CCM kama chama kwa sababu karibu kila mtu ni mwanachama wa CCM iwe asili ama wa kuja...Na huwezi kuwaondoa CCM kwenye Uchaguzi nchi za Ulaya hazikakuacha na ndilo linalotendeka huko Guinea wameshaanza kupiga kelele kwa sababu (kulingana na fununu) yale madini ya kutengenezea Aluminium yanatakiwa sana na kuna hatari ya viongozi hawa kubatillisha Mkataba uliotangulia.
 
- Bob mimi ninavyowasoma hawa Guinea, ni kwamba hawa wanajeshi wana tatizo kubwa kwa sababu either wakae kwa muda mrefu au wawape hao hao waliowapindua sasa ili waishie kuwaua wao wenyewe wanajeshi kina Camara,

- Inaonekana wengi wa juu hawakufurahishwa sana na haya mapinduzi, halafu kuna tatizo sana junior officers wanapochukua nchi, maana senior hawatalala mpaka wajibu mapigo kama vile Liberia na Doe,

Anyways, binafsi siungi mkono mapinduzi kwa siku za sasa, maana tatizo lake ni kwamba huwezi ku-draw the line yataanzia na kuishia wapi, unless wazungu waingilie kati.
 
Ni rahisi sana kwa Tanzania kupinduliwa na Macaptaini kuliko Majenerali wanaokula Bure na kwenda chooni bure hapa Tanzania. Macaptain walitikisa kiberiti mwaka fulani wakaishiakukopeshwa magari wakaridhika. Lakini nijuavyo mimi kundi la makepteni ndo kundi la wanajeshi wengi walo irudi shule.

Kwamba kunaweza kutokea mapinduzi nchini Tanzania? Ndiyo kuna possibility hiyo. Lakini sioni Brigedia au Generali yeyote mwenye hamu ya kufanya hivyo.

Mapinduzi ni jambo zuri?Sina uhakika, nijualo ni moja kwamba ubadhirifu wa mali ya umma na Ufisadi ni kati ya mambo yawezayo kuzaa wazo la kupindua serikali.
Wengi wa Makepteni hali zao huwa mbaya pale tu watakiwapo kustaafu, kwani wao hustaafu wakiwa na miaka 50. Kwa tabia zao kwamba wengi wao wameoza kwa chini na hivyo huchelewa sana kuoa,mara nyingi hustaafu wakiwa waya huku watoto wao wakiwa bado chekechea.
 
JIPYA ni kuwa Uncle Captain Camara katangaza kuwa sampuli ya kina EPA huko Guinea itakuwa chakula cha risasi kuanzia sasa. CCM na Mwenyekiti wake na ubavu kwa hili.

Vilevile Camara kaamua mikataba yote ya uchimbaji madini ya almasi, dhahabu, bauxite na uranium ipitiwe upya a itakayoandikwa iwe na faida kwa wa Guinea wa kawaida na sio watu wachache tu!

Naunga mkono mapinduzi ya Guinea kwa mikono na miguu miwili na ninaanza kujifunza Kifaransa nikachangie maendeleo ya nchi ambayo nadhani sasa imeondoa gia ya rivasi na imeshaweka gia namba moja! Mbele kwa mbele.... Bonjour Guinea, j'arrive bientoit!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…