Tanzania na baadae yake

Tanzania na baadae yake

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Nidhamu katika uongozi ni jambo muhimu sana. Bila nidhamu uongozi unakuwa shida na usiokuwa na mwelekeo. Ni muhimu sana kufahamu hili. Ili taifa lolote liendelee viongozi wake lazima wawe na nidhamu.

Kwakuwa bila viongozi kuwa na nidhamu itakuwa vigumu sana kwa raia kuwa na nidhamu. Ni muhimu kufahamu kwamba nidhamu huleta utii na utii huleta order.

Kwahiyo nidhamu kwa watu wetu wote ni muhimu sana kwakuwa bila nidhamu hakuna utii wa sheria. Utawala unakuwa mgumu sana pasipo nidhamu.

Jukumu letu kama taifa tulilonalo kwa sasa ni kuipanga nchi kwaajili ya maendeleo jukumu hili ni la kila mmoja wetu. Hili halitowezekana kama hakutakuwepo uongozi wenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo hayo.

Jambo la msingi na la kwanza ni uwepo wa uongozi wenye dhamira ya kweli na ya dhati ya kuleta maendeleo ya watu wetu na ya taifa kwa ujumla.

Ni wazi hili haliwezi kufanikiwa pasipo ushiriki wa wananchi wenyewe kwakuwa hili ni taifa lao na watajivunia pale watakapo shiriki moja kwa moja kuleta maendeleo yao wenyewe na sio kuletewa.

Fikra hizi za serikali kufikiria itawaletea wananchi maendeleo bila ushiriki wao ni fikra potofu. Wananchi lazima wahamasishwe kuwa na fikra za kulipenda na kulitumikia taifa lao na sio kinyume chake cha kuisubiri serikali. Serikali inachotakiwa ni kuonyesha uongozi tu lakini gurudumu la maendeleo liko kwa wananchi wenyewe ndio wanao lishikilia taifa kuendelea kwa taifa kutategemea sana juhudi zao na ushiriki wao katika ujenzi wa taifa.

Wakati umefika sasa wa kufundisha watoto wetu kulipenda taifa hili na kuwa tayari kulitumikia. Naongea haya nikiwa na ufahamu wa kutosha kuhusu hali halisi ya taifa letu lilipofikia. Nidhahiri tunahitaji dawa dhidi ya ubinafsi ili kuleta watu wa taifa hili pamoja katika malengo yetu.

Ufisadi na rushwa vimetawala na hakuna mtu anayejali taifa hili tumekuwa watu wa binafsi hatuishi kama taifa. Tumeondoka katika njia iliyo sahihi. Ni muhimu sasa kufundisha watu wetu kutumikia. Na kuhifadhi misingi ya haki. Tumebomoa misingi ambayo hujenga taifa lolote imara. Misingi ya kutumikiana na utu. Siasa yetu imeharibika imekuwa ya watu wanaotafuta pesa badala ya kutumikia hizi ni changamoto za wetu tunahitaji kuzitatua na vijana wa taifa hili ni lazima wazijue.

Changamoto hizi hazitoondoka pasipo sisi kuchukua hatua na kubadilisha mwelekeo tulionao. Ili tujenge taifa bora kwaajili ya vizazi vijavyo. Hili linawezekana kama tukiwa wamoja. Na kama elimu yetu ikitengenezwa si kwaajili ya manufaa binafsi ya mtu bali kwaajili ya ukombozi wa umma. Ni lazima tujenge jamii ya watu wanaotumikiana.

Ni muhimu sasa kuleta uthamani wa uraia wetu na utanzania ambao umeanza kuondoka kwa wananchi wengi. Hili jambo linawezekana kama tukithaminiana na kuheshimiana na kama tutafanya kazi pamoja kukabiliana na changamoto nyingi tulizonazo. Tunauwezo wa ku design taifa hili kuwa miongoni mwa mataifa bora sana duniani ikiwa tutapendana na ikiwa tutakuwa tayari kukabiliana na changamoto zinazotukabili kwa pamoja na kwa roho ya dhati bila unafiki.

Ni lazima tuwe na fikra moja linapokuja suala la ujenzi wa taifa hili. Kwasababu bila kuwa kwetu wamoja taifa hili halitoendelea. Naamini kila mtu ana uwezo wa kuchangia katika maendeleo na ujenzi wa taifa hili. Wazazi lazima watambue qana umuhimu wa pekee katika ujenzi wa taifa hili kwa kuwaingizia utaifa na uwajibikaji watoto kwa taifa lao.

Kila mtu katika taifa hili lazima ajue ana wajibu tatu muhimu. Wajibu kwake binafsi na kwa familia yake, wajibu kwa jamii iliyomzunguka na wajibu kwa taifa. Wajibu hizi tatu ni muhimu kwa ukuaji wa taifa lolote linalotaka kuendelea.

Kwahiyo kazi ya kiongozi ni kupanga watu na kuweka uongozi kuanzia ngazi ya chini ambao watawajibika kwa watu. Ni lazima kuwepo na kuaminiana kati ya wanaoongoza na wanaoongoza pamoja na nidhamu na uaminifu. Tunahitaji wananchi wawasikilize viongozi wao na wawe well informed katika kila kitu kitakachohusu taifa lao, vitongoji vyao na mitaa yao.

Kitu kimoja ambacho kila mmoja wetu lazima afahamu pasipo kulipenda taifa letu hatutapata maendeleo ni lazima kwanza tulipende na tuwe tayari kulitumikia. Kama tutalipenda taifa letu hatutakuwa tayari kufanya chochote ambacho kitakuja kuangamiza taifa letu.

Ni muhimu kufahamu kwamba ubinafsi na rushwa huondoa umoja wa taifa lolote na kuleta mgawanyiko na huzalisha vita na vurugu. Kama tunalipenda taifa hili hatutafanya mambo hayo kwasababu faida yake ni ya kipindi kifupi lakini madhara yake ni ya muda mrefu na sidhani kama tuko tayari kuhatarisha umoja na amani ya taifa letu tukafanya familia zikasambaratika na mfumo wa kijamii kuharibika kwasababu ya faida ya muda mfupi ya ufisadi na rushwa.

Taifa la watu wezi na mafisadi haliwezi kuwa na amani hata kidogo. Wakati umefika sasa tupende haki na tuwe tayari kuitumikia. Tutalijenga taifa hili kuwa imara kwa kutumikiana na sio kwa ubinafsi. Ni lazima tupendane kama watu wa taifa moja. Tuwe tayari wakati wa vita kupambana pamoja na wakati wa amani kulijenga pamoja taifa letu. Kwa njia hii pekee mungu wetu atatufanya tuwe imara. Sio katika ubinafsi na ulafi. Haya ni matumaini yangu kwa watanzania wote .Ni wakati sasa wa kuamka na kujitambua. Ni wakati sasa wa kuamka na kujua nafasi yetu ni ipi katika dunia.

Kama mmbuyu ukuavyo na sisi tunaweza kukua ni jitihada zetu na umoja wetu , ni muhimu kushikamana kwakuwa katika hili ndipo kuna tumaini la pekee. Kina kaka na kina dada, kina mama na kina baba wakati utafika ambapo watoto wote wa taifa hili watajivunia kuwa watanzania. Roho ya utanzania itasambaa kwa kila mwananchi mkulima kwa mfanyakazi na wote tutakuwa tayari kulitumikia taifa hili. Tutalijenga taifa hili kwa fikra sahihi na matendo yaliyo sahihi.

Sisi wa kizazi hiki tunawajibika kwa kizazi kijacho ni lazima tumalize changamoto zetu ni lazima tutengeneze mazingira bora kwa kizazi kijacho na tuache kurithisha matatizo yetu kwa kizazi kinachokuja ni muhimu kuwapa ahueni kizazi kijacho ni lazima tumalize matatizo yetu.

Hili jambo liko mikononi mwetu tuna uwezo nalo kama tutakuwa ni wenye akili na bidii na kama tutaachana na uvivu wetu.

Bado naamini kuna matumaini kwa taifa hili kuwa kubwa. Tuna watu na tuna ardhi pamoja na maliasili. Tutengeneze siasa zetu ziwe bora ili kiwe chombo cha ukombozi wetu badala ya mgawanyiko. Dhamira ya dhati na elimu kwa watu wetu italikomboa taifa hili.

Kwa wanasiasa wote na kwa wananchi wa taifa hili ni muhimu sana kutafakari haya mambo ya msingi kwa mustakabali wa taifa letu. Nafahamu kuna watu wengi wameingia kwenye siasa ambao dhamira zao sio ukombozi wa watu wa taifa hili bali faida binafsi ni changamoto tuliyonayo kwa sasa ambayo raia mwema mwenye fikra nzuri anaiona na hiki ndicho chanzo cha kukosa mwelekeo kwetu. Hawa watu wameyumbisha nchi sana tunawajua na tunawaona wakati wao haijafika bado.

Nawaomba watanzania waendelee kuwa na matumaini na taifa lao bado kuna njia tutapita tu bado kuna matumaini changamoto hizi taifa lolote lazima lipitie ili watu wake bora waliosahauliwa waibuke. Kama dhahabu ipitishwavyo kwenye moto ndivyo taifa lolote lazima lipitie ili liwe imara na watu bora waibuke. Tutasimama imara ba tutachukua nafasi yetu katika dunia naomba mniamini. Hili halitofanikiwa pasipo kuwaondoa wanasiasa waovu nchini.
 
Back
Top Bottom