Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Kidijitali ya Comoro, Muinou Ahamada.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Balozi Yakubu alimueleza Mtendaji Mkuu Bwana Ahamada kuhusu hatua kubwa ambazo Tanzania imepiga katika kuhakikisha nchi inanufaika na uchumi wa kidijitali ambapo mpaka hivi sasa mapato ya Serikali yamekuwa yakiongezeka kutokana na malipo kufanyika kwa mifumo maalum iliyowekwa. Alimueleza pia uwepo wa mifumo ya utendaji kazi Serikalini ambayo imesaidia kupunguza gharama na kuongeza ufanisi kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake, Bwana Ahamada alieleza utayari wa Comoro kushirikiana na Taasisi za Tanzania kama vile Wakala wa Mtandao Serikalini ( EGA), TCRA ili kuona namna ya kuimarisha Taasisi zao.
Soma Pia: Tanzania na Comoro zajadiliana kuongeza ushirikiano katika Sekta ya Elimu
Aidha, alitoa wito kwa Taasisi binafsi za Tanzania kuangazia fursa za ushirikiano Comoro kwani yako maeneo kadhaa yanatohitaji uwepo wa Sekta binafsi.