Tanzania na India wajifungia kuujadili uhalifu unaovuka mipaka

Tanzania na India wajifungia kuujadili uhalifu unaovuka mipaka

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Jeshi la Polisi nchini linaendelea kuchukua tahadhari katika kuzuia uhalifu unaovuka mipaka ukiwemo uhalifu wa mitandao na ugaidi ambapo kupitia ushirikiano wa Tanzania na India wamekubaliana kushirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa mafunzo kwa Askari Polisi na vifaa vya kisasa.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Dkt. Maduhu Kazi wakati wa mkutano wa pili wa pamoja kati ya Tanzania na India katika mapambano dhidi ya uhalifu uliowashirikisha Maafisa kutoka Jeshi la Polisi Tanzania na maafisa kutoka nchi ya India.

Dkt. Maduhu alisema Makosa yanayotokana na uhalifu unaovuka mipaka yameendelea kuwekewa mkazo na mikakati mbalimbali na Jeshi la Polisi Tanzania ili makosa hayo yaweze kudhibitiwa kabla hayajatokea na kuifanya nchi yetu kuendelea kuwa salama.
Kwa upande wake Kamishna wa Intelejia ya Jinai ambaye alimwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, CP Charles Mkumbo alisema katika kikao hicho watatilia mkazo makosa yanayovuka mipaka na kutoka na maazimio ya kutekeleza ili kuzuia makosa hayo.

Alisema, Jeshi la Polisi pia litaendeleza ushirikiano uliopo na India hususani katika mafunzo kwa Askari Polisi ili kuukabili uhalifu kwa njia ya mtandao ambao umeendelea kuwa changamoto ambapo nchi ya India imepiga hatua katika kuuzuia kutokana na matumizi ya teknolojia za kisasa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Kamati ya Pamoja ya kupambana na ugaidi kutoka Wizara ya Mambo ya nje ya India, Balozi Kishan Dewal alisema mkutano huo wa pili unafaida kubwa kwa nchi zote mbili hususani katika kuzuia na kupambana na uhalifu unaovuka mipaka.
Balozi Dewal alisema pia kikao hicho kitajadili matumizi ya teknolojia mpya pamoja na kuweka mikakati mipya ya kuzuia uhalifu.
 
Back
Top Bottom