waltham
JF-Expert Member
- Jan 23, 2014
- 2,522
- 1,045
Filamu zenye tafsiri ya Kiingereza kibovu zinatudhalilisha
SHARE
BOOKMARK
PRINTEMAILRATING
Posted Jumapili,Novemba30 2014 saa 12:57 PM
KWA UFUPI
Watazamaji hao hawasemi Kiingereza cha wasanii wa filamu hii ni kibovu bali wanasema "Watanzania bwana, kweli ni mbumbumbu hebu angalia hicho kinachopita kwenye ‘screen'. Hii ni kutudhalilisha sisi Watanzania hasa wale ambao wanajua wangeweza kuweka tafsiri za Kiingereza sahihi kwenye filamu hizo.
Pengine hilo linahitaji kujitokeza kwa watu wenye uwezo wa kutunga hadithi nzuri, kuandaa misuada mizuri na watu wengine wenye weledi katika nafasi mbalimbali za sanaa hiyo. Pamoja na hayo kwa kiwango fulani filamu zetu na wasanii wanakubalika hapa nchini na nchi nyingine za jirani. Hivyo kwangu mimi siwezi kusema kuwa viwango hivyo vya chini vinatudhalilisha. Kinachonisikitisha ni Kiingereza kibovu kinachotumika kutafsiri filamu za kiswahili. Huu ndio naona ni udhalilishaji, na ni udhalilishaji unaoweza kuepukika. Ni kwa nini katika nchi hii iliyo na watu wanaojua lugha ya Kiingereza vizuri iwe na filamu za kiswahili zenye tafsiri ya Kiingereza inayotia aibu kiasi hiki? Mimi najisikia vibaya sana ninapoangalia filamu hizo na kusoma tafsiri hizo zinazodhalilisha.
MSEMAJI UMENENA UKWELI MTUPU,SHINDA NI SIKIO LA KUFA HALIKII DAWA.....................................

Mimi napenda uigizaji; uwe katika filamu, vichekesho, maigizo n.k. kama vimetengenezwa katika kiwango kinachoridhisha huwa napenda kuangalia bila kujali igizo hilo limetengenezwa na wasanii wa nchi gani. Ninachoangalia je, ipo katika lugha ninayoijua?, Je, inanifurahisha au kunituliza kwa kiwango ambacho mimi nakitaka? Kwa maana hiyo naangalia filamu na maagizo kutoka katika nchi mbalimbali.zikiwemo zile zinazotengenezwa toka katika nchi yangu Tanzania. Natambua sana kwamba katika sanaa hii bado viwango vyetu vipo chini.